Huna sababu ya kuwa baba wa kambo hasa ukiwa chini ya miaka 45

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
39,988
Reaction score
92,674
HUNA SABABU YA KUWA BABA YA KAMBO HASA UKIWA CHINI YA MIAKA 45.

Anaandika, Robert Heriel Tz
Mtibeli.

Naongea na vijana wa Tibeli, naongea na binti za Tibeli. Nazungumza na wanaume wa Tibeli. Nazungumza na wanawake watibeli. Na wote wenye ufahamu.

Najua duniani inatabaka mbili. Watumwa na watawala.
Wanyonyaji na wanywonyaji.
Wanaume misukule na Wanaume wafalme.
Nafahamu wanaume misukule wapo kwaajili ya kutumikishwa na kutumikia. Hivyo sitaki hilo libadilike. Nataka liwe hivyohivyo.

Nimeandika kwa Watibeli ili muwaambie vijana wenu, na vijana wajue kuwa sisi Watibeli ni watu huru. Kwa sababu Akili ndio silaha yetu, na haki ndio mustakabali wetu. Na upendo ndio hutupa furaha na amani ya kweli. Na Ukweli ndio hutupa njia.

Kijana kama upo below yaani upo chini ya miaka 45 huna sababu ya kuwa Baba wa kambo. Usifikirie kwa urefu wa pua yako. Fikiria miaka 20 na 30 ijayo. Nini kitatokea.
Niliwahi kukuandika tawala Tatu ndani ya familia. Karudie ile post. Utanielewa.
Sio kila siku utakuwa na nguvu kijana.
Nguvu zako zitaisha siku moja.

Wahenga walisema, mwanaume aliumbwa kuanzisha familia yake. Na sio ku-join kwenye familia ya mtu mwingine.

Pili Dunia ilianza kwa mtu mke na mume. Na sio vinginevyo.

Nilisema kama utataka kuoa Mwanamke mwenye mtoto basi itakupasa awe mke wa pili yaani tayari ulishakuwa na mkeo, ulishakuwa na familia yako.

Sisemi kuwakandia wanawake kwa sababu mimi ni Baba, mume na Kaka na kesho kutwa nitakuwa Babu. Nina Mama zangu na wanasoma hapa, Nina Dada wanasoma hapa, Nina Binti zangu wa kuwazaa wanasoma hapa, Nina wakwe zangu, mashemeji na rafiki zangu wakike, wote wanasoma hapa.

Sisemi haya kwa sababu ninawachukia bali nasema haya kuokoa jamii na tawala za wanaume.

Ni muhimu kama mwanamke yeyote ataumia basi atumie post hii kujionya na kuonya mabinti wasizae kabla ya ndoa. Pia kulinda ndoa za watoto wao. Kushauri vijana wao wakioa wasiache wake zao. Kumaanisha wachague mwanamke sahihi.
Lakini kama kuna mwanamke yeyote, nasema yeyote bila kujali nafasi yake. Ataumia na kuchukia na hataki kubadilika na kuwa mwema au kufanya watoto wake wawe wema wasiwe kama yeye muovu huyo wala sisi Watibeli hatuhangaishi kwa sababu hata porini wapo wanyama kama Fisi, na wapo wadudu kama Nzi na mende.

Kwa kifupi kwa nini huna sababu ya kuwa Baba wa kambo ukiwa na umri chini ya miaka 45

a) Umri wako bado ni wa kujijenga.
Ukiwa chini ya 40, unaweza kuwa bado unaweka msingi wa kazi, biashara, fedha na maisha yako. Kuingia kwenye jukumu la Baba wa kambo kunaweza kuongeza majukumu kabla hujawa tayari. Mtu hata kipato chako hakifiki milioni 2 unajiangika msalabani. Ndio ile tunasema duniani Wapo walioumbwa kuwa misukule.

b) Mtoto anaweza asiwe tayari kukukubali.
Usifikiri kwa sababu unampenda mama yake basi mtoto atakupokea moja kwa moja kama baba. Anaweza kukataa, kukupinga au kukulinganisha na baba yake mzazi.
Hili wengi hunipigia simu na wakilalamikia.
Juzi hapa kuna Mdau alinipigia simu kapigwa na Mtoto aliyemlea mwenyewe. Tena dogo mwenyewe yupo kidato cha sita, na anatakiwa kuingia chuo mwezi November. Jamaa ananiambia hatamlipia Ada.

c) Baba wa kambo si suala la kumpenda mama tu.
Unapomuoa mwanamke mwenye mtoto, kwa namna fulani unaingia pia kwenye maisha ya mtoto. Mtoto anahitaji muda, malezi, uvumilivu na uwepo wako. Hilo ni jukumu kubwa kuliko ndoa yenyewe.
Na yote utakayoyafanya haimaanishi yatabadili ukweli kwamba huyo sio mtoto wako. Na anahaki ya kumjua babaake mzazi na kumpenda pia.

d) Baba mzazi wa mtoto anaweza kuwa sehemu ya maisha yenu.
Hili ndilo ningesisitiza sana. Kama baba wa mtoto bado yupo, unaweza kujikuta kuna maamuzi, migogoro au mipaka ambayo itahitaji hekima kubwa. Je, uko tayari kuishi na hali hiyo bila kuumia kihisia?
Huwa nashangaa wanaume wanaokataza Wake zao kuongea na Wazazi wenza wao. Hilo haliwezekani. Hao wana mtoto pamoja. Wanahitajiana kwa ustawi wa mtoto wao. Acha mihemko ya kitoto.

e) Usifikiri utamwokoa mwanamke kwa kumuoa.
Kama kuna matatizo katika maisha yake, ndoa si lazima iwe suluhisho. Kwanza jiulize kama mnalingana kweli.
Vijana wengi huoa single mother kwa kumhurumia. Ni ujinga mkubwa.
Ndio maana wakigombana kidogo huanza manyanyaso, oooh! Nilikukuta umezalishwa, nilikukuta huna mbele wala nyuma, oooh! Nilikukuta hata kumtunza mtoto wako huwezi. Wanaume walikukimbia mimi nikakuoa.
Hivi zinakutosha kweli?
Kwa hiyo ulifikiri ndoa ni mbinu ya kumuokoa mwanamke?

f) Unahitaji uhakika kwamba unataka kulea mtoto ambaye si wako wa damu.
Kuna siku mtoto atakuita baba, lakini kuna siku anaweza kukuambia, “Wewe si baba yangu.” Kama hujajiandaa kihisia kwa hilo, unaweza kuumia sana na hata ndoa ikayumba.
Nimesikia mara kibao watoto wengi wakiambia baba zao wakambo wewe sio Baba yangu mzazi. Kwa masikio yangu.
Hasa pale Baba unapojaribu kumuamulia mtoto jambo ambalo yeye halitaki.

g) Ni kawaida Mtoto akikua yeye na Mama yake kukugeuka.
Bora ugeukwe na mtoto wako wa kumzaa. Mtoto ni mtoto. Zimwi likujualo halikuli likakwisha. Mtagombana leo kesho mtawasiliana.
Lakini mtoto kama sio wako ni sio wako. Na dunia itakuthibitishia hilo.

h) Siku ukiachana na huyo Mwanamke unapoteza mke na mtoto.
Fikiria mtoto umemkuza tangu akiwa na mdogo. Umetoa jasho lako, mawazo, nguvu, malezi. Mtoto amefikisha miaka 20 ikatokea lakutokea mkapeana talaka na huyo mwanamke.
My friend umepoteza kila kitu. Umepoteza mwanamke, mtoto, pesa, muda, nguvu na akili zako zote.
Usije fikiria kwamba oooh mtoto atakumbuka fadhila sijui hisani. Weewe! Tumia akili.

Dunia hainaga fadhila wala hisani. Watoto wako wenyewe wa kuwazaa wanafanya hivyo kwa sababu wewe ni Baba yao, wanaohuo wajibu kiasili. Lakini mtoto asiyewako hana huo wajibu.

Utaumia sana. Utakuwa fundisho kwa wengine.

Vijana, haya maisha hayahitaji makisio. Narudia ni bora uteswe na mtoto uliyemzaa wala hautaumia sana kama kuteswa na mtu uliyefanya jambo ambalo hukustahili kumfanyia. Ulimpa msaada tuu.
Ndipo ile kauli ya penye chuki Wema ukitangulia.

Kumtendea mtoto wako Wema ni wajibu wako. Hivyo hata asiporudisha sio lazima kwani atarudisha tuu kwa kukuongezea ukoo huko na kuongeza kizazi chako. Lakini baba wa kambo ukipoteza umepoteza tangu siku ya kwanza.

Ukishakuwa na mke wako mwenyewe. Ambaye mlianzisha familia yenu wenyewe. Ukazaa watoto wenu wenyewe. Mkajenga familia yenu wenyewe. Kama itakuona yakupasa kuongeza mke au suria(mchepuko) kama kuna huo ulazima basi ndio unaweza kufikiria kuwa Baba wa kambo.

Mimi nimemaliza. Jicho lako lisiwe na huruma hata kidogo kwa sababu Dunia haitakupa nafasi ya kuhurumiwa. Shauri yako.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Usiwa pangie watu maisha.
Waache watu wapendane hayo mengine watajua namna ya kuyashugulika

Maana katika upendo hakuna kinachoshindikana. Love can move mountains.

Kuna wanawake wamezalishwa lakini ni bora zaidi ya vicheche wanaishia kudanga ndani ya ndoa.

Infact angalia mtu, na matendo, angalia kama ana align na goals zako. Je unaona future naye? Je, anakidhi vigezo vya kuwa mshirika bora wa kile unacho dhani unahitaji katika kufikia malengo ya maisha yako?
 
Usiwa pangie watu maisha.
Waache watu wapendane hayo mengine watajua namna ya kuyadhugulika

Maana katika upendo hakuna kinachoshindikana. Love can move mountains.

Kuna wanawake wamezalishwa lakini ni bora zaidi ya vicheche wanaishia kudanga ndani ya ndoa.

Infact angalia mtu, na matendo, angalia kama ana align na goals zako. Je unaona future naye? Je, anakidhi vigezo vya kuwa mshirika bora wa kile unacho dhani unahitaji katika kufikia malengo ya maisha yako?

Mambo ya Watibeli yanapangiaje watu wengine maisha?

Au mambo yenu watu wengine yanapangiaje sisi Maisha yetu?
 
Acha kujidanganya kuwa mtu yuko accustomed kwa culture fulani. Kila mtu ana uhuru wa kuchagua. Kutokana na kile anaona inafaa kwake despite ni Mtibeli ama msukuma

Wewe ni kitu gani ulichochagua ambacho kipo nje ya utamaduni? Nitajia kimoja tuu.

Kingine, Sisi Watibeli hatuingilii maisha yenu. Tukitoa hotuba zetu ni kwaajili yetu tuu. Ni kiherehere cha watu wengine kushindwa kujua na kufuata yanayowahusu au yaliyo ndani ya mipaka yao
 
HUNA SABABU YA KUWA BABA YA KAMBO HASA UKIWA CHINI YA MIAKA 45.

Anaandika, Robert Heriel Tz
Mtibeli.

Naongea na vijana wa Tibeli, naongea na binti za Tibeli. Nazungumza na wanaume wa Tibeli. Nazungumza na wanawake watibeli. Na wote wenye ufahamu.

Najua duniani inatabaka mbili. Watumwa na watawala.
Wanyonyaji na wanywonyaji.
Wanaume misukule na Wanaume wafalme.
Nafahamu wanaume misukule wapo kwaajili ya kutumikishwa na kutumikia. Hivyo sitaki hilo libadilike. Nataka liwe hivyohivyo.

Nimeandika kwa Watibeli ili muwaambie vijana wenu, na vijana wajue kuwa sisi Watibeli ni watu huru. Kwa sababu Akili ndio silaha yetu, na haki ndio mustakabali wetu. Na upendo ndio hutupa furaha na amani ya kweli. Na Ukweli ndio hutupa njia.

Kijana kama upo below yaani upo chini ya miaka 45 huna sababu ya kuwa Baba wa kambo. Usifikirie kwa urefu wa pua yako. Fikiria miaka 20 na 30 ijayo. Nini kitatokea.
Niliwahi kukuandika tawala Tatu ndani ya familia. Karudie ile post. Utanielewa.
Sio kila siku utakuwa na nguvu kijana.
Nguvu zako zitaisha siku moja.

Wahenga walisema, mwanaume aliumbwa kuanzisha familia yake. Na sio ku-join kwenye familia ya mtu mwingine.

Pili Dunia ilianza kwa mtu mke na mume. Na sio vinginevyo.

Nilisema kama utataka kuoa Mwanamke mwenye mtoto basi itakupasa awe mke wa pili yaani tayari ulishakuwa na mkeo, ulishakuwa na familia yako.

Sisemi kuwakandia wanawake kwa sababu mimi ni Baba, mume na Kaka na kesho kutwa nitakuwa Babu. Nina Mama zangu na wanasoma hapa, Nina Dada wanasoma hapa, Nina Binti zangu wa kuwazaa wanasoma hapa, Nina wakwe zangu, mashemeji na rafiki zangu wakike, wote wanasoma hapa.

Sisemi haya kwa sababu ninawachukia bali nasema haya kuokoa jamii na tawala za wanaume.

Ni muhimu kama mwanamke yeyote ataumia basi atumie post hii kujionya na kuonya mabinti wasizae kabla ya ndoa. Pia kulinda ndoa za watoto wao. Kushauri vijana wao wakioa wasiache wake zao. Kumaanisha wachague mwanamke sahihi.
Lakini kama kuna mwanamke yeyote, nasema yeyote bila kujali nafasi yake. Ataumia na kuchukia na hataki kubadilika na kuwa mwema au kufanya watoto wake wawe wema wasiwe kama yeye muovu huyo wala sisi Watibeli hatuhangaishi kwa sababu hata porini wapo wanyama kama Fisi, na wapo wadudu kama Nzi na mende.

Kwa kifupi kwa nini huna sababu ya kuwa Baba wa kambo ukiwa na umri chini ya miaka 45

a) Umri wako bado ni wa kujijenga.
Ukiwa chini ya 40, unaweza kuwa bado unaweka msingi wa kazi, biashara, fedha na maisha yako. Kuingia kwenye jukumu la Baba wa kambo kunaweza kuongeza majukumu kabla hujawa tayari. Mtu hata kipato chako hakifiki milioni 2 unajiangika msalabani. Ndio ile tunasema duniani Wapo walioumbwa kuwa misukule.

b) Mtoto anaweza asiwe tayari kukukubali.
Usifikiri kwa sababu unampenda mama yake basi mtoto atakupokea moja kwa moja kama baba. Anaweza kukataa, kukupinga au kukulinganisha na baba yake mzazi.
Hili wengi hunipigia simu na wakilalamikia.
Juzi hapa kuna Mdau alinipigia simu kapigwa na Mtoto aliyemlea mwenyewe. Tena dogo mwenyewe yupo kidato cha sita, na anatakiwa kuingia chuo mwezi November. Jamaa ananiambia hatamlipia Ada.

c) Baba wa kambo si suala la kumpenda mama tu.
Unapomuoa mwanamke mwenye mtoto, kwa namna fulani unaingia pia kwenye maisha ya mtoto. Mtoto anahitaji muda, malezi, uvumilivu na uwepo wako. Hilo ni jukumu kubwa kuliko ndoa yenyewe.
Na yote utakayoyafanya haimaanishi yatabadili ukweli kwamba huyo sio mtoto wako. Na anahaki ya kumjua babaake mzazi na kumpenda pia.

d) Baba mzazi wa mtoto anaweza kuwa sehemu ya maisha yenu.
Hili ndilo ningesisitiza sana. Kama baba wa mtoto bado yupo, unaweza kujikuta kuna maamuzi, migogoro au mipaka ambayo itahitaji hekima kubwa. Je, uko tayari kuishi na hali hiyo bila kuumia kihisia?
Huwa nashangaa wanaume wanaokataza Wake zao kuongea na Wazazi wenza wao. Hilo haliwezekani. Hao wana mtoto pamoja. Wanahitajiana kwa ustawi wa mtoto wao. Acha mihemko ya kitoto.

e) Usifikiri utamwokoa mwanamke kwa kumuoa.
Kama kuna matatizo katika maisha yake, ndoa si lazima iwe suluhisho. Kwanza jiulize kama mnalingana kweli.
Vijana wengi huoa single mother kwa kumhurumia. Ni ujinga mkubwa.
Ndio maana wakigombana kidogo huanza manyanyaso, oooh! Nilikukuta umezalishwa, nilikukuta huna mbele wala nyuma, oooh! Nilikukuta hata kumtunza mtoto wako huwezi. Wanaume walikukimbia mimi nikakuoa.
Hivi zinakutosha kweli?
Kwa hiyo ulifikiri ndoa ni mbinu ya kumuokoa mwanamke?

