Defining, Refining and Understanding Zitto Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Defining, Refining and Understanding Zitto Kabwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Nov 1, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mh. Zitto Kabwe,

  Kwa heshima na taadhima naomba nikuzungumze pamoja na wasifu wako.

  Ni wasifu gani alionao Zitto Kabwe?

  Kijana, Msomi, Mwanaharakati, Mwanasiasa, Mwanataaluma, na kadhalika.

  Lakini tunapokaa na Zitto Kabwe ambaye bado ni kijana mbichi kisiasa na kiumri, tunampokea kwa namna gani na tunashabihiana naye kwa mantiki ipi?

  Je Zitto huyu ambaye yu nasi humu JF, tunamuelewa? Je anaeleweka kwetu na kwa jamii ya Watanzania?

  Kwangu mimi, Zitto ni kijana, msomi na mtaaluma kuliko mwanasiasa. Bado yupo katika nafasi ya kutambaa kama mtoto anavyotambaa!

  Je kauli zake zinaeleweka au kuaminika? Majibu ni ndiyo na hapana. Ndiyo kwa maana huongea bila kufikiria Kisiasa na Hapana kwa kuwa majibu na kauli zake huleta mgongano wa hisia au kiitikadi na hivyo kufanya wasifu na taswira ya Zitto isieleweke.

  Nimewahi kukutana na Zitto na tukapiga soga kwa saa moja, tukiongelea mambo mbali mbali. Zitto huyu hana tofauti na mimi nilivyokuwa miaka 7-10 iliyopita katika utashi wa mambo ya kisiasa.

  Tofauti yetu, Zitto ni Mtaaluma (academic, intellectual) mno wakati mimi ni mbangaizaji wa mtaani nikiangalia kilichopo na kukipima kisiasa. Wakati Zitto ni Centrist, mimi ni Radical, hivyo utaona tofauti zetu hata kama tunaweza simamia kitu kimoja na upande mmoja.

  Je inawezekana kushindwa kwetu kumuelewa Zitto kunatokana na uchanga wake na kushindwa kwake kujitambulisha kama Mtaaluma au Mwanasiasa?

  Yes Zitto can be Naive, sound Arrogant and very Self assured. It is a blessing and a curse in the environment of Watanzania today.

  Je ana msimamo imara na thabiti? majibu nayo yanakuja ni Ndiyo na Hapana, ikitegemea na upande ulioegemea wewe unayempim na kumsikiliza na utashi wako.

  Kwangu mimi, Zitto tunamt\wisha mzigo na msalaba mzito kabla ya wakati wake. Ana nafasi kubwa ya kujifunza kutoka kwetu na sisi kujifunza kutoka kwake.

  Zitto ana uwezo mkubwa akishaweza jitengeneza na kuwa na taswira moja ambayo tutaikubali na kumuelewa kuwa kiongozi mkubwa na mwenye mvuto mkubwa mno. Lakini taswira hii ni lazima iwe yake mwenyewe na si kwa matakwa yetu. Ni sisi ambao itnabidi tumkubali na taswira yake pindi itakapopevuka na sisi kuiva na kumkumbatia.

  Wengi wetu hapa JF na katika jumuiya za Watanzania tunaotaka mabadiliko, tunatafuta Radical na si Centrist katika mazingira tuliyonayo sasa hivi na ndio maana sishangai jinsi Zitto anavyobanwa humu ndani na kusulubiwa kila siku.

  Kadri anavyokua na kukomaa na sisi kushabihiana naye, ndivyo tunaweza kuungana na kuelewana.

  Lakini, bado kuna mambo ambayo Zitto itabidi ayaweke sawa kwanza machoni mwa Watanzania wote aeleweke si kwa wachache tuu bali kwa wote kwa kuwa tayari watu wameshaanza kumtarajia awe kiongozi makini.

  Mambo haya ni Uchaguzi Mkuu wa Chadema 2009, Kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Rais ya Bomani na kauli zake kuhusiana na Dowans na IPTL.

