Defining, Refining and Understanding Zitto Kabwe

Defining, Refining and Understanding Zitto Kabwe

Kishoka, Mkandara,

..hii hoja hata mimi imeanza kunichefua.

..huu mchezo anaoufanya Zitto wa kutumia jina lake na nickname Omarilyas ni utoto wa kupindukia.

..kitu kimoja nimejifunza ni kwamba Zitto/Omarilyas anahitaji muda akue.

Mkuu m,bona hao ni watu wawili tofauti na majina yao ni halisi?

Unataka picha zao(kidding)?
 
Waberoya,

..kwa hapa ilipofikia nahitaji Administrators privilleges ku-sort out suala hili.
 
Binafsi naona zito kama mwanaharakati yuko sawa kabisa, ni kijana wa kuigwa na vijana wengi wa kitanzania tunataka mtu anayejiamini na anayesimamia hoja yake mpaka mwisho kama mwanasiasa huwezi kuwa well defined, kila mtu anamjudge kutokana na msimamo wako na ueleo wako. Zito anatoa constructive criticism kwenye bunge ambazo ni za kisomi sio hadithi tu kama wabunge walio wengine ambao wamepitwa na wakati.
 
omy
sikujui ila unaonekana ni mtu wa karibu na zitto, na kama sio samahani..
kama watu wanajua wewe ni mtu wa karibu/mshauri wa zitto, wanafikiria zitto anawaona viongozi wa chadema ni magoigoi, na hiyo inamjengea chuki zitto na viongozi wenzake wa chadema...

lakini kama wewe unawaona viongozi wa chadema ni magoigoi (ni haki yako ya kifikira) ungejitenga na zitto hapa JF ili kuondoa mgongano...
na kama unataka kuwa karibu na zitto hapa JF inabidi umtendee zitto haki kwa kujibu majibu yako responsibly

Nadhani ushauri mzuri, Omarlyas unamweka kwenye wakati mgumu Zitto.



HAwa akina MWAFRIKA, Solomon, Julius wanatoa challenge tu na ni nzuri kuwa nazo katika maisha , Challenge zinakomaza na zina kuza, zinakupa mwanga wa kuangalia many dimensions.In other words na wewe unatoa same challenge kwao, ila zisiwe harsh

Wanapotoa mawazo wanasema kama wao, wewe nawe unapojibu jib u kama wewe Zitto asiwemo.

Zitto atabaki kuwa great leader of his time, na ndio maana kaanzishiwa thread, mimi nikianzishiwa thread humu, ni baada ya kufanya kituko ambacho ni unique sana! labda ugoni(God forbid)! tehe, tehe, tehe
 
Waberoya,

..kwa hapa ilipofikia nahitaji Administrators privilleges ku-sort out suala hili.

wako so close kiasi cha kuwa huwezi kutofautisha, Omar anakosea kwa kumwaga kila kitu humu, kiasi cha ww kuchanganyikiwa.

Omar ana hasira sana, akija kupewa uwaziri mkuu, lazima ataleta za Sokoine
 
Julius,

..ndugu yangu, utu uzima tu na kuangalia mwenendo wao hapa naona kama Zitto ndiyo Omarilyas. au labda nazeeka vibaya.

..kwa jinsi Zitto alivyo mkali na protective kuhusu image, misimamo, na mitazamo yake, angeisha m-disown na kumsimamisha Omarilyas asiendelee kumwaga sumu humu.

Jokakuu,

Zitto na Omarilyas ni watu wawili tofauti. Wote wanatumia majina yao halisi. Omarilyas alikuwa anatumia nick ya Tanzanianjema zamani ila akaamua kubadili na kutumia jina lake la kweli ambalo ni Omar Ilyasi.

Omar na Zitto wote wamesoma mlimani na ni marafiki wakubwa sana. Kama wanajua pw za kila mmoja na kuzitumia hapa, hilo siwezi kujua na sina hata chembe ya uthibitisho. Wakati mwingine inakuwa too convenient kwa Omar kuingia hapa kila mara zitto anapobwana. Je ni zitto anaingia kwa jina la Omar? Sina jibu katika hili ingawa ukweli ni kuwa Zitto na Omar ni watu walioko karibu sana na unaweza kudhani kuwa wanafikiri sawa.

Tofauti ya Zitto na Omar ni kwamba, Zitto ni mbunge lakini pia ni mpinzani wa ccm kisiasa (ni mwanachadema) ila Omar hajui kama awe mpinzani au awe mwanaccm.

Omar hana cha kupoteza baada ya kujitoa kwenye staff ya Zitto kiaina kwa hiyo hana ukaribu wowote na chadema na hajali kitakachotokea huko chadema. Mara nyingi nimekuwa namuuliza kama anachoandika ni mawazo yake binafsi au ni ya Zitto lakini amekuwa hasemi.

Wanaomfahamu Omar kama mimi, wanajua anachotaka - anataka kula pande zote mbili (za ccm na chadema). Usishangae sana kusoma anachoandika humu.

Habari ndiyo hiyo.
 
Rev. Kishoka,
Yaani hata sina nguvu tena na kumjadili mtu yeyote...after all, siwajui hivyo!

kweli sikio la kufa halisikii dawa
yani hawa watu gani wasioelewa, kila siku waonywe wao tu...
baada ya yaliyotokea kwenye uchaguzi wao tukategemea watajifunza
mabadiliko TZ bado ni safari ndefu sana..
 
...
Wanaona wao ndio wana haki ya kumtukana na kumzushia kila uozo na kugeuza maneno ya Zitto kila wakati wakitegemea Zitto hatakuwa tayari kuwajibu kwa maslahi ya chama chake.

Acha hizo omar,

Mbona Zitto alijibu kwa hasira nyingi sana na kutoa mambo yasiyo na uthibitisho wowote kuhusu kifo cha Wangwe na kuhusu jamii za wachaga ndani ya chadema na kwenye vyombo vya habari.

Unajua inachukua nguvu kidogo sana kumjua mnafiki, uchaguzi wa chadema ulimfunua Zitto kwa watu wengi sana waliokuwa hawamfahamu vyema.

..

Hawa jamaa wanapaswa kukaa chini na kufanya self reflection ya matatizo yao badala ya kukimbilia kutafuta mchawi kwa Zitto ama Omarilyas. Wachawi wao wenyewe wakiongozwa na sumu mbaya za Kiranja aka Mpakakieleweke....

Omar,

Hauna uthibitisho wowote kuwa Kiranja ndiye Mpakakieleweke. Hasira zako hizi mpaka unataka kuvunja sheria za JF?

Kuhusu kumuongelea Zitto, as long as wanakuja hapa na kwengineko na uzandiki wao i will not stop deciphering their cheap and loosy spinnings.....Kama wao wanadhani wana haki ya kumpaka uozo wao wa Zitto basi nami nina haki ya kupambana na uozo wao.

Acha vitisho mkuu,

Hata wewe uzandiki wako hautaachwa kupita hivi hivi. Wewe huitakii mema chadema na hili linajulikana wazi. Mbinu zako za kichochezi hizi nitakutana nazo sehemu yoyote, mahali kokote na wakati wowote ule.
 
Na wewe bana...sasa "undavyaundavya" ndio nini maana'ake?

Julius,

Wewe unamkosoa Mwl? Utakamatwa (msemo wa UD) wakati wa mtihani ... ohh shauri yako.

Kitila, heshima mbele mkuu, this is just a snack
 
Julius,

Wewe unamkosoa Mwl? Utakamatwa (msemo wa UD) wakati wa mtihani ... ohh shauri yako.

Kitila, heshima mbele mkuu, this is just a snack

Heheheheheee...nathubutu kufanya hivyo kwa vile nimekimbia huko. Ningekuwepo unadhani hata ningethubutu?
 
Zitto: Ushauri wa bure: Whenever you feel like saying "I" put "We". There is no "I" in a team with a common cause. Are thinking of "I" now ....mmmh dont say it put "We" then say whatever you want to say..... Ok. Always we we we we we ... right sio 'mimi', "mimi", "mimi":Sisi sisi Sisi.When there is too much I's people gets bored and always want to attack and it is a sign of lack of team work... which is very key ingridient in modern leadership...team work ... thenku ndugu Zitto
 
Zitto - who is Zitto! Made to think by rev and all of you. Who are my friends? Ninaanzia hapo. Kila la kheri
Kwa waliosoma vitabu vya Ngugi wa Thiong'o nadhani watamkumbuka character mmoja kwa jina Kabonyi. That is Zito. Bongolander kakuelezea vizuri sana hapo chini.
I beg to differ gents. I do not trust the guy, yes he is charismatic, energetic and may be pro-development. Lakini alivyoiyumbisha Chadema ameonesha kuwa he is somekind of an opportunist and somekind of self centred politician.

Mtu kama huyu akipewa kiti kikubwa anaweza kuburuzwa na kuyumbishwa, au anaweza kufanya mengi ya ajabu ambayo ni unpredictable.
You nailed it. Kwenye thread iliyokuwa inazungumzia ununuzi wa mmitambo ya DOWANS nilisema he is a traitor.

namsifu Mr.Zitto Kabwe kwa sababu ni muwazi na angalau anajali zaidi ya hayo ni jasiri, ni viongozi wachache wa ngazi yake wanaokuja hapa JF au kwenye mitandao mingine mikubwa ya siasa kuchangia mawazo yao na kusoma mawazo ya wengine wakiwa katika majina yao halisi...bila kujali kujadiliwa kulaumiwa, kuwa defined, refined etc...

I wish wote wenye madaraka mazito ktk nchi hii wangekuwa na ujasiri kama wake...
Ujasiri wa kuhalalisha tumlipe mwizi wetu?

Namwomba Zito azingatie yafuatayo akitaka:
1. Msimamo usioyumba. Bado anapungukiwa hili na limekigharimu sana CHADEMA kwenye chaguzi za Mitaa zilizopita. Angechaguliwa yeye kuwa Mwenyekiti wa Taifa hadithi ingekuwa nyingine sasa hivi kwa siasa za Nchi hii.
2. Umimi. Anajiimarisha yeye zaidi kuliko chama chake. Hili halitamfikisha popote zaidi ya kupata UMAARUFU. Awaulize akina Mrema waliotumia staili hii walikofikia.
Ameishia hapo hapo haendi zaidi kwani si mtu wa kujisahihisha

NL,
DOWANS, Zitto katoa misimamo miwili; kwanza alitaka TANESCO iinunue mitambo ile, pili kwenye press conference yake ya hivi karibuni akataka itaifishwe!
Buzwagi hakuna alichofanikisha pale. Mkataba umebaki uleule uloosainiwa London. Raisi alipounda ile tume ya Jaji Bomani na yeye akawemo. Wakawa wanalipwa Shs 350000/= kwa siku. Ripoti yao imefanyiwa kazi kiasi gani sijui.
Halafu eti watu wanataka tuamini ni mtu wa misimamo
Mkuu Next Level mimi simfahamu zitto sana ila kwa hii issue ya Dorwans nimeona hana msimamo kabisa maana mara iuzwe baada ya wananchi kuja juu angaangalia nitoke vipi akaja tena na kuitaifisha
That is what is about

Zitto ni msomi mwenye upeo mkubwa sana. Uwepo wake katika siasa za Tanzania ( Bungeni ) umeleta mwelekeo mpya wa uendeshaji wa bunge letu na siasa kwa kitaifa kwa ujumla wake.

Kama binadamu ana mapungufu yake, lakini by far mapungufu yana out-weigh mazuri.

Sakata la mikataba ya madini, ufisadi na hata kuanguka kwa serikali nzima (Richmond-gate) kote huko kna mkono wa Zitto.

Jamaa kwa umri wake na hata elimu yake amefanya makubwa sana kwenye siasa zetu kuliko akina Mzindakaya ambao tuna wasikia toka tukiwa wadogo, tunasoma na mpaka tu watu wazima. Wengine kwenye mabenchi yao bungeni kuna vishimo kwa kupiga makofi kuunga mkono miswada mbalimbali ya serikali.

Hakuna ubaya kutoa criticism kwani kwa namna bora kunamjenga na kumsadia mlengwa, lakini wengine mnakuwa critical kwa minajili ya kumkatisha mtu tamaa kwa sababu tu ya msimamo wake fulani ambao kwa namna moja au nyingine mtu haukumfurahisha. Nitoe mifano miwili ya haraka; suala la Zitto kugombea uenyekiti Chadema na yaliyojiri kutokana na hatua hiyo yameacha makovu kwa baadhi ya watu, lakini we need to get over it and move on. Whether it was bad move or good one let by gone be by gone. La pili suala la Dowans, hili limewagawa watu ( hususan washabiki/wenye mapenzi na Zitto ) kwenye mapande mawili. Ninachotaka kusema hapa ni kuwa katika hili Zitto kaweka msimamo wake tena very firm na if anything jamaa ndio kiongozi pekee alie wa face watanzania na kuwaeleza nini kifanyike kuliko hata hao wenye dhamana waliojifungia ndani na kushindwa kusema kitu. Haikuwa nia yangu kuleta mjadala wa Dowans hapa, lakini ninachotaka kusema Zitto ni zaidi ya Uenyekiti wa Chadema na Dowans, ana potential kubwa sana kwa taifa apewe ushirikiano sio kukatishwa tamaa na kama kuna criticism then basi ziwe constructive one.
Unatoa criticism na inakuwa constructive kama mtu anasikiliza kama ambavyo wewe umeanza kuwa msikivu. Nadhani labda kuna dalili za mafisadi kushindwa (lol) Mchukia Fisadi naona anakufahamu vyema
Kumbe kuna wakati akili zako huwa zinafanya kazi vizuri?
inaelekea mara nyingine ukisema mambo ovyo tofauti na hapa nitakupeleka Milembe!

Kwa nini tunataka Zitto alime, apalilie, avune, apike, ale na kutumezea chakula, kwa nini nasi tusijitume na kuungana naye katika uzalishaji mali na kwa kila hatua tunayotaka kuwe na mafanikio? Maana sielewi tunapoanza kudai afanye kila kitu, sisi tukae mkao wa kula tukifurahia nini?
Wote hatuwezi kuwa mjengoni. Mchango wetu ni mawazo na hayo tulimpa wakati kahongwa tununue dowans. Ka make 360 degrees turn bila kukiri alikosea.

May be I should twist the wind this way. Why are we seeking for Zitto to conform to our desires and needs rather than us conforming to his leadership syle and personality?
Our needs are to see a country without corruption. anybody who associates himself with this vice we can not conform with his leadership and personality.
Swali muhimu sana kaka.....watanzania bado tunashindwa kujenga utamaduni wa kidemokrasia wa kuheshimu mawazo na mitizamo tofauti na maslahi na matamanio yetu. Halafu tunaishia kutafuta uchawi ndani ya CCM wakati hata hao wapiga kelele za demokrasia nao bado wamegubikwa na fikra za kidikteta..

Tuna safari ndefu kaka.......
Mawazo ya ovyo ovyo hayawezi kuheshimiwa kwa sababu tu ya demokrasia




Omarilyas,

..hicho ni kipande cha statement aliyotoa Zitto Kabwe kuhusu tatizo la mgao wa umeme.

..kwa mtizamo wangu anaelekeza lawama kwa wanasiasa wenzake waliokataa mitambo ya Dowans, badala ya Management ya Tanesco na Uongozi wa Wizara kwa kushindwa kutupatia mitambo mipya.

..pia Zitto amepata wapi haya mawazo ya taifisha-taifisha? huyu inaelekea anaamini kutaifisha ni kuchukua bure . sasa ni vizuri aelewe kwamba hata mali tulizotaifisha mwaka 1967 tuliwafidia wamiliki wake. tena wengine walitupeleka mahakamani na tuliishia kuliingiza taifa hasara kubwa.

..pia umedai Zitto aliambatana na viongozi wa Chadema wakati akitoa mapendekezo kuhusu mgao wa umeme. naomba basi utuhakikishie kwamba statement ile ni ya Chadema na siyo yake binafsi. pia naomba utahakikishie kwamba Chadema sasa inaunga mkono sera ya utaifishaji mali.
Asante mkuu huwa humng'unyi maneno. Taabu hawa jamaa kumbukumbu zao ni mbofu

Haya mambo ya kijinga kijinga ndio huturudisha nyuma nchini. Umbeya umbeya na majungu majungu. Hoja hapa ni Mbunge anayeitwa Zitto na siyo Omar.

Pili, bila hata ruhusa ya Omar mwenyewe ninataka niseme wazi wazi kuwa Omar ana kazi. Kama mnadhani kazi ni kuajiriwa katika ofisi na kuamka asubuhi kwenda basi lazima kichwani hakuko sawa. Omar amejiajiri na anafanya kazi zake kama consultant. Ubalozini New York huenda kwa sababu ya utafiti wake kuhusu UN.

Tatu, Omar Ilyas ni Msaidizi Maalumu wa Dkt. Salim Ahmed Salim - The President of Tanzania who never became. The longest serving ex Secretary General of the OAU, The only African south of SAHARA who nearly became the secretary General of UN and lost it because of his ideological stand and that of his Boss Julius Nyerere, The only Tanzanian who Nyerere asked to contest (mtasema Mkapa, sio kweli Mkapa alipelekewa na Jenerali Ulimwengu na Patrick Qorro kama alternative ya Salim), The Ex- Premier and Minister of Defence and a Board member of Mo Ibrahim Foundation.

Salim ni chuo Kikuu of his own. Omar ni sawa na mfanyakazi wa library ya chuo kikuu kilichosheheni vitabu vinavyosema.

Unathubutu kusema hana kazi?
Halafu huyu ndio eti alitaka kuwa mwenyekiti wa chama. Na chini ndio mshauri wake.

Ulitaka ifike wapi na ifike kwa namna gani? Je ulitaka zitto afanyaje ili aifikishe huko unakokutaka? Je na wewe umefanya nini ili ufikishe huko? Je unadhani kwa ufinyu wa wabunge wa chama chake ama udhaifu wa kimikakati na sasa kiasasi uliopo huko angeliweza kufikisha hapo ullipotaka wewe?

Je tuliingiaje mkataba wa kuzalishiwa umeme kwa kutumia mitambo chakavu?
Hoja yako hapa ni ipi? Kwamba kwa sababu tuliingia mkataba basi mitambo siyo chakavu au?

Katumwa na mafisadi na anakuja kama nyati aliyejeruhiwa na nyati
Umefanya jumuisho zuri sana.
 
Sasa Cpt Hadock, nini hitimisho lako?

Kama sikufikia hitimisho wacha niseme hapa. Zito anaweza kuwa charismatic kama watu wanavyodai lakini mi nasema siyo. Ni opportunist tu. The guy is arrogant, egoistic and stubborn. Kwa akili ya kawaida huwezi kusema tununue halafu kesho unakuja na tutaifishe bila hata kukiri ulipotoka. Hafai kuwa kiongozi wazee wa CHADEMA waliona mbali ni kama Nyerere alivyomkata JK lakini watu wakaona mzee yule yule alikuwa amepitwa na wakati na sasa tunaona nji inayumba.
 
Quote:


Je tuliingiaje mkataba wa kuzalishiwa umeme kwa kutumia mitambo chakavu?

Hoja yako hapa ni ipi? Kwamba kwa sababu tuliingia mkataba basi mitambo siyo chakavu au?

Blistering Barnacles,

Hoja yangu ni kuhoji aliyesema kuwa TANESCo isinunue mitambo mikuukuu au michakavu. Mimi nikauliza, ilikuwaje tukaingia mkataba wa kuzalishiwa umeme kwa kutumia mitambo mikuukuu?

Je kama mfanp Richmond wangeweza kufanya kazi yao na hawakuwa kampuni ya mazabe, lakini wakatumia mitambo mibovu na chakavu, je pale ambapo wangeshindwa kuzalisha umeme inavyotakikana kutokana na ubovu huo tungemlaumu nani?

Or in other owrds, kwa nini Serikali huruhusu kukodisha mitumba mfano kama ule wa ATCL kukodisha Airbus lililochoka lakini tukaingia gharama karibu sawa na kununua ndege mpya?

That is my point Jellyfish!
 
Would Zitto raise and be as charismatic and motivating like Mwalimu Nyerere?

Zitto, tuko nyuma yako! (Usiogope kama Mzee Mwinyi alipoogopa aliposikia watu wakidai wako nyuma yake! kwi kwi kwi)

Mwinyi ni wa pwani zitto ni wa bara, hahisi wala haogopi mtu kuwa nyuma yake hahaha!
Ninayo machache dhidi ya Mhe. wangu Zitto. Kwanza nikubaliane na wewe Rev.Kishoka, Zitto ni charismatic leader to be. Zitto ana malengo, malengo lazima yapaliliwe kabla ya kufikiwa. Kupalilia kwa Mhe.Zitto, ni kujidhihirisha mbele ya wtz kwa yale anayoyatetea kwa maslahi ya umma. Unapopalilia malengo yako, kuna vikwazo njiani, kwanza, wasiopenda mtizamo wako watakuzulia mabaya ili kukuchafulia juhudi zako. Au kama hauko kwenye system yao kwa lugha rahisi kama si mwenzao basi watajiunga pamoja kwa lengo la kukumaliza. Haya yamefanyika dhidi ya zitto, kasimamishwa Bungeni, akina Matlida Burian mashangingi ya Chama yakishangilia tukio hilo. Lakini umma wa wtz, ulikuwa nyuma yake, wapiga kura wake wako pamoja naye. Tumpe support, tunamkosoe pale anapofanya ndivyo sivyo, tumsaidie kumnyooshea njia apite bila matatizo na kufika kwenye enzi (Urais) anazochugulia bila kukwama. Ni kiongozi, ni mzalendo, ana sifa, ana uchungu na nchi yake, tujiandae kumkabidhi rungu, rungu hilo liwapige Mafisadi wa RICHMOND, KAGODA, RADA, NDEGE YA RAISI, TICTS, IPTL na wenzi wengine wa mali ya umma. Lazima atufikishe pale tunapotaka kwenda, Maisha bora kwa wote
 
Back
Top Bottom