Dilemma ya kumpenda mwanamke mwenye mtoto

Dilemma ya kumpenda mwanamke mwenye mtoto

Gunner11

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2021
Posts
14,917
Reaction score
28,648
Wanabodi..

Ni heri mmeamka salama kwenda kuyakabiri majukumu ya siku hii ya leo.

Ningelipenda kuwasumbua kidogo. Je hii ni sawa au nataka kuingia kwenye mtego?

Kuna binti nimetokea kumpenda sana, ila bahati mbaya ama nzuri tayari ana mtoto Au amezaa na mtu mwingine.

Binafsi nimependezwa naye katika kila angle, na niko radhi kulea mtoto wake na kumpenda maana ukipenda boga huna obligation ya kulipenda pia uwa lake.

Naona kabisa yeye kuwa na mwanae sio tatizo kwangu, ila nimekuwa Niki Sikia kuwa kupenda singo mama ni kujichimbia kaburi mapema, ila mbona anaheshima, ni mstaarabu ana utii na mwerevu?

Je, eti kisa watu wanasema kuwa single mama ni vichomi na mimi niache mtu ni naye mpenda kwa dhati?

Je, niko delusional ama ni ufwate moyo wangu? Na wenye experience Naombeni uzoefu ndugu zangu.

Asanteni.
 
Vitu vingine fanya research mwenyewe
Kabla hujapata ushauri kutoka kwa watu wenye trauma na single mother

But kwenye wengi kuna mengi fatilia comment halafu changanya na za kwako kila la kheri

Halafu hapo unaposema upo tayari kumlea mtoto kwani baba ake yupo wapi?
 
Usiyumbishwe na maneno ya mitaani kaka. Umempenda na unaona kabisa anakidhi vigezo vyako unanzaje kuuliza watu kaka?

Kuna ma single mother wengi sana wameachana na wazazi wenzao mazima na wameanzisha familia zenye afya sana na wanaume wengine

Hivi kuna hao wasio na watoto wangapi ambao wameolewa na wamekuwa vichomi balaaa kwenye ndoa zao?
 
Wanabodi..

Ni heri mmeamka salama kwenda kuyakabiri majukumu ya siku hii ya leo.

Ningelipenda kuwasumbua kidogo. Je hii ni sawa au nataka kuingia kwenye mtego?

Kuna binti nimetokea kumpenda sana, ila bahati mbaya ama nzuri tayari ana mtoto Au amezaa na mtu mwingine.

Binafsi nimependezwa naye katika kila angle, na niko radhi kulea mtoto wake na kumpenda maana ukipenda boga huna obligation ya kulipenda pia uwa lake.

Naona kabisa yeye kuwa na mwanae sio tatizo kwangu, ila nimekuwa Niki Sikia kuwa kupenda singo mama ni kujichimbia kaburi mapema, ila mbona anaheshima, ni mstaarabu ana utii na mwerevu?

Je, eti kisa watu wanasema kuwa single mama ni vichomi na mimi niache mtu ni naye mpenda kwa dhati?

Je, niko delusional ama ni ufwate moyo wangu? Na wenye experience Naombeni uzoefu ndugu zangu.

Asanteni.
Hakuna jambo gumu kama kumshauri mtu aliyeko kwenye mapenzi au anayekaribia kutapeliwa
 
Marrying a single mother is a personal choice,
But remember you are not just marrying a woman,you are stepping into a family that already includes her children and potentially an ex partner/biological father,

Man was created to start a family,not to join a family,you don't choose the family you're born into,But you can choose the family you create,

This is just a piece of advice,the rest is up to you.
 
Vitu vingine fanya research mwenyewe
Kabla hujapata ushauri kutoka kwa watu wenye trauma na single mother

But kwenye wengi kuna mengi fatilia comment halafu changanya na za kwako kila la kheri

Halafu hapo unaposema upo tayari kumlea mtoto kwani baba ake yupo wapi?
Research?
Kuna any paper au tovuti inaelezea kuhusu madhara ya kuoa au kuwa kwenye mahusiano na single mama?

Au research hiyo itanipasa nitembelee sehemu gani ili niweze kupata data rasmi na majibu yaliyo fasaha?

Sijajua atakuwa wapi, ila I know mtoto atahitaji huduma pia, na nikisema hilo sio jukumu langu Nitakuwa na jizima data tu, labda kama Nita hakikisha huyo mzazi mwenza yupo na ana kipato kizuri hapo itanilazimu kumwita na kufanya mazungumzo naye juu ya mtoto wake asiye na hatia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom