Ni vigumu kwa Mwafrika Dr Tedros Ghebreyesus kuendelea kuongoza WHO, Marekani yaondoa fedha za mchango nyuma ya pazia, yashinikiza Tedros aondolewe

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,464
2,000
Dr Tedros alianza kuonekana kwenye televisheni duniani akitoa maelezo mbalimbali kuhusiana na ugonjwa wa COVID-19.

Pia aliweza kuonekana akijibu masuali mbalimbali ya waandishi wa habari juu ya maendeleo ya ugonjwa huo na taarifa zingine nyingi tu kupitia mitandao kama ya twitter na kadhalika.

Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus ambae ni raia wa Ethiopia, alichaguliwa kuongoza WHO miaka mitatu ilopita kwa kipindi cha miaka mitano katika mkutano mkuu wa shirika hilo ambalo lipo chini ya Umoja wa Mataifa.

Ni Mkurugenzi wa kwanza ambae alichaguliwa kutoka kwenye kundi la wagombea zaidi ya mmoja na ni Mkurugenzi wa kwanza kuongoza shirika hiko kutoka bara la Afrika.

Dr Tedros kitaalam ni mtafiti wa ugonjwa wa Malaria na alipokuwa nchini kwake aliwahi kushika nafasi za uwaziri wa afya na uwaziri wa mambo ya nje toka mwaka 2012 hari 2016.

Dr Tedros ana shahada ya kwanza ya sayansi ya bilojia alohitimu kutoka chou kikuu ya Asmara (sasa mji mkuu wa Eritrea) mwaka 1986.

Pia baadae mwaka 1993 Dr Tedros alihitimu shahada ya uzamili inayohusu magonjwa ya kuambukiza kutoka chou kikuu cha London kitivo cha tiba za magonjwa ya kitropiki na baadae mwaka 2000 akafuzu shahada ya uzamivu kuhusu afya ya jamii kutoka chou kikuu cha Nottingham nchini Uingereza.

Katika kazi ambazo Dr Tedros amenekana amezifanya kwa ufanisi ni pamoja na kupunguza kwa kiasi kikubwa kasi ya kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi katika mkoa wa Tigray ambao alipangiwa kazi, na ugojwa wa uti wa mgongo kwa asilimia 69.

Pia chini ya uangalizi wake Dr Tedros alihakikisha kila hospitali, kituo cha afya na cliniki mkoani humo vinaunganishwa na mtandao wa kompyuta na kunakuweko na mtandao wa internet ambao haukatiki mambo ambayo hayakuwahi kuwepo mkoani humo.

Jambo jingine kubwa ambalo mtaalam huyu alilifanya kwa nchi yake ni kuhakikisha kila kilomita 10 kunakuwa na kituo kinachotoa huduma za afya na kuwezesha asilimia 60 ya wananchi wanapata huduma hizo.

Pamoja na sifa hizo pia Dr Tedros amesimamia kampeni dhidi ya magonjwa kama wa kifua kikuu, uzazi wa mpangp na kusaidia kuzuia mimba za utotoni na kuboresha afya za akina mama na watoto.

Dr Tedros anaelezwa na vyanzo mbalimbali kwamba ana sifa au skills za uhamasishaji na ni mhamasishaji na mjenga mzuri na ana uwezo wa kuleta hoja na kuhamasisha jambo na likakubalika.

Bila shaka kutokana na rekodi hii shirika la afya duniani lenea makao yake makuu mjini Geneva nchini Switzerland likamchagua Dr Tedros kutoka kwenye kundi la watahiwa wengine wenye sifa mbalimbali.

Leo hii Rais Donald Trump anatangaza kusitisha mchango wa Marekani kwa WHO akitoa sababu kwamba shirika hilo la afya duniani limeshindwa kusimamia kimadhubuti ugonjwa wa COVID-19 na pia limeshindwa kuibana China ambayo imekuwa haitoi ushirikiano khasa wa kupeana taarifa kuhusu taarifa za ugonjwa huo.

Pia katika madai hayo Rais Trump akasema WHO haikupaswa kuipongeza China kwa kuwa wazi kwenye kutoa taarifa za ugonjwa wa COVID-19.

Pia baadae Jumatano Rais Trump kuona hio haitoshi akaamua kusema kabisa dukuduku lake kwamba China imekuwa inadanganya katika taarifa zake za ugonjwa wa COVID 19.

Marekani ni mchangiaji mkubwa kwenye shirika hilo kiasi cha dola milioni 400 kwa mwaka na China imejibu kwa kuiomba Marekani ifikirie uamuzi wake huo.

Pia Mkurugenzi mkuu wa WHO Dr Tedros naye amesema WHO inasikitishwa na uamuzi huo wa serikali ya Marekani chini lakini inaamini kwamba uamuzi huo utafikirwa upya na Rais Donald Trump.

Mpaka sasa nchi nyingi hazijatoa tamko lolote lile kuhusiana na uamuzi huo wa Marekani wala kujibu kauli zinazotoka Washington lakini baadhi wameanza kuonekana wanaunga mkono kaui za Rais Trump.

Nchini Uingereza mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi wa nje la MI6 bwana John Sawer amesema kwamba China ilificha kwa dunia taarifa za mlipuko wa ugonjwa wa COVID -19.

Jasusi Sawer amesema ujasusi ni kupata taarifa ambazo zimefichwa usizipate kutoka kwenye nchi na wahusika wengine. Lakini kulikuwa na ufichwaji wa taarifa za awali zilizokuwa zikitolewa tangu mlipuko uanze mwezi Disemba na januari kwa nchi za magharibi na Marekani.

Madai hayo ya jasusi huyo mbobezi yanalingana na madai ya majasusi wa Marekani na vyanzo vingine mbalimbali ambao walimpatia raisi Trump taarifa kwamba pamoja na kirusi COVID -19 kutokea kiasili lakini kuna kila dalili kwamba kirusi huyo alitengenezwa kwenye maabara ya Virolijia mjini Wuhan.

Taarifa hizo zimeeendelea kudai kuwa kulikuwa na mwanafunzi wa kike katika maabara hiyo ambae hakufuata protokali za matumizi ya maabara hiyo na kwenda nyumbani akiwa ameambukizwa kirusi hicho kisha kwenda kumuambukiza rafiki wake wa kiume ambae nae kesho yake alikwenda kwenye soko la wanyama ambalo halikuwa katika mazingira mazuri ya usafi.

Rais Donald Trump akihojiwa na mwandishi wa Fox News bwana John Robert ambae aluliza kwamba, ‘Multiple sources are telling Fox the US government now has high confidence that while the coronavirus is a naturally occurring virus, it emanated from a virology lab in Wuhan.

Rais Trump akajibu kwa kusema ,‘I don’t want to say that John, but I will tell you, more and more were hearing the story and we’ll see.’

Rais Trump pia alionyesha kukubaliana na vyanzo vya bwana Robert kwa kusema,, ‘and when you’re saying multiple sources there's a case when you can use the word sources. But we are doing a very thorough examination of this horrible situation.’

Ikumbukwe pia katika kipindi hicho daktari mmoja nchini China Dr Li Wenliang alikufa baada ya kuambukizwa ugnjwa huo na kabla ya kifo chake aliwaonya marafiki zake juu ya ubaya wa ugonjwa huo na baadae kuitwa kwenye kamati ya maadili ya chama cha kikomunisti.

Sasa mpira umeelekezwa kwa Dr Tedros kwamba ameisaidia China kudharau taarifa za awali za mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 na hiyo ikiwa ni baada ya wataalam na wachunguzi mbalimbali kuanza kutaka mtaalam huyo ajiuzulu nafasi yake hiyo ya ukurugenzi mkuu.

Dr Tedros amejikuta katika mgogoro wa mataifa haya makubwa Marekani na China, mgogoro ambao ni wa muda mrefu na kitovu chake kikiwa ni mkataba wa kibiashara.

Lakini bila kufahamu nafasi yake haikuwa ni ya kudumu mahali hapo na wengi watu wasio waafrika hawakuwa wanafurahia kwa mtu kama Dr Tedros kushika nafasi hiyo na kuzungumza na vyombo vya habari vya dunia.

Wiki ilopita bara la Afrika na waafrika walitoa kauli za kumuunga mkono Dr Tedros huku mwenyekiti wa Umoja wa Afrika bwana Moussa Faki Mahamat akisisitiza umoja kwenye kupambana na ugonjwa huo hatari.

Rais Kagame wa Rwanda nae alitoa kauli yake kupitia mtandao wa Twiter kusema kwamba huu si wakati wa siasa bali nguvu ya pamoja kupigana na ugonjwa wa COVID-19. Viongozi wengne walotoa kauli za kumuunga mkono Dr Tedros ni wa nchi za Afrika Kusini, Namibia na Nigeria.

Lakini mazingira yanayozidi kutengenezwa yanaweka njia ya kuondolewa kwa mtaalam huyo ili mataifa ya magharibi yweze kutekeleza ajenda zao.

Dr Tedros anajaribu kuunganisha juhudi kwa nchi wanachama wapatao 194 zijitahidi kuchangia shirika hilo na akifanikiwa kwenye hili basi atatoboa.
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,709
2,000
"Taarifa hizo zimeeendelea kudai kuwa kulikuwa na mwanafunzi wa kike katika maabara hiyo ambae hakufuata protokali za matumizi ya maabara hiyo na kwenda nyumbani akiwa ameambukizwa kirusi hichi kicha kwenda kumuamnukiza rafiki wake wa kiume ambae naeoi Kesho yake alikwenda kwenye soko la wanyama ambalo halikuwa katika mazingira mazuri ya usafi.

Raisi Donald Trump akihojiwa na mwandishi wa Fox News bwana John Robert ambae aluliza kwamba, ‘Multiple sources are telling Fox the US government now has high confidence that while the coronavirus is a naturally occurring virus, it emanated from a virology lab in Wuhan."

Nilivyosoma tu hio part niliyoi-quote hapo juu nikajua nimepoteza muda wangu kusoma vitu vya kijinga jinga.

Inshort nimepoteza muda wangu buuuuuure.
 

Mapensho star

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
2,687
2,000
ata mimi nimeona kuna mapungufu kwenye hilo shirika wanatoa maelekezo ambayo hayana uhakika sana hii imepelekea dunia iangamie kuna pesa haitumiki vilivyo kufanya utafiti
walisema barakoa inabidi wavae wahudumu tu na wagonjwa ila sasa wamekuja na utafiti mwingine kwamba wote wavae maambukizi yanasambaa kupitia hewa
 

Joh Doe

JF-Expert Member
Sep 23, 2019
441
1,000
We need to stop playing the race card here. The WHO failed. The dude is incompetent and failure. They should have had a clear warning system. Individual countries can ignore the warning but it was clearly needed. This is part of their mandate.

The ones who started all this was WHO giving false information. People didn't know it was serious until it was too late.

The WHO;
  • Claimed there is no human to human transmission
  • Said travel bans are not necessary
  • Praised China after they lied Covid-19 is under control
  • Told us to wash our hands and wearing mask is not necessary
Never trust anything that comes out of WHO. They're like headless chickens running around in all directions.

This is just the beginning, the world will never be the same as many things are bound to change.
 

ATRACURIUM

JF-Expert Member
Jul 2, 2018
722
1,000
Wiki ilopita bara la Afrika na waafrika walitoa kauli za kumuunga mkono Dr Tedros huku mwenyekiti wa Umoja wa Afrika bwana Moussa Faki Mahamat akisisitiza umoja kwenye kupambana na ugonjwa huo hatari.

Jr

Rais wa Uganda anaongelea Covid19, Rais Uhuru, Kagame, Trump etc locally and international wanaongelea Corona, mbona wewe husikiki mkuu au kwa vile jamaa wamebana mpunga nawe wasusa?
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,709
2,000
Kama mfadhili mkuu wa WHO (Marekani) anataka huyo mkurugenzi aondoke basi lazima ataondoka tu.

Hata hao viongozi wa Africa wanaomtetea Dr Tedros yaani kina Kagame,Buhari na Ramaphosa wanafahamu vizuri hilo.
Na aondoke tu ili wamarekani weusi wa huku wilaya ya Nzega waelewe beberu Trump hataki mazoea na Ma-shithole Niggas wenye vyeo huko WHO.
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,675
2,000
Sasa kama China walificha data, Trump alitegemea WHO ndo wakafanye investigation na kuupata ukweli kwa 100%? I thought CIA wapo kwa kazi kama hizo?

Trump anadeflect attention tu. Huyu ndugu alitonywa tangu Nov 2019 ila kwa kuwa ni mtu wa kiburi na dharau, he didnt care at all. Yeye mwenyewe alimsifu sana Presidend XI katikati ya Jan 2020. Yaani mpaka early March Trump bado alikuwa anabishabisha tu

Dr. Tedros wanamuandama bure kwa kuwa ni Mwafrika. Hii kitu ina chembechembe zote za ubaguzi


1587031031555.png
 

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
6,542
2,000
Kama mfadhili mkuu wa WHO (Marekani) anataka huyo mkurugenzi aondoke basi lazima ataondoka tu.

Hata hao viongozi wa Africa wanaomtetea Dr Tedros yaani kina Kagame,Buhari na Ramaphosa wanafahamu vizuri hilo.
Wakati CORONA inashika kasi jamaa anaongelea mambo ya FIFA...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom