Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kutoka Diamond Jubilee Mkutano Mkuu wa ACT–Wazalendo: Membe apata kura za Ndiyo 410 za Urais Tanzania, Maalim Seif Ndiyo 419 za Zanzibar

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
617
1,541
Chama cha ACT–Wazalendo leo tarehe 05 Agust 2020 kinafanya Mkutano wake Mkuu Diamond Jubilee–VIP Hall.

#MkutanoMkuuACT2020
#KaziNaBata
#TheFutureIsPurple
=====

UPDATES

======

#UCHAGUZI2020: MEMBE, MAALIM KUPEPERUSHA BENDERA ZA ACT WAZALENDO URAIS TANZANIA NA ZANZIBAR

- Chama hicho kimempitisha Bernard Membe kuwa mgombea Urais wa Tanzania kwa kura 410 za 'Ndiyo' kati ya kura 420

- Maalim Seif amepitishwa kuwa mgombea Urais Zanzibar kwa kura za 'Ndiyo' 419 kati ya kura 420
AJENDA KUU

1. Kupitisha na kutangaza majina ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar

2. Kupitisha Ilani ya Chama ya 2020 kwa Uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano na Uchaguzi wa Zanzibar.

Sasa kinachoendelea na utambulisho na Ufunguzi kwa Maombi kutoka Madhehebu mbalimbali.

1153HRS: Maalim Seif anaingia kufungua Mkutano rasmiACT.JPG

Hotuba ya ufunguzi -- Maalim Seif Hamad

Ndugu kiongozi wa chama, ndugu makamo wa mwenyekiti, ndugu katibu mkuu na manaibu wako. ndugu wajumbe wa kamati kuu ndugu wajumbe wa halmashauri ya kamati kuu ya taifa ndugu wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa ndugu, ndugu wajumbe na wananchi na ndugu waalikwa wageni wetu.

Ndugu wananchi mkutano mkuu wa chama chetu leo umekutana, nina furaha kubwa kuwa leo tupo tumejumuika hapa kwenye mkutano mkuu wa chama hiki chenye miaka 6 tokea kuanzishwa kwake ni chama kichanga kuliko vyama vyote na kwakweli pamoja na uchanga wake ndugu Membe aliwahi kusema kuwa ni chama kinachokuwa kwa haraka kabisa.

Ngugu viongozi nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kukutana tena mara ya mwisho tulikutana mwezi Machi tulipokuwa na mkutano mkuu wa kawaida na mwezi huu wa nane tunakutana kwa mkutano mkuu maalum.

Ndugu wajumbe nichukue nafasi hii kuwashuru wote ambao mmetoka sehemu zote Tanzania, Tanzania bara na Zanzibar katika mikoa yote na majimbo yote mkaweza kufika hapa kwa umoja wenu na kwa wingi wenu nafahamu kwamba safari ni tabu mmepata mihangaiko mikubwa kwenye mabasi kwenye maboti lakini mioyo yenu uzalendo wenu hamkujali yote hayo umefika kwa wingi hapa .

Niwashukuru wageni ambao wametupa heshima ya kukubali mwaliko wetu na kuweza kufika hapa kutuunga mkono asante sana na kamati ya maandalizi ambo mwezi mzima hawalala wanatayarisha mkutano huu nao wanastahili pongezi asante sana na kamati hiyo inaongozwa na Naibu katibu mkuu wa Zanzibar ndugu Nasoro Hamed Mazurui tunawapongezi .

Ndugu wajumbe iwapo itatokea mapungufu yoyote tunaomba samahani sana hatukukusudia yametokea kwa sababu ya ubinadamu hivyo tunaomba samahani sana.

Ndugu wajumbe tumeelezwa maudhui moja ya mkutano huu ni kupata viongozi ambao watapeperusha bendera ya chama chetu kwenye ngazi ya urais tunaomba tuwachague ambao tuna imani kwamba tukiwakabizi bendera yetu wataweza kushinda na pia kuunda serikali na kuitekeleza ilani yale ambayo yameahidiwa kwenye ilani ya chama chetu.

Wananchi mnajua miaka 59 ya utawala wa CCM walipoifikisha nchi hii, watu wamekuwa masikini zaidi na kila uchao umasikini unazidi wananchi wamekuwa wajinga zaidi na kila uchao ujinga unazidi maradhi yametamalaki katika nchi yetu wenzetu ni kujisifu tu lakini katika miaka hii mitano hii ya mwisho kumalizia mwaka huu hali mbaya zaidi.

Zaidi mwananchi sasa huna uhuru katika nchi yako mwenyewe tumemwondoa mkoloni tujitawale ili sisy wenyewe tuendeshe nchi hii na nchi hii ni ya watanzania wote sio nchi ya mtanzania mmoja na wala sio nchi ya kikundi fulani sote ndio tunamiliki Tanzania kwa hivyo kwa kweli tunastahili kuchukia sana haya mabayo yanatendeka leo raia huna uhuru leo vyombo vya habari havina uhuru leo ukisema kitu mpaka uangalie huku na huku usikiki na mtu mwingine na hii sio Tanzania tunayoita wala sio Tanzania ilitakwa na Nyerere na Karume hii ni Tanzania nyingine kabisa kinyume na matakwa ya watu wa na waasisi Taifa hili.

Jana nikizungumza na mtu mmoja kuwa wametoa kanuni za maudhui ya mtandaoni akasema kila anaetaka kuandika lazima awe amepewa kibali kwamba mtu yoyote haruhusiwi kuandika maudhui mtandaoni mpaka awe na kibali.

Tukishindwa kihalali tutakubali na mimi mtu yoyote atakayeshinda kihalali kule Zanzibar nitampa mko kabisa lakini na sisi tukishinda msije mkafanya makosa mbinu na hadaa ya kunyang'anya kabisa kabisa mara hii tumekusudia kulinda nguvu ya maamuzi ya wananchi sawa sawa.

Hutuba ya Zuberi Zitto Kabwe

Ndugu Wajumbe Mkutano Mkuu,
Ndugu Wananchi wa Tanzania,
Ninafuraha kubwa sana kuwa leo tupo tumejumuika hapa kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Chama chetu hichi chenye miaka 6 tokea kuanzishwa kwake. Ni chama kichanga kuliko vyama vyote vilivyopo Tanzania kwa umri wake. Taaswira ya Mkutano huu ni tofauti kabisa na umri wa chama chenyewe. Mkutano huu umejumuisha Wajumbe kutoka kila kona ya nchi yetu. Hongereni sana wana ACT kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kujenga Chama imara. Kwa taaswira hii sina mashaka baada ya October 2020, ACT kitakuwa ni chama kinachoongoza Serikali.

Ndugu Wananchi wa Tanzania,
Wiki chache zijazo tutaanza kuzunguka nchi yetu, kila Kijiji, kila Kata na kila Jimbo kuzungumza na Wananchi kuhusu maono yetu juu ya nchi yetu. Tutawapa Wananchi machaguo ya aina ya Watanzania wanayotaka kuishi katika miaka mitano inayokuja – Wananchi watakuwa na chaguo la wazi kati ya Tanzania wanayoishi sasa au Tanzania mbadala ambayo sisi ACT Wazalendo tunataka kushirikiana nao kuijenga. Sisi tunakwenda kuwashirikisha Watanzania, wabara na wa Zanzibar, aina ya Taifa tunalotamani kuwa nalo - Tanzania yenye watu wenye hali bora kijamii na furaha ya kweli, yenye kujali utu, yenye mfumo mzuri wa utoaji haki, yenye demokrasia ya kweli, yenye uhuru na yenye uchumi jumuishi, imara na unaostawi”

Katika Miezi 2 ya kuzunguka huko tutakuwa tunakamilisha zoezi muhimu la kikatiba la kila miaka 5 Watanzania kupata fursa adhimu ya kuchagua viongozi wao. Uchaguzi wa mwak huu ni uchaguzi muhimu sana katika maisha ya Taifa letu. Kiongozi Mkuu wa Taifa tunayekwenda kumchagua na Wawakilishi wetu katika Baraza la Kutunga sharia na mabaraza ya madiwani ndiye atakayetuongoza kuingiza nchi katika muongo wa sita tangu Tanganyika ipate uhuru na tangu Jamhuri ya Muungano iundwe. Vile vile tunakwenda kuchagua Kiongozi ambaye ataiongoza Zanzibar kuingia muongo wa sita tangu Mapinduzi ya Zanzibar. Kwa uzoefu wa miaka mitano iliyopita Watanzania wanakwenda kufanya maamuzi muhimu sana.

Uchaguzi wa mwaka 2020 ni uchaguzi wa kuchagua
- Uhuru wa kweli kwa kila mtu dhidi ya ukandamizwaji,
- Matumaini dhidi ya hofu,
- Amani na usalama kwa kila mtanzania dhidi ya tafrani na misukosuko
- Siasa safi dhidi ya siasa za chuki na za kizandiki
- Utaifa na mahusiano yenye tija kimataifa dhidi ya mgawanyiko na kujitenga
- Maendeleo Jumuishi ya watu dhidi ya maendeleo ya vitu,
- Utajiri wa watu dhidi ya utajiri wa serikali,

Muhimu zaidi ni uchaguzi wa kuchagua kurudisha utu na heshima kwa kila mtanzania hasa wanawake na watoto dhidi ya kejeli, manyanyaso ya makundi fulani ya jamii yetu. Ni uchaguzi wa Watu dhidi ya Uchaguzi wa Vitu.

Mkutano Mkuu huu wa chama chetu leo utafanya maamuzi muhimu ya ajenda hizi za uchaguzi wa mwaka huu na watu watakaobeba ajenda hizi. Ni matumaini yangu kuwa mtawapa Watanzania wagombea ambao kwa kuwatazama tu watarejesha nyuso za furaha na matumaini ambayo yamepotezwa katika miaka mitano iliyopita.

ACT wazalendo imedhamiria na kujiandaa kikamilifu kujenga na kuongoza Tanzania ya Watanzania. Tanzania ambayo kila mtanzania, mtoto, kijana, mwanamke, mwanamume, mzee, wa kijijini na mjini ana haki sawa mbele ya sheria na ana fursa stahiki za kujenga na kuzifikia ndoto zake. Tanzania ambayo, watanzania wanajivunia kuwa watanzania na sio Tanzania hii ya sasa ambayo mamilioni ya watanzania wanavumilia kuwa watanzania.

Chama cha ACT Wazelendo kinaamini kwa yakini, miongo inayokaribia sita tangu tupate uhuru wetu kutoka kwa mkoloni, watanzania na Wazanzibari, hawapaswi na hawastahili kuishi kwa hofu na kufifishwa ndoto zao, bali wanapaswa kuwa wenye raha na furaha, na matumaini yakufia na kuishi mafanikio yao binafsi na kuwa sehemu ya mafanikio ya taifa kwa ujumla.

ACT wazalendo inataka kuunda Serikali ambayo itahakikisha upatikani na ulinzi wa haki na ustawi wa wanawake ambao ndiyo ni walezi wa taifa hili, watu wenye ulemavu, watoto hasa walioko kwenye mazingira magumu, jamii na makundi yaliyopo pembezoni. Tafiti za kisayansi zimeonyesha na kuthibitisha kuwa kuwezesha na kuwekeza kwa wanawake na makundi mengine maalumu, kuna tija endelevu kiuchumi na kijamii. Muhimu zaidi, kunaleta umoja na usawa katika jamii.

Tunataka Serikali ambayo sio tu itatokomeza ubaguzi ila pia itafanya jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa kila mtanzania, bila kujali jinsia, dini, maumbile, itikadi, umri, kabila, anashiriki kikamilifu katika kuongoza taifa hili katika nyanja mbalimbali na anaishi maisha yenye mafanikio, maisha ya raha na furaha. Kauli mbiu yetu ya #KaziNaBata ni dhana jumuishi, kwa sababu kila Mtanzania, ana haki ya kufurahia utanzania wake, na maisha yake. Tunataka Watanzania wafanye Kazi kwa bidii na pia wafaidi matunda ya jasho lao. Wawe na Raha na Furaha. #KaziNaBata.

Kwenye Taifa lenye zaidi ya 80% ya watu wake wakiwa na umri chini ya miaka 35, ni dhamira yetu, kuwekeza na kutengeza sera, sheria na taratibu zitakazohakikisha kuwa vijana wa taifa hili wanakuwa kipaumbele na chachu ya maendeleo, kwao wao na kwa taifa. Tunataka Serikali zitakazoongozwa na ACT Wazalendo, zikatae kuona vijana wa Nchi zetu mbili wananyang’anywa fursa, wanakatishwa ndoto zao, wanakandamizwa na kufanywa watwana ndani ya taifa lao.

Tunataka kuona Serikali itakayoundwa na ACT Wazalendo, kuwa serikali ya vijana kwa ajili ya vijana wa Tanzania wa kike na wa kiume. Lakini pia kuandaa maisha stahiki uzeeni kwa kuwa na Mfumo Madhubuti wa Hifadhi ya Jamii kwa wote ambayo itahakikisha kuwa kila Mtanzania na kila Mzanzibari anakuwa na Bima ya Afya na Pensheni akifika umri wa kutoweza kufanya kazi.

Tunataka kuhakikisha kuwa huduma za jamii bora, zenye ufanisi zinatolewa kwa wakati stahiki hazitakuwa na upendeleo kwa viongozi au watu wachache, bali zitakuwa kwa kila Mtu.Tunataka tuwe na Elimu bora yenye kukidhi vigezo vya soko la ajira na kuwaanda wahitimu kuvumbua na kujiajiri. Hatutaki kuona vijana wamalizapo vyuo vikuu au vyuo vya ufundi kuwa na mzigo wa madeni ndio maana Serikali itachukua mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa Elimu ya Juu mpaka sasa ili kuondoa mzigo kwa vijana kuhudumia madeni hayo na kuanza upya mfumo wa kugharamia Elimu kwa kutoa ufadhili wa gharama za masomo ‘tuition fee’ bure kwa Watu wote watakaodahiliwa kwenye vyuo vya Elimu ya Juu na Vyuo vya Ufundi Mchundo.

Vijana wote watakaojiunga na Elimu ya Ufundi ya VETA watasoma bila malipo ili kuondoa kikwazo cha vijana kupata Stadi na ujuzi kuendesha maisha yao. Vijana wanaonisikiliza leo wana chaguo la wazi kabisa – kuchagua chama na mgombea wa chama ambacho kitaendelea kuwaweka katika mnyororo wa madeni au kuchagua chama na mgombea wa chama ambaye atawaondoa katika utumwa wa madeni ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani.

Tunataka Serikali ambayo itahakikisha Huduma bora za afya kwa watu wote na sio Serikali inayotamba kwa kujenga majengo. Chaguo kwa Wanawake waja wazito lipo wazi katika uchaguzi wa mwaka huu – kati ya chama na mgombea wa chama ambacho kitaendelea kulipisha huduma za afya na kugeuza afya kuwa bidhaa kama nyanya sokoni kuchagua chama na mgombea wa chama ambaye atahakikisha kila Mtanzania ana Bima ya Afya na ana hifadhi ya Jamii ambayo ina mafao yatakayomwezesha asiwe na mashaka kabisa apatapo majanga. Ni uchaguzi ulio wazi kabisa.

Tunataka Serikali ambayo itahakikisha upatikaji wa maji safi na salama kwa kila mtu. Watu wenye kipato kidogo hapa nchini wana chaguo la wazi kabisa katika uchaguzi wa mwaka huu – kati ya chama na mgombea wa chama ambacho kitaendelea kuwafanya masikini walipie maji kwa gharama kubwba zaidi kuliko watu wenye kipato kikubwa na mgombea wa chama ambaye atahakikisha kuwa ndani ya miaka mitano watu wote wanapata maji na salama kwa kutekeleza mradi wa kimkakati wa ujenzi wa miradi ya Maji yote nchini kwa pamoja kwa kutumia maarifa ya fedha za maendeleo.

Ndugu wajumbe,
Kwa Wananchi wa Zanzibar wana hiari ya kuamua kati ya chama na mgombea ambaye ataendelea kuifanya Zanzibar kuwa duni kimaendeleo kwa kukandamizwa na upande mmoja wa Muungano kwa sababu tu Mkuu wa Serikali ya Muungano hataki kutoa shikamoo; na chama na mgombea ambaye atahakikisha kuwa kwanza Zanzibar inatumia kikamilifu mamlaka yake yaliyo kwenye Katiba ya sasa ya Muungano na Katiba ya Zanzibar na pili atakaye hakikisha kuwa Muungano unaimarishwa kwa kufanya mabadiliko makubwa ya mundo wa Muungano ili kuwa na Muungano wa Haki, Usawa na wenye kuheshimiana.

Ndugu Wajumbe, Ndugu Watanzania,
Uchaguzi wa Mwaka huu unahusu pia uchumi wenu. Unahusu maisha yenu ya kila siku. Hatma ya maisha ya kila Mtanzania ipo mikononi mwake sasa na ataamua tarehe 28 Oktoba 2020.

Ninataka kuwahakikishia kuwa Uchumi wa taifa litakaloongozwa na serikali ya ACT Wazalendo utakuwa Uchumi Jumuishi;

- UCHUMI WA WATU SIO VITU.
- Uchumi wa Wananchi walio wengi na si uchumi wa Serikali na kundi la wachache.
Tunataka Serikali itakayowekeza kwenye sekta zinazoajiri watanzania wengi, hasa Kilimo, Ufugaji na uvuvi, ili kuleta kilimo cha kimapinduzi ambacho kitawaondoa Wakulima, Wavuvi na Wafugaji kutoka katika dimbwi la umasikini. Wakulima, Wavuvi na Wafugaji wa Tanzania wana uchaguzi ulio wazi kabisa – kuchagua chama na mgombea ambaye kwa miaka mitano amewadharau, kuwapora fedha zao na kuwafukarisha kwa kuchoma nyavu zao au kuwaondoa kwenye maeneo ya malisho AU kuchagua chama na mgombea ambaye anatambua umuhimu wa kilimo na atawekeza kwenye kilimo na kujenga ushirika wa kisasa wa wakulima, wavuvi na wafugaji ili kulinda haki zao na kuboresha maisha yao kutokana na shughuli zao.

Tunataka Serikali ambayo itaboresha na kuwezesha ustawi wa sekta isiyo rasmi hasa ya biashara ndogo ndogo ambazo nyingi zinafanywa na wanawake na vijana. Mifumo ya kodi na urasimishaji biashara vitalenga katika kuleta ufanisi na kukuza biashara na si kudumaza na kuleta ukiritimba. Tafiti, sayansi na tekinolojia vitakuwa chachu katika kutengeneza fursa na kukuza uchumi jumuishi. Serikali yetu itahakikisha wataalamu wa fani mbalimbali wanawekewa mazingira sawia ili walisaidie Taifa katika kukuza uchumi ambao unaboresha maisha ya mtu mmoja mmoja.

Ndugu Wajumbe na ndugu Watanzania,
Tunataka Serikali ambayo inatambua mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi yetu. Wafanyabiashara nchini wana chaguo la wazi kabisa mwaka huu. Kwa Wafanya biashara huu ni uchaguzi kati ya;

- Chama na mgombea wa chama ambaye anaweza kuamka asubuhi na kutegemea na alivyoamka na kuvunja mikataba ya kisheria dhidi ya Chama na mgombea wa chama ambaye ataheshimu mikataba na malipo na migogoro kutumia njia halali kutatua migogoro hiyo
- Chama na mgombea wa chama ambaye anakusanya kodi kwa mitutu ya bunduki dhidi ya chama na mgombea wa chama ambaye ataheshimu sheria na kukusanya kodi kwa mujibu wa sheria bila kupoka uwezo wa makampuni kuzalisha mapato zaidi.
- Chama na mgombea wa chama ambaye akiamka asubuhi na kutegema na alivyoamka anaweza kuingia kwenye akaunti ya benki ya mfanyabiashara na kuchukua fedha zake dhidi ya chama na mgombea wa chama ambaye ataheshimu haki za watu kumiliki mali.

Ndugu Wajumbe na ndugu Watanzania,
Tunataka Serikali ambayo itajikita katika kufufua na kuimarisha uhusiano wetu na mataifa mengine na haswa nchi jirani. Tumedhamiria kurudisha heshima ya Tanzania kwenye medani ya kimataifa. Nikiwa Kiongozi wa chama hiki napenda kuwahakikisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa chama chetu na Wagombea wote wawili watakaopitishwa na chama chetu watajitahidi kwa nguvu zao zote kuimarisha utangamano wa eneo letu la kikanda. Hapatakuwa na siasa za tit for tat, kuchoma vifaranga wala kurushiana maneno. Ninukuu maneno ya Rais John F Keneddy ya mwaka 1961 akihutubia Bunge la Kanada;

“Geography has made us neighbors. History has made us friends. Economics has made us partners, and necessity has made us allies. Those whom God has so joined together, let no man put asunder”.

ACT Wazalendo itaenzi juhudi za viongozi waliotangulia kuimarisha Afrika Mashariki moja, imara na inayoheshimiana. Watanzania wataamua hivyo mwaka huu.

Ndugu wajumbe na Watanzania,
Serikali yetu ya #KaziNaBata haitaweza kufikiwa kama wasanii na wanamichezo wataendelea kunyonywa na kufanya kazi katika mazingira magumu. Kwa kushirikiana na wasanii na wanamichezo mbalimbali, serikali yetu itawekeza kwa kiwango kikubwa kuhakikisha vipaji na vipawa vya watanzania vinakuwa vyenye tija kwao, burudani kwetu na tunu ya taifa katika majukwaa ya kimataifa. Sanaa na Michezo itakuwa ni moja ya vipaumbele vya Sera yetu ya mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa ili kujenga taswira chanya ya Nchi yetu na kuongeza Mapato ya Fedha za Kigeni. Serikali zote mbili ile ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar zitahakikisha kuwa michezo na burudani inaimarika.

Ndugu Wajumbe,
Chama chetu cha ACT Wazalendo kimeongoza juhudi za kuona tunakuwa na mashirikiano na vyama makini katika uchaguzi huu. Mwenyekiti wetu amefanya kazi kubwa sana ya kuwasilisana na baadhi ya viongozi wa vyama kufanikisha hili. Kwetu sisi ushirikiano na vyama vyengine vya siasa vilivyo makini ni jambo muhimu sana katika kukabiliana na CCM. Tunaamini kupitia ushirikiano na vyama vyengine, kazi ya kuiondoa CCM Madarakani inakuwa rahisi mno kuliko kila chama kupigana kivyake.

Nitumie fursa hii kuwahakikishia Watanzania kuwa ACT tumefanya na tutaenelea kufanya kila lilo ndani ya uwezo wetu kuona tunapata mashirikiano na vyama vyengine vya siasa. Tunafahamu suala la ushirikiano ni hitajio la watanzania walio wengi wanaotaka mabadiliko. Niwahakikishie Watanzania wanaonisikiliza muda huu kuwa chama ninachokiongoza mimi chini ya uwenyekiti wa Maalim Seif ambaye sote sisi wana mageuzi wa zama hizi tunachukua busara zake hakiwezi kuwa Mchawi wa ushirikiano, Niwaambie mpaka muda huu ninapozungumza bado mashauriano yanaendelea na kwenye Mkutano huu pia Wajumbe mtapokea tarifa ya mashauriano haya ili nanyi mtupe muongozo wenu.

Ndugu Wajumbe,
Leo mtapokea pia tarifa ya maandalizi ya Ilani ya uchaguzi itakayowezesha yote niliyoyataja hapo juu. Niwaambie kuwa Wajumbe wa Kamati Kuu na Halimashauri Kuu wamefanya kazi kubwa ya kutupatia ilani bora ili wagombea wetu waweze kuwa na ajenda mahususi ya kutuwezesha kushinda uchaguzi mwaka huu.

Ilani hizi ni dhamira ya chama katika kuifikia na kuijenga Tanzania ya watanzania na Zanzibar ya Wazanzibari, zaidi ni mkataba kati cha chama na watanzania na chama na Wazanzibari. Sisi, ACT Wazalendo tunaamini na tunawataka watanzania waamini pamoja nasi kuwa, INAWEZEKANA

 Kufanya kazi na kula Bata
 Kuishi Maisha ya Raha na Furaha
 Kuondoa Serikali dhalimu madarakani
 Kuwa na Serikali inayoheshimu sheria, utu, uhuru na ustawi wa watu wake
 Kujenga Uchumi jumuishi na endelevu
 Kila mtanzania kufikia ndoto zake
 Kuwa na umoja wa kitaifa na heshima kimataifa
Nawashukuru sana

Mwakilishi wa vyama vya siasa Tanzania - Sisti Nyahoza

Nipo hapa kumuwakilisha msajili wa vyama vya siasa ndugu Francis Mutungi na kama kawaida ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa tunahudhuria mikutano mikuu ya vyama vya siasa na vikao vya maamuzi ambavyo vinafanya maamuzi mbalimbali yanayohusu sheria yetu ya vyama vya siasa ili kujihakikishia kwamba vyama tulivyovisajili vinaendesha shughuri zake kwa mujibu wa kanuni na katiba mlizojitungi anyie wenyewe na kunakuwa na demokrasia na vinaendeeshwa kama taasisi ili tujenge demokrasia katika vyama vyenu.

Kwa hiyo kiongozi mkuu wa chama na mwenyekiti msisitizo tulio nao katika mikutano ya uteuzi wa wagombea urais ambayo tumekuwa tunahudhuri amsisitizo tulio nao ni kuheshimu sheria za nchi kuheshimu sheria ya vyama vya siasa muheshimu katiba zenu muheshimu kanuni zenu katika uteuzi wa wagombea na katika mchakato wa uchaguzi ambao unakwenda kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu .

Tunaelewa uchaguzi ni ushindani,tunaelewa kwamba kwenye siasa za ushindani kuna mbwembwe nyingi na hapa ameongea hapa mwenyekiti wa chama kwamba mtalinda ushindi na sisi tunasema mlinde kwa mujibu wa sheria, mwenyekiti fanyeni mbwembwe zote lakini kwa mujibu wa sheria zile barua zetu zile haziishi.

Kwa sababu lengo ni kuhakikisha tunaendesha mfumo wa demokrasia kwa mujibu wa sheria na sheria ndio itakayo fanya tuendeshe uchaguzi huu kwa haki uhuru na amani na utulivu tusipozingatia hamwezi kila chama msifuate sheria mko wengi na kila mmoja anataka kushinda, fanyeni mbwembwe zote lakini kwa mujibu wa sheria.

Oscar Makaidi Chama cha NRD

Nwapongeze kwa mkutano mzuri sana hakika mkutano huu unaonesha mbele kuna mafanikio makubwa sana pili niwapongeze kwa wagombea wenu chama kimepata wagombea makini Maalim Seif simsemei Kwa sababu wasifu wake ni mkubwa sana na pia mmepta Ndugu Membe ambae anahitajika kwenye siasa za zama hizi na naamini atapeperusha bendera ya chama chenu vizuri na tuna imani nae. Tunawaahidi ushirikiano tunaahidi kumuunga mkono Maalim Seif na Bernad Membe kama walivyosema viongozi mbalimbali vyama hivi ni lazima tushirikiane ili tuitoe CCM madarakani.

Mwaka 2015 tuliushirikia vyama 4 tu tukaunda UKAWA na chamoto walikiona na si lazima tuwe msusus wa vyama hata 4 vilevile vinatosha na sisi tunawaahidi ushirikaiano.

CHADEMA- Tundu Lisu

Ndugu zangu wa ACT Wazalendo nimeona marafiki zangu wengi sana hapa na niseme kuwa asanteni sana kwa kunialika kuja kushiriki nanyi katika mkutano mkuu wa chama sijashangazwa hata kidogo na mwaliko huu niliutegemea kwa sababu ni mwaliko wa marafiki ukweli ni kwamba hata msinge nialika ningejileta mwenyewe halafu nione wa kunambia hebu tuone kadi ya mwaliko.

Nawashukuruni sana nyie ni marafiki wa kweli washwahili wanasema akufaaye wakati wa dhiki ndiye rafiki na nyie ni marafiki wa kweli kwa sababu kuna kipindi mimi binafsi nilikuwa kwenye dhiki na nilipoamka nililala siku kadhaa na nilipoamka nikakuta nipo nchi nyingine na mazingira tofauti katika watu waliokuja kuniangalia na kunisaidia kunifariji katika dhiki yangu alikuja Maalim na alikuja na Babdun na alikuja Ismail Jusa na alikuja Salim Bimani nilimuona mahali na wazanzibari na watanganyika wa ACT walikuja kunifariji kwenye dhiki ile .

Kuna wengine sio tu walikuja Nairob kuna wengine walinifata hospitali Ubelgiji kaka yangu Zitto alikuja mara mbili sijui tatu na alikuja na familia yake kumwangalia Lisu na dada yangu Fatma alikuja Ubelgiji alikuwa ananililia pale kitandani nikamwambia yataisha. Kwa hiyo nyie wote ni marafiki wa kweli.

Hivyo naomba niseme hapa kuwa tupo pamoja tutakuwa pamoja na kila mtu amekubali kwa habari ya ushirikiano na tutashirikiana na kwa sababu tunaelewa tumewekewa mitego kwenye kwenye hili neno ushirikiano unaangalia kama kipande cha mkate kuna ndoano na sisi kama watu wazima tutaangalia wapi kuna mtego na wapi kuko salama, lakini niseme tutashirikiana tuko pamoja.

La pili mimi siku zote nikiwa kwenye kikao kimoja kiwe cha ndani au cha nnje na Maalim Seif Hamadi ninakuwa mdogo sana na ujana una mambo yake kuna watu wengi hapa nimewazidi umri lakini kwa Maalim mimi ni kijana, ujana una matatizo yake sisi vijana mara kwa sababu ya ujana wetu hatujui kwamaba kuna watu ambao wameacha kuwa watu binafsi kwa sababu ya mchango wao katika jamii na historia ya nchi wamekuwa ni taasisi na Maalim Seif Hamadi ni Taasisi umchukie umpende nae ni kiongozi wakihitoria wa kitaasisis Zanzibar. Na Maalim kama ni malipo ya kupigania haki ya wanzan=zibar amelipa kuliko gharama halisi wwangapi wanafahamu kuwekwa kizuizini yaani kufungiwa bila kosa unafungiwa tu hupelekwi mahakamani kuambiwa umekosa hiki ila unafungiwa, na huyu ameonja hiyo na hii ni miaka ya 80 kabla ya vyama vingi na wengi hapa tulikuwa wadogo au tulikuwa CCM hivyo tunapaswa kumheshimu sana huyu mzee.

Sisi wa CHADEMA na mie mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA hatutahujumu jambo lolote la kuhujumu harakati za miaka mingi za wazanzibar mnaweza kulihifadhi neno hili.

Na mimi na mgombea mwenzangu hatutakuwa wa kuilanisha ile kamba ambayo imetumika kunyonga maslahi ya wazanzibar kwa miaka mingi bali tutashirikia na ACT kuikata.

Sisis na ACT tutahakikisha wazanzibar wanaongozwa na viongozi wazanzibar, kuna watu wanasema wao ni viongozi wa Zanzibar lakini wametengenezwa Dodoma na wanaweka madarakani kwa nguvu ya mtut wa huku na sis na ACT tutahakikisha kwamba kwa mara ya kwanza tangu mwaka 64 Zanzibar inasema hawa ni viongozi wetu na hii ni serikali yetu , madhambi ya Tanganyika kwa Zanzibar ni mengi mno tunataka tusaidie madhambi ya Tanganyika kwa Zanzibar yanakwisha

Nisiwe msemaji mkuu wa pili maana huu ni mkutano mkuu wenu naomba niseme neno lingine la mwisho, Uchaguzi mkuu huu ni uchaguzi wa kihistoria, fikiria hii miaka mitano imekuwaje halafu fikiria tuongeze miaka mingine mitano kama hii fikiria tu itakuwaje maana tayari wanasema tutamwongeza atake asitake kwa hiyo ndugu zangu uchaguzi huu tukikosea tumekwisha, tukikosea Tanzania ya vyma vingi iko rehani na iko rehani kwa sababu hawajifichi ilitangazwa hadharani ilikuwa Singida tarehe 6/02/2016 siku wanaadhimisha na miaka 39 ya CCM alisema ifikapo mwaka 2020 atahakikisha amemaliza vyama vya upinzani ila bado tumesimama.

Kwa hiyo fikirieni tukimwongezea miaka mingine mitano itakuwaje. uchaguzi huu hauko sawa na uchaguzi mwingine wowote unaoweza kuufikiria, tukikosea ni sisi ndio tutakao poteza yeye hatashinda yaani ule utabili wa kwamba 2020 hatutakuwa na upinzani umefeli kabisa na sasa tunanguvu kuliko awali na sisi wa CHADEMA tunawagombea pote haijawahi kutokea sasa inabidi tuzungumze mambo ya ushirikiano .

Na baada ya vipigo tumekomaa kwelikweli na kuna siku tutamshukuru Magufuli kwa kutuondolea ujinga kwa vipigo vyake na sasa tuko tayari kwa uchaguzi wa Oktoba 2020 lakini sio tu tuna nguvu na ACT mna nguvu , chama dhaifu hakiwezi kuwa na mkutano mkuu kama huu wala kuwa na ilani kama hii niliyoisikia niwapongeze kwa hilo.

Matendo yao ya miaka mitano yamewaondolea ushawishi kila mahali, mimi nimekaa Ulaya miaka mitatu na Tanzania ya Magufuli haina rafiki hata mmoja nje na kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki rafiki yao ni yule mrithi wa Pierre Nkurunzinza, Hebu fikirni miezi michache iliyopita Rais Moi amefariki ameebda kuzikwa na Marais wanne waliopo madarakani na Marais wawili wastaafu akiwemo Hayati Mzee Mkapa, ameenda kuzikwa na waanzilishi wenzake wa jumuiya ya Africa Mashariki Kaguta Museven alikuwepo na Ben Mkapa alikuwepo wameenda kumzika mzee mwenzao.

Amefariki Mzee Mkapa na Mungu amuweke mahala pema peponi nani aliye kuja nambieni nani aliyekuja kumzika mzee Mkapa kutoka nje, alikuja mrithi wa Nkurunzinza, na kama unataka ushahidi wa kwamba Tanzania ya Magufuli imepoteza marafiki wa nchi yetu wote mfano ni huo.

Sisi watanzania pamoja na kwamba tuko Afrika mashariki lakini ni wanachama waanzilishi wa SADC sisi ndio tuliochangia mapambano ya uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika tulilipa gharama ya SADC leo hii tuko wapi katika SADC leo hii tumepoteza marafiki wa kihistoria tumepoteza majirani zetu mara yamwishi ulimsikia Magufuli ameenda Adia Ababa lini kwenye mkutano wa AU lini? sasa nje ya Afrika ndio usiseme.

Sasa nachotaka kusema ni kwamba mazingira ya kimataifa yamebadilika sana hata wachina amewapoteza wachina wanataka kufanya biashara na mtu anejua biashara Magufuli anajua biashara?

Kwa hiyo kimataifa wametengwa ndani yanchi wamefanyaje kuna wafanyabiashara hapa kwisha, watumishi wa umma nani anemuunga mkono humu wamebaki wanaimba nyimbo za CCM kwa sababu za kutishwa tu sasa serikali ambayo imebaki inategemea mapolisi tu wamebaki wanatumia nguvu ya polisi tu itadumu madarakani muda gani kwa hiyo nikisema sisi ndio tutakao poteza uchaguzi huu nina maana hiyo wamebaki na nguvu ya dola tu hawana kingine.

Sasa naomba nipendekeze kenu halafu nishuke, njia ya kwanza ya kutushinda ni katika kutuengua wakati wa mchakato wa uteuzi hiyo ndio silaha pekee waliyonayo ndio inabidi tuitafutie dawa na dawa yake sio kutegeana kwamba aenguliwe huyu mimi niingie dawa yake ni kusema hadharani kwamba jaribuni muone .

Tunasema hii kwa watu wetu ili watuelewe na tutaisema hii kwa Dunia ili watuele kwamba hatutakubali kuengeliwa kihuni tutaingia barabarani, tukienguliwa kihuni hatutakubali weka hili kwenye kumbukumbu .

Nawaombeni ndugu zangu ACT tuwe na kauli moja kwenye hili CCM isipate ushindi kwenye meza ya tume ya uchaguzi na wasimamizi wa uchaguzi na wale wasimamizi ambao huwa wanakimbia maofisi wakimbie kipindi hiki waone, wakikimbia tukaikuta ofisi wajue hiyo ofisi ni halali yetu hatutakubali kuenguliwa kihuni tunataka tushindwe kwenye box la kura na sio kwenye meza ya tume ya uchaguzi SISI TUMESEMA SASA BASI.

Niwapongeze kwa mwaliko huu na niwaombeni tushikamane twende mbele pamoja nilitaka kusahau waliambiwa kuwa mimi nakupa gari na mshara mzuri halafu unatangaza wapinzani watatutangaza kwa sababu atakayediriki kutotutangaza wakati tumeshinda tutakutana barabarani, nataka rafiki atuelewe, adui atuele na dunia ituelewe na naamini dunia inatuunga mkono.

Kaka yangu Membe nikupongeze sana karibu kwenye mapambano huku ni kugumu na sisi tuna miaka mitano ya kuthibisha huku kulivyo kugumu na kama umeingia huku uko tayari kwa mapandano . Asanteni sana.

1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.jpg
5.jpg
6.jpg
8.jpg
9.jpg

 
Lakini chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, kilipofanya mkutano wake mkuu, kituo hicho pamoja na vingine, viligoma kabisa kurusha LIVE mkutano wao!

Mkae mkao wa kula kwani mwisho wenu, ni mwezi October wa mwaka huu, ili mkabidhi kwa amani kwa Shujaa Tundu Lissu atakayekuwa amepata ushindi wa Tsunami, katika uchaguzi mkuu ujao
ACT wazalendo wamelipia bwashee!
 
Lakini chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, kilipofanya mkutano wake mkuu, kituo hicho pamoja na vingine, viligoma kabisa kurusha LIVE mkutano wao!

Mkae mkao wa kula kwani mwisho wenu, ni mwezi October wa mwaka huu, ili mkabidhi kwa amani kwa Shujaa Tundu Lissu atakayekuwa amepata ushindi wa Tsunami, katika uchaguzi mkuu ujao
Na iwe hivyo, AMEEEN!
 
Lakini chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, kilipofanya mkutano wake mkuu, kituo hicho pamoja na vingine, viligoma kabisa kurusha LIVE mkutano wao!

Mkae mkao wa kula kwani mwisho wenu, ni mwezi October wa mwaka huu, ili mkabidhi kwa amani kwa Shujaa Tundu Lissu atakayekuwa amepata ushindi wa Tsunami, katika uchaguzi mkuu ujao
Badala mlipie mnataka mrushwe kwa huruma! Nchi ishatoka kwenye ujamaa kitambo sana
 
Kuna wakati najiuliza hivi upinzani ni fikira za kusadikika au ni fikira zinazo ishi

Kama kweli chama cha ACT WAZALENDO

Kilikuwa na nia ya kushirikiana na chadema kilipaswa kuachana na mpango huu kilipaswa kiseme tunaungana na chadema kwenye uraisi

Na kwenye ubunge wangetengeneza majimbo ya kimkakati hii ingeonyesha hapa ndio upinzan unakuja na maono ya kukua sasa na nyinyi mnachagua tena wagombea ili wakashindane na ccm au chadema

Inawezekana walio chagua upande mapema hata kama maamuzi yao yalionekana ya kipuuzi kuliko mnao chagua kugawana kura


Au chama cha Act ndio walitaka wasimamishe mgombea na wakati chadema ila raslimali watu

Kweli adui wa upinzan ni wapinzan wenyewe
 
Back
Top Bottom