Dilemma ya kumpenda mwanamke mwenye mtoto

Dilemma ya kumpenda mwanamke mwenye mtoto

Wanabodi..

Ni heri mmeamka salama kwenda kuyakabiri majukumu ya siku hii ya leo.

Ningelipenda kuwasumbua kidogo. Je hii ni sawa au nataka kuingia kwenye mtego?

Kuna binti nimetokea kumpenda sana, ila bahati mbaya ama nzuri tayari ana mtoto Au amezaa na mtu mwingine.

Binafsi nimependezwa naye katika kila angle, na niko radhi kulea mtoto wake na kumpenda maana ukipenda boga huna obligation ya kulipenda pia uwa lake.

Naona kabisa yeye kuwa na mwanae sio tatizo kwangu, ila nimekuwa Niki Sikia kuwa kupenda singo mama ni kujichimbia kaburi mapema, ila mbona anaheshima, ni mstaarabu ana utii na mwerevu?

Je, eti kisa watu wanasema kuwa single mama ni vichomi na mimi niache mtu ni naye mpenda kwa dhati?

Je, niko delusional ama ni ufwate moyo wangu? Na wenye experience Naombeni uzoefu ndugu zangu.

Asanteni.
Wenye uzoefu tunayaelewa mambo yenyekufanana yanayoumiza wanaume kuoa 'SM' ambayo baadaye huenda yakakuletea kero maishani mtapozoeana.
1-Mawasiliano na mzazi mwenza.
2-Kama ikitokea uzazi utasumbua.

Hayo ni mambo pasua kichwa unatakiwa ukae chini uyatafakari.
 
Wanabodi..

Ni heri mmeamka salama kwenda kuyakabiri majukumu ya siku hii ya leo.

Ningelipenda kuwasumbua kidogo. Je hii ni sawa au nataka kuingia kwenye mtego?

Kuna binti nimetokea kumpenda sana, ila bahati mbaya ama nzuri tayari ana mtoto Au amezaa na mtu mwingine.

Binafsi nimependezwa naye katika kila angle, na niko radhi kulea mtoto wake na kumpenda maana ukipenda boga huna obligation ya kulipenda pia uwa lake.

Naona kabisa yeye kuwa na mwanae sio tatizo kwangu, ila nimekuwa Niki Sikia kuwa kupenda singo mama ni kujichimbia kaburi mapema, ila mbona anaheshima, ni mstaarabu ana utii na mwerevu?

Je, eti kisa watu wanasema kuwa single mama ni vichomi na mimi niache mtu ni naye mpenda kwa dhati?

Je, niko delusional ama ni ufwate moyo wangu? Na wenye experience Naombeni uzoefu ndugu zangu.

Asanteni.
Sijausoma Uzi wote ila nnachokwambia Kwa wivu mkubwa sana KIMBIA KWA NGUVU ZAKO ZOTE.
 
Yaani umekiri kabisa umekuwa ukisikia watu wengi wakiwasema vibaya single mothers lakini bado huoni lisemwalo lipo?

Shuhuda nyingi zimetolewa humu namna single mothers wanavyowapiga matukio waume zao wa ndoa na kwenda kuziniwa na waume zao wawapendao kwa dhati waliowazalisha.
Au mimi ndiyo sikio la kufa ambalo halisikii dawa?
 
King of reactions tayari maamuzi anayo mkononi. Ni ngumu sana kumkataza mtoto aende disko mpaka pale atakapoona madhara yake.

Hakuna mtu anaweza kubadili maamuzi yake. Apo anataka tu kuona watu wanavyoyachukulia maamuzi yake.
Hapana mkuu, inachukua point na kujifunza namna ya kukabili jambo hili Zito lililopo mbele yangu
 
Mtoa mada hapa jf linapokuja swala la single maza watu huwa hawawi kati kwa kati,asilimia kubwa husema negative kuhusu single maza

Kiukweli ni kwamba tukiacha matukio ambayo watu wamepigwa na single mazas, bado kuna single mazas ambao wamemove on,wameamua kuishi maisha mapya kabisa,wameachana na vichomi wao wa zamani na kuamua kuanza maisha upya

Hawa hutasikia drama kutoka kwao,hawa wanaheshimu mahusiano,na wanataka kurekebisha palipo haribika

Sasa kosa la watu wa jf na waathirika wa hao single mazas,siku zote hawataona pande mbili za shilingi,hawa hawatakuja kuona ukweli kwamba kuna single mazas ambao wapo gud na wanaweza kuwa wife Materials

Sasa ila sipingi ukweli kwamba asilimia kubwa karibia asilimia 90,mara nyingi single mazas ni mtihani sana,wengi huja kuzingua baadae kwa kulala na baba watoto wao

Kwahiyo je utatuaje huyu single maza ni tofauti na wengine,ni kupitia mazungumzo,muulize maswali magumu juu ya mzazI mwenzio,namna watakavyo wasiliana juu ya malezi ya mtoto wao,na kwa namna gani hatokuleta sintofahamu ambayo inaweza pelekea kukupa wewe mashaka.

Narudia tena pamoja story nyingi mbaya kuhusu single mazas lakini bado kuna wazuri miongoni mwao.
Asante sana ndugu mdau,

Na hii ndio hope ambayo ninayo baada ya kupata kujiridhisha tabia yake, nahisi atakuwa ni mwanamke swafi kabisa na hata leta zongo yoyote maana hata yeye anasema wanaume wazuri nao wamebaki wachache sana.

Watu wengi sana wame leta negative response ila haiondoi kuwa kuwa singo Maza ni kosa na itamfanya mtu awe traumatized hadi asitulie kabisa kwenye mahusiano.

Asante na Nita hakikisha tunakaza chini na kuhojiana maswali magumu ili asije kutokea haya yanayozungumzwa
 
mkuu na uyakumbuke maneno yangu mausiano ya kimapenzi na sigle mother ni kwa ajiri ya kujiburudisha tu na si vinginevyo kama endapo utakaidi maneno yangu basi kuna siku nyingine utakuja kushusha nyuzi nyingine ya maumivu makali mno na mimi nitakuombea dua tu
Duuh hadi wewe sheikh kweli? 😂

Aisee, mbona kazini kuna kazi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom