Diamond: Manara ana mchango mkubwa kwenye mpira, tukiendekeza chuki za mtu mmoja mmoja ni kudidimiza mpira. Aiomba Serikali imfungulie

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,831
Msanii wa mziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz akiwa kwenye birthday party ya Manara jana usiku, alitumia sehemu kubwa ya salam zake kuongelea sakata la Manara kufungiwa na TFF kujishirikisha na mpira wa miguu Tanzania. Diamond amesema ni chuki na kuiomba Serikali ifanye jambo.

Diamond amesema ameshawahi kuongea na Manara na Haji aliomuomba Diamond kutokana na hadhi yake kwenye jamii amsaidie kuwauliza wahusika shida nini!

Diamond amedai alikuwa hajui chochote kwenye mpira ila ameufatilia kwasababu ya Manara.

Diamond: Lazima tukubali, huyu bwana kwenye mpira wa Tanzania ana nafasi kubwa, ana mchango mkubwa. Tukiendekeza chuki za mtu mmoja mmoja ikiwepo Serikali inatazama inadidimiza mpira wenyewe.

Unaangalia, yani huyu ana ubaya gani kwenye hii nchi, yaani ana baya gani haswa alilolifanya katika nchi hii, ni binadamu mbaya kiasi gani! Karia wakati mwingine chuki tu.

Alisema Diamond

Huo sasa ni upuuzi kabisa yaani Diamond anaituhumu mamlaka iliyomfungia Haji kuwa ilimuonea tu halafu anaiomba imfungulie hivi hizi akili za wapi hizi?
 
Back
Top Bottom