Dilemma ya kumpenda mwanamke mwenye mtoto

Dilemma ya kumpenda mwanamke mwenye mtoto

Aisee mbona tafrani sasa mkuu?
Mwanzoni utasema jamani Mwanamke si ndio huyu? Nilikuwa wapi mimi.

Mkuu niseme ukweli niache utani, Single maza sio wote wabaya, lakini hakikisha unaongea naye Mada ngumu Maana na yeye asije akawa anakupenda kwa hisia Tu ambapo baadaye mtakosna na itakuwa Chanzo cha ugomvi

Mad ngumu ni zipi? Historia ni Muhimu Sana Maana unayofanya Leo ndio hatuna yako ya kesho, aloyofanya zamani yanadefine maisha yake ya Leo, usisikilize wajinga wanaosema forget the past.

1. Kwanini alizaa kabla y Ndoa
2. Kwanini waliachana na Mume wa Mwanzo
3. Mume wa Mwanzo Yuko wapi na nfnu nini?
4. Umweleze kabisa kinaga ubaga kuwa hakuna Mwanaume anatelekeza Mtoto maisha Yote au Mtoto ataacha kumtafuta baba yake

5. Mwambie kwa uswazi huyo Mtoto sio wako, Mamlaka yoote yako kwa Baba Yake na ukoo wao, asikubeshe majukumu yasiyo yako, Maana naona ameshakuingiza kwenye mfumo wake
6. Mwambie Mimi siko tayari kulea Mtoto ambaye ana Baba Yake, Mimi nihenyeke usiku na mchana kuuguza mtoto, kusomesha, kulisha wakati Baba yake mfanya kazi hela Anafanya kulewa, kuhonga na kutombea wanawake wengine? Wewe utakuwa ni Zuzu.
7. Kabla ya kukubaliana kuona wekeni Mipaka ya mawasiliano, Mume mwenzako na yeye na Mtoto, hap Mwanzo atakwambia Hana mawasiliano na hajui alipo, ni uongo mkubwa sana n inaonesha bado kuna mambo anakuficha
 
Usiyumbishwe na maneno ya mitaani kaka. Umempenda na unaona kabisa anakidhi vigezo vyako unanzaje kuuliza watu kaka?

Kuna ma single mother wengi sana wameachana na wazazi wenzao mazima na wameanzisha familia zenye afya sana na wanaume wengine

Hivi kuna hao wasio na watoto wangapi ambao wameolewa na wamekuwa vichomi balaaa kwenye ndoa zao?
Umeongea point nzuri sana mkuu.
Asante sana, nitalizingatia hilo na nitazidi kuangalia mwenendo wake bila ku judge kuwa amesha zaa.
 
Research?
Kuna any paper au tovuti inaelezea kuhusu madhara ya kuoa au kuwa kwenye mahusiano na single mama?

Au research hiyo itanipasa nitembelee sehemu gani ili niweze kupata data rasmi na majibu yaliyo fasaha?
Kwa akili yako research ni mpaka utembelee tovuti?
Huko mtaani ulipo hakuna watu?
Hakuna single mother?
Hakuna waliooa single mother?
Sijajua atakuwa wapi, ila I know mtoto atahitaji huduma pia, na nikisema hilo sio jukumu langu Nitakuwa na jizima data tu, labda kama Nita hakikisha huyo mzazi mwenza yupo na ana kipato kizuri hapo itanilazimu kumwita na kufanya mazungumzo naye juu ya mtoto wake asiye na hatia
Kanye west soma tena ni kitu gani hiki umeandika
 
Wanabodi..

Ni heri mmeamka salama kwenda kuyakabiri majukumu ya siku hii ya leo.

Ningelipenda kuwasumbua kidogo. Je hii ni sawa au nataka kuingia kwenye mtego?

Kuna binti nimetokea kumpenda sana, ila bahati mbaya ama nzuri tayari ana mtoto Au amezaa na mtu mwingine.

Binafsi nimependezwa naye katika kila angle, na niko radhi kulea mtoto wake na kumpenda maana ukipenda boga huna obligation ya kulipenda pia uwa lake.

Naona kabisa yeye kuwa na mwanae sio tatizo kwangu, ila nimekuwa Niki Sikia kuwa kupenda singo mama ni kujichimbia kaburi mapema, ila mbona anaheshima, ni mstaarabu ana utii na mwerevu?

Je, eti kisa watu wanasema kuwa single mama ni vichomi na mimi niache mtu ni naye mpenda kwa dhati?