f) Unahitaji uhakika kwamba unataka kulea mtoto ambaye si wako wa damu.
Kuna siku mtoto atakuita baba, lakini kuna siku anaweza kukuambia, “Wewe si baba yangu.” Kama hujajiandaa kihisia kwa hilo, unaweza kuumia sana na hata ndoa ikayumba.
Nimesikia mara kibao watoto wengi wakiambia baba zao wakambo wewe sio Baba yangu mzazi. Kwa masikio yangu.
Hasa pale Baba unapojaribu kumuamulia mtoto jambo ambalo yeye halitaki.

g) Ni kawaida Mtoto akikua yeye na Mama yake kukugeuka.
Bora ugeukwe na mtoto wako wa kumzaa. Mtoto ni mtoto. Zimwi likujualo halikuli likakwisha. Mtagombana leo kesho mtawasiliana.
Lakini mtoto kama sio wako ni sio wako. Na dunia itakuthibitishia hilo.

h) Siku ukiachana na huyo Mwanamke unapoteza mke na mtoto.
Fikiria mtoto umemkuza tangu akiwa na mdogo. Umetoa jasho lako, mawazo, nguvu, malezi. Mtoto amefikisha miaka 20 ikatokea lakutokea mkapeana talaka na huyo mwanamke.
My friend umepoteza kila kitu. Umepoteza mwanamke, mtoto, pesa, muda, nguvu na akili zako zote.
Usije fikiria kwamba oooh mtoto atakumbuka fadhila sijui hisani. Weewe! Tumia akili.

Dunia hainaga fadhila wala hisani. Watoto wako wenyewe wa kuwazaa wanafanya hivyo kwa sababu wewe ni Baba yao, wanaohuo wajibu kiasili. Lakini mtoto asiyewako hana huo wajibu.

Utaumia sana. Utakuwa fundisho kwa wengine.

Vijana, haya maisha hayahitaji makisio. Narudia ni bora uteswe na mtoto uliyemzaa wala hautaumia sana kama kuteswa na mtu uliyefanya jambo ambalo hukustahili kumfanyia. Ulimpa msaada tuu.
Ndipo ile kauli ya penye chuki Wema ukitangulia.

Kumtendea mtoto wako Wema ni wajibu wako. Hivyo hata asiporudisha sio lazima kwani atarudisha tuu kwa kukuongezea ukoo huko na kuongeza kizazi chako. Lakini baba wa kambo ukipoteza umepoteza tangu siku ya kwanza.

Ukishakuwa na mke wako mwenyewe. Ambaye mlianzisha familia yenu wenyewe. Ukazaa watoto wenu wenyewe. Mkajenga familia yenu wenyewe. Kama itakuona yakupasa kuongeza mke au suria(mchepuko) kama kuna huo ulazima basi ndio unaweza kufikiria kuwa Baba wa kambo.

Mimi nimemaliza. Jicho lako lisiwe na huruma hata kidogo kwa sababu Dunia haitakupa nafasi ya kuhurumiwa. Shauri yako.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
"Wakishua; maisha umeyapatia na hasa ukizingatia uandishi nayo kazi, basi Mungu akupe nini tena!.
 
Wewe ni kitu gani ulichochagua ambacho kipo nje ya utamaduni? Nitajia kimoja tuu.

Kingine, Sisi Watibeli hatuingilii maisha yenu. Tukitoa hotuba zetu ni kwaajili yetu tuu. Ni kiherehere cha watu wengine kushindwa kujua na kufuata yanayowahusu au yaliyo ndani ya mipaka yao
Acha kujidanganya wewe..

Binafsi nimechagua kuwa optimistic thinker.. Na sio mfungwa wa mila.. Hicho ni kimoja..

Watibeli? Kwa dunia gani mnayoishi? Usije kudhani utafanya mtu aishi kwa Matakwa yako wewe, fanya kuinspire lakini Utapigwa na inabidi uone kawaida tu. Hata Watibeli wenye akili huru hawawezi kuishi kwa mawazo ya mtu mmoja
 
We jamaa single mothers wamekukosea nini? Mtu kama wewe ungekuwa na uwezo ungeangamiza single mothers wote. Punguza chuki bro. Kuwa na mtoto sio uhalifu. Pia acha kupangia watu jinsi ya kuishi ili mradi hawavunji sheria. Unaandika uzi mrefu uliojaa chuki dhidi ya binadamu wenzako. Sio sahihi mkuu. JIREKEBISHE.
 
Back
Top Bottom