  Gharama za kuwa mwanasiasa ni kuwekwa kwenye kiti moto, usailiwe na wapiga kura.

  Je Zitto anaweza kujijenga na kueleweka ndani ya jamii ya Watanzania na hata kadiri anavyopevuka tunaweza kumkumbatia na kumwamini anaweza kutuongoza akiwa ni mtu mwenye siasa za mrengo wa kati?

  Mh. Zitto, napenda kuwasilisha salamu zangu,

  Nduguyo, Mchungaji!
   
 2. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #2
  Nov 1, 2009
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mchungaji,

  Hiyo kazi uliyompa Zitto ya kuyaweke sawa mambo kadhaa machoni mwa Watanzania wote ili aeleweke si kwa wachache tuu bali kwa wote ni mzigo mkubwa sana na sidhani kama atauweza.

  Sijawahi kusikia mtu/kiongozi yeyote akaeleweka na jamii yote. utakubaliana nami kuwa hata Yesu haeleweki na wakristu wote. I am not sure if Mohammed ameshaeleweka na waislamu wote.

  Kama unahitaji Zitto aweke sawa baadhi ya mambo kwa ajili ya career yake as a politician, afanye hivyo. but dont expect kwa kufanya hivyo ataeleweka kwa watanzania wote.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Maadam yupo Chadema, basi ana kasoro kadhaa, licha ya wewe kujitahidi kumpamba!
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishoka,

  Mimi namkubali sana Zitto kwa sababu ndiye kiongozi pekee anayeweza kukubali kusimama kujitetea hata kama kuna makosa kulingana na mtazamo wa wengine..

  Huyaweka mawazo yake wazi kabisa na yupo huru kuyatetea kama sisi tunavyoweza kujitetea ktk hoja mbali mbali. Tofauti kubwa ya Zitto na pengine wengi wanashindwa kumwelewa ni kwamba huyu Zitto yupo vitani, yupo mstari wa mbele katika mapambano ambayo kwa kila hali inaonyesha team yake kushindwa na dakika 45 za lala salama zinaondoka.

  Kibaya zaidi ni pale tunapopima hasira za washabiki wanaoutazama mpira huu na kuona team yetu inafungwa tunapochanganya na hasira za mchezaji ambaye yupo Uanjani akicheza mpira..

  Trust me, mkuu wangu kama umewahi cheza mpira utaelewa nazungumza kitu gani..Hofu na hasira za mchezaji zinakuwa na impact kubwa kuliko zile za mtazamaji na mara zote watazamaji humatza mchezaji wao kwa kila pass anayotoa ili kupata goal au ushindi lakini wasifikirie zaidi jinsi team nyingine inavyojiandaa poia kuongeza goal la pili.

  Hivyo Zitto kama mchezaji ana hasira zake, anaweza kutokubaliana na mchezo (formation) inayotumika, Refa, vibendera, na hata wachezaji wenzake wanapotoa pasi mbovu au kutokuwa ktk position zao..Matokeo yake kwa uchungu wa kufungwa anaweza hata kutaka kucheza rafu karibu na penalt box au kufunga goal kwa mkono...Yoote haya ni mawazo ya mchezaji hayawezi kubalika kwa mtazamaji unless mawazo hayo yamezaa goal la kusawazisha.. hapo ndipo ushujaa wa mchezaji huonekana hata kama kafunga kwa mkono lakini watazamaji tungependa sana Zitto afunge magoli kwa kisigino..

  Binafsi namwelewa sana na hakika kuwepo kwake hapa JF ni Blessing kwetu, sisi wote humu ni watazamaji tu hatuwezi hata kupiga danadana kumi kwa mguu mmoja lakini tunaelewa vizuri mchezo mzima wa siasa..

  Tukiweza kuelewa tofauti hizi baina yetu na Zitto sidhani kama tutakuwa mbali na Ukweli.. Mafisadi wanapotupiga bao na Zitto akawa mfungaji wa goli hilo wakati akijaribu kuokoa mpira wa kona isiwe ndio Usaliti wa Zitto kwa wananchi..

  Tuelewe kazi ngumu ya beki wetu, kwamba kazidiwa maarifa, na kuchaguliwa kwake Taifa Stars (kamati za bunge) kusiwe sababu ya kufikiria kwamba Zitto ni CCM kwa sababu tu jezi za taifa stars ni bendera ya CCM...
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  And I assume you CCMers are the perfectionists, no?
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Uwezi kuwa Chadema ukawa perfect! Utakuwa una matatizo tu, tena makubwa!
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kibunango,
  Mkuu wangu weee huna haja ya kusema mengi, hiyo signature yako inajieleza vya kutosha..
   
 8. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #8
  Nov 2, 2009
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mimi nafikiri ni vigumu watu wengi kumwelewa Zitto sababu yupo kwenye opposition. kila anachokifanya, hata kama kina maslahi makubwa kwa nchi watu hawataki ku-analyse na wanakichukulia kuwa ni siasa tu. lakini naamini kabisa haya haya anayoyafanya, angekuwa kwenye rulling party angeeleweka na angepata sifa nyingi tu kwa watu wengi.

  Kucheza rough ni part of the game hasa ukiona umezidiwa, na sometimes unaweza kucheza rough unintentionally.

  Although I am not into politics lakini ukweli namu-admire sana Zitto sababu analeta changamoto zenye akili kwenye siasa (ni mtazamo wangu tu, sio lazima ukubaliane nami), so keep it up Zitto! I believe kuna wengi wanaku-support
   
 9. D

  Donrich Senior Member

  #9
  Nov 2, 2009
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Zitto ni Mwanafalsafa ambaye ameingia kwenye siasa kwa ajili ya kutetea maslahi ya Watanzania,ndio maana siku zote amekuwa akitetea anachokiamini hata kama atapingwa na Watanzania wote,ninaamini kama ilivyokawaida ya wanafalsafa siku moja baada ya kumaliza kazi aliyotumwa na watanzania atarudi kwenye shughuli zake za kifalsafa.
   
 10. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Would Zitto raise and be as charismatic and motivating like Mwalimu Nyerere?

  Zitto, tuko nyuma yako! (Usiogope kama Mzee Mwinyi alipoogopa aliposikia watu wakidai wako nyuma yake! kwi kwi kwi)
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Maoni yangu ni kwamba on Zitto, mazingara ya siasa Tanzania hayaruhusu wanasiasa wa aina yake kushamiri, yuko mbele sana na wakati miaka 50 ijayo ndio anaweza kuwa kiongozi anayefaa kwa taifa letu lakini sio sasa, he is way too far ahead of the times.

  - Zitto, hana tofauti kubwa sana na Mkapa, (wanatofautiana kwenye ufisadi tu) lakini otherwise, nawaona wakifanana sana, maana Mkapa alipoingia kwenye power alikuwa na nia ya kufanya kweli sio siri, lakini mazingara ya siasa yetu kitaifa ndiyo yaliyomkatisha tamaa, mwisho akakubali kufuata ya viongozi wenziwe wengi yaani ya ufisadi, ingawa simtetei na ufisadi wake ni fisadi anyways!

  - Kwa kifupi, Zitto yuko mbele sana ya wakati na akijaribu tu ku-adjust ili a fit-in na mzingara ya siasa Tanzania, basi ndio mwisho wake politically sasa hivi anahitaji kufanya a very careful navigation, infact anaweza kujisaidia zaidi, iwapo atakaa pembeni na siasa kwa muda na kurudi siku za mbeleni, otherwsie he has the right attitude kiuongozi, tatizo ni time bado kufikia.

  Respect.


  FMEs!
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  FMES,
  Duh, mkuu wangu kumfananisha Zitto na Mkapa hapo kweli hukumtendea haki kwa sababu sisi wote ndio tulokuwa wajinga kufikiria kwamba Mkapa he meaned good!..Mkapa had his own plan ambayo wewe na mimi hatukuifahamu. Ufisadi sio tabia inayotokana na hali fulani ya maisha ni HULKA ya mtu.

  Mkapa hakuweza kufanya aliyoyafanya kwa sababu hakupewa nafasi wakati wa Nyerere na siku alipoipata tu ndipo true colors zake zilipoonekana, na ndio maana hadi leo hii haoni Ufisadi kuwa ni deal...Na kibaya zaidi mkuu wangu ni pale sisi tunapofikiria kwamba kuna kitu kilichomlaghai Mkapa hadi kufikia hatua ya kuwa Fisadi.

  Nitakwambia kitu fulani, mkuu wangu unajua waazi kwamba sisi tumepitia wakati mgumu sana, Tumepitia wakati wa Ujamaa tukiwa watu wazima meaning tunajitegemea kimaisha..vumbi la Ujamaa tunalifahamu na baada tu ya Ujamaa kufa, maswala ya Unga yaliingia kwa nguvu za ajabu.. You could have been a drug dealer tena la nguvu kwa sababu ulikuwa na Mtaji kisha ulikuwa na uwezo wa kifedha na kusafiri nje kirahisi..Lakini jiulize kwa nini hukufanya hivyo! Na sio tu wakati ule hadi leo hii umekuwa ni FMES yule yule ktk mazingira tofauti..

  Bila shaka utakubaliana nami kwamba huna HULKA ya Ufisadi kwani kuwepo na matatizo ama vishawishi sio sababu kabisa ya mtu kuhalalisha Haramu.

  Kwa mtazamo wangu Mkapa sii kiongozi wa kumwekea mfano ktk viongozi bora kwa sababu hakuna kipimo chochote cha uongozi bora ambacho Mkapa anaweza kupita...

  Nilikwisha sema hali nzuri ya kiuchumi ambayo anasifiwa Mkapa ilichangiwa zaidi na kuanguka kwa shilingi yetu toka Tsh 500 wakati wa Mwinyi hadi Tsh 1000 kwa dollar moja..Kinyume cha hapo huwezi kupata ongezeko lolote la uzalishaji nchini ktk sector yoyote ile..Mkuu wangu sina chuki na Mkapa ila mimi pia nilikuwa mmoja wa watu waliofikiria kwamba Mkapa alikuwa na nia nzuri..Kumbe hakuwa saint kabisa..
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Nov 2, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Nafurahi huwa anaita kijiko kijiko, hapo tu ndio namkubali, na yuko huru kusema kile anachokiamini. Si kuzunguka zunguka na kutafuta maneno ya faraja!
   
 14. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nukuu toka kwa Rev.


  Mch. nakubaliana nawe kwa kiasi kikubwa katika hilo.

  Hata hivyo niongezee kuwa kipimo tunachokitumia kumpimia Mh. Zito na wengine wote waliojitambulisha humu kwa majina yao halisi ni tofauti na kile tukitumiacho kwa wale tusiofahamika au niseme tunaodai kutofahamika. Rejea hapa ni kanuni ya mawasiliano yenye ufanisi isemayo, "The image of the Communicator to the Audience does influence greatly the acceptability or non acceptability of the Communicator's message'.

  Hivyo utaona kuwa mara kadhaa migongano ya hisia juu yake inaibuka pale anapokuwa mwepesi kutamka jambo humu ambalo wengine tukiliweka katika mizani ya Zito tunayemfahamu (kitaaluma, kisiasa, kimrengo, kiimani n.k ) tunaona kuwa au asingestahili kusema hayo ama asingestahili kusema hivyo au asingestahili kusema lolote hapo ama asingestahili kukaa kimya katika hilo n.k.

  Sote tunastahili kuwa makini tunapoamua kuandika kama vile ambavyo tunatakiwa pia kuwa makini tunapoamua kutokuandika chochote.

  Hasilani, siamini kuwa kila mwenye posts nyingi ndiye mchangiaji bora wala kwamba kila mwenye posts chache ndiye mchanga na au asiyekuwa na uwezo wa kuchambua au kuchangia mada hapa!

  Kaka Zito chukua hii changamoto na uifanyie kazi.

  Mimi huyooo nafia kwenye ka-signature kangu!!
   
 15. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2009
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Mimi simwelewi. Nategemea nitamwelewa siku moja.
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Bob, mimi ni Mkristo saafi, siku zote ninawahukumu wengine knowing kwamba na mimi ninatakiwa kuhukumiwa kwa standards zile zile na hasa na Muumba wangu, sasa huwa ninajaribu sana kuwa mkweli, ingawa sometimes I fall short kwa sababu siasa sio hard truth or facts kama science!

  - Mkapa alipoanza alianza vizuri sana, ninakumbuka siku alipomuita Msuya Ikulu na kumuambia one on one, kwamba hana nafasi katika serikali yake mpya na viongozi wengi wa zamani, infact jeuri yake ya kuwaacha viongozi wa zamani ilimuogopesha hata Mwalimu, ambaye in private alisema wazi kwamba huyu Ben anaonekana yuko serious, yes alionyesha kwamba yuko serious, sasa ni wajibu wangu kumhukumu kwa kukubali ukweli, na ukweli ni kwamba mwanzoni alionyesha kuwa serious, sasa katika kile kipindi alichokuwa serious alisema na kufanya mengi yanayolingana sana na Zitto, mazuri lakini hayakueleweka na wanachi.

  - Sasa katika hicho kipindi Mkapa alichokuwa serious, hakuna m-Tanzania aliyemuelewa exactly alikuwa anaongelea nini hasa majukwaani, infact mpaka leo kuna viongozi wengi wa juu hawaelewi alipokuwa akisema "utandawazi" alikuwa hasa anaongelea nini? That is my point, kuanzia alipokuja kugeuka hapo ndipo tofauti yake na Zitto inapoingia.

  - Naomba nirudie ninamuhukumu kiongozi wa taifa kwa kulinganisha mazuri na mabaya yake, mabaya ya Zitto ninayoyajua hayajali-cost taifa letu anything so far, infact mazuri yake yametusaidia sana taifa, lakini ushauri wangu kwake kwa sasa ni angepumzika siasa kwa muda na kurudi tena mbele ya safari ni ushauri wangu wa bure kwake.

  Respect.


  FMEs!
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  FMES,
  Hapo mkuu nakukubali Ukitaka kumjua Mkapa waulize kina mama kuhusu Ulaghai wa baadhi wanaume wanapotongoza wanavyojua kupanga maneno..Utafikiri wao ndio wanaume kuliko wanaume woote, subiri akisha pewa ufunuo!
  Zitto ni mkweli na mara nyingi mwanamme asemaye ukweli huonekana hana mpango..Ndivyo Tulivyo!
   
 18. Companero

  Companero Platinum Member

  #18
  Nov 2, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  ZK anajiita 'pragmatic' na kwa mujibu wa Kamusi yangu 'pragmatism' ni:

  1. (philosophy) the doctrine that practical consequences are the criteria of knowledge and meaning and value.

  2. The attribute of accepting the facts of life and favoring practicality and literal truth.
   
 19. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #19
  Nov 2, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Zitto - who is Zitto! Made to think by rev and all of you. Who are my friends? Ninaanzia hapo. Kila la kheri
   
 20. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Namkumbusha Zitto vitu viwili tu!

  1. Ajifunze "communication skills zaidi alivyo leo"; unaweza kumtukana mtu bila kutamka tusi, nyerere alikuwa anafanya hivyo. namna yako kaka ya kusema wengine wameshindwa sio nzuri. Ilaleta hasira zisizokuwa na maana kabisa.

  2. Ku-shine kwako kuna relation kiasi fulani na kwamba kuna vijana wachache sana Bungeni, hivyo usijione malaika it is only b'se ni kijana wa Team ya Taifa anacheza kwenye timu ya Veteran wa Simba na Yanga... so shinning is a must.... Ingawa una sifa kubwa sana ambayo waTanzania wengi hawana nayo ni "Kusoma"
   
Loading...