Je, niko delusional ama ni ufwate moyo wangu? Na wenye experience Naombeni uzoefu ndugu zangu.

Asanteni.
Tafuta video ya mchekeshaji chery kuhusu kumkuta Single Maza akiwa Ghetto kwake anapelekewa MOTO na mzazi mwenzake.
 
Marrying a single mother is a personal choice,
But remember you are not just marrying a woman,you are stepping into a family that already includes her children and potentially an ex partner/biological father,
Stepping into a family? ( what if she never got married but found herself bearing unnecessary pregnancy?) and. What if she doesn't have any interest to that specific partner?
Man was created to start a family,not to join a family,you don't choose the family you're born into,But you can choose the family you create,

The is just a piece of advice,the rest is up to you.
Is it true, that marrying a single woman is joining a family? Are you trying to say that a woman's value is dependent on a number of people she's had children with, and that she only deserves one husband and that's it?

Anyways, thanks for your contribution. I'll think about it
 
Wanabodi..

Ni heri mmeamka salama kwenda kuyakabiri majukumu ya siku hii ya leo.

Ningelipenda kuwasumbua kidogo. Je hii ni sawa au nataka kuingia kwenye mtego?

Kuna binti nimetokea kumpenda sana, ila bahati mbaya ama nzuri tayari ana mtoto Au amezaa na mtu mwingine.

Binafsi nimependezwa naye katika kila angle, na niko radhi kulea mtoto wake na kumpenda maana ukipenda boga huna obligation ya kulipenda pia uwa lake.

Naona kabisa yeye kuwa na mwanae sio tatizo kwangu, ila nimekuwa Niki Sikia kuwa kupenda singo mama ni kujichimbia kaburi mapema, ila mbona anaheshima, ni mstaarabu ana utii na mwerevu?

Je, eti kisa watu wanasema kuwa single mama ni vichomi na mimi niache mtu ni naye mpenda kwa dhati?

Je, niko delusional ama ni ufwate moyo wangu? Na wenye experience Naombeni uzoefu ndugu zangu.

Asanteni.
Au sio, nenda tu Mkuu ila ipo siku huko mbeleni hata miaka 10 huko utakumbuka majina ya ID zote zilizokushauri katika huu uzi.



Kwa kifupi ukishakuwa nae karibu itafika mahala baba wa mtoto wake huwa anaibuka na kutaka kuwa nae karibu pia, ndugu za baba wa mme wake huibuka na kumsonga au kumjali zaidi kwa kumshirikisha mambo mbalimbali mazuri juu yake na mtoto wake, utasikia tunataka kumkatia mtoto Bima ya Afya, tunataka kumnunulia kiwanja kwa jina lake, tunataka kufanya hiki na kile hapo ndio utaanza kuona anaanza kuwaelewa na kubadilika na ww utaona husikilizwi tayari mgogoro.

Nimewah kuwa na singo maza na mtoto wake bahati nzuri alikuwa kwa mama wa baba walie zaa nae,

Gues what walipohisi ana mtu, huyo mama mkwe akipiga simu ni maongezi ya masaa 2, kule mtoto kila dakika wanajaza vocha kwenye simu na kumlazimisha aongee na mama yake.


Yani akinywa chai simu, akimeza chai simu, akivaa nguo simu, akicheka simu, akitoka na wenzie simu simu simu simu simu simu...


Wakimaliza baba mtu ulieambiwa walikosana nae anaanza nae, akiblokiwa huku anaibukia kule na akiibuka anamwambia nataka tujadili hatma ya mtoto..😀😀😀😀😀😀
 
Wakuu hiyi app mpya inanishindwa namna ya kuandika uZi hebu mnipe maelezo
 
Kwa akili yako research ni mpaka utembelee tovuti?
Huko mtaani ulipo hakuna watu?
Hakuna single mother?
Hakuna waliooa single mother?

Kanye west soma tena ni kitu gani hiki umeandika
So you mean, utajua je kuwa huyu ni single mama kwa kwenda kila Kaya na kuanza kuulizia?

Twende kwa fact, unaposema kufanya research means that lazima uwe na methodology inayo eleweka kuweza kupata matokeo na statistic zinazo eleweka sio kusema unafanya research bila mpangikio
Kanye west soma tena ni kitu gani hiki
Ewe ndugu mdau Kanye west ndo nini? 😂

Haya nieleweshe maana sioni kibaya nilicho andika, badala ya kunipa vibweka naomba nieleweshe namna iliyo bora ya kuweza kuhimili swala hili kubwa lililo mbele yangu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom