Kaka ulitaka nimjibu vipi.
Zitto amehangaika huko alikohangaika akapata mkataba. akarisk maisha yake akaulipua. Akapewa adhabu ambayo ikawarudi wale waliompa na kuwapa nafasi nzuri CHADEMA kufaidika kisiasa. Zitto kama angekuwa oppurtunist basi angeamua kung'ang'ania hiyo ni ajenda yake na asingeamaua kuwapa jukwaa alilolitengeneza kwa gharama kubwa wakubwa zake kina Mbowe, Silaa, Mrema, Hamad Rashid na wengine wengi hapa.
Wengine wakaamua kujilundikia ajenda zingine bila hata kushughulikia hiyo na kujua mwisho wake. Sasa hizo ajenda walizorukia tayari wameporwa. Cha ajabu badala ya kuwa creative kuja na ajenda zingine zenye maana zaidi kwa watanzania, wameng'ang'ania na ajenda hiyohiyo wakati wakijua wazi hawana umma wala uzito wa kimadaraka wa kuweza kufikisha hiyo ajenda to the conclusion.
Kama wao pamoja na hao washikaji zao kina Mwakyembe wameshindwa kushughulikia hayo wanayoyapigia kelele, iweje wategemee Zitto asimamishe ya Buzwagi. Tena wanadhani atawezaje kufanya hivyo wakati wao wenyewe wako bize kumpiga vita wakijidanganya kuwa eti watammaliza kisiasa kumbe wanasaidia wengine kuwamaliza wao kama chama. Yaani hawa wote wamebebwa mgongoni na Zitto huyohuyo kuingizwa CHADEMA sasa wanajidanganya kuwa eti wao ndio wenye chama. Huyo Mzee Mtei mwenyewe hathubutu kujiona hivyo itakuwa hawa.
Sasa yamewashinda wanaanza kutafuta mchawi kwa Zitto na wengine. wakiambiwa ukweli kuwa wanasumbuliwa na majungu na fitina za kina Kiranja aka Mpakakieleweke pamoja na ugoigoi wa kimikakati wanaishia kusema wanatukanwa.
Wanaona wao ndio wana haki ya kumtukana na kumzushia kila uozo na kugeuza maneno ya Zitto kila wakati wakitegemea Zitto hatakuwa tayari kuwajibu kwa maslahi ya chama chake.
Sasa mimi sina loyalty ama kwa chama chao au mwenyekiti wao. And they know it. Hapo zamani nilikuwa ninaamini kuwa wanaweza kuwa chachu ya mbadala makini kwa watanzania kuchagua. Lakini sasa ni wazi kuwa tusipokuwa makini sisi basi tutaletewa bora mbadala ambao utaishia mambo ya NARC Kenya ya IT'S OUR TURN TO EAT...
Kama nina haki ya kukosoa uvundo wa CCM vilevile nina haki ya kukosoa uozo wa CHADEMA kabla nao haujageuka uvundo.
Kaka najua na wewe pia ungetamani kuona mbadala makini out of CHADEMA. Samahani kwa kukukwaza lakini kamwe siwezi kuacha kuwakosoa hawa kwa manufaa ya watanzania.
Ili tuweze kufanikisha matunda ya siasa za demokrsia ya vyama vyingi tunahitaji mbadala makini kutoka katika chama chenye utashi wa kuleta mabadiliko ya kweli na sio bora mbadala usio na tija na pengine yakawa na athari zaidi kwa Tanzania yetu.
Hawa jamaa wanapaswa kukaa chini na kufanya self reflection ya matatizo yao badala ya kukimbilia kutafuta mchawi kwa Zitto ama Omarilyas. Wachawi wao wenyewe wakiongozwa na sumu mbaya za Kiranja aka Mpakakieleweke....
Kuhusu kumuongelea Zitto, as long as wanakuja hapa na kwengineko na uzandiki wao i will not stop deciphering their cheap and loosy spinnings.....Kama wao wanadhani wana haki ya kumpaka uozo wao wa Zitto basi nami nina haki ya kupambana na uozo wao.
Mkuu shukran sana kwa kulifunua kawa kwani nimeipata harufu ya hilo biriani lililokolea pilipili manga...eeeeh matumbo yananiunguruma duh!...Unajua siku zote nimekuwa nikijiuliza mengi kuhusiana na mwenendo wa viongozi wa washabiki wa Chadema pasipo kuelewa kinachoendelea na hakika LEO NIMEJUA UKWELI.
Mapambano yaliyotokea hapa JF baina ya Zitto na Mpakakieleweke na BI asha yalinipa picha ndogo sana lakini maadam wewe umakuja hapa na kunieleza kwa ufupi yatokanayo, nimekupata na mengine nitajazia mwenyewe...
Kitu kimoja kilichokuwa wazi kabisa ni kwamba malumbano haya, nyie nyote mnawasaidia CCM Ufisadi na sii kwamba wao au Zitto ndiye mchawi, wachawi ni nyote kwa sababu maswala yote muhimu yamekuwa mali zenu..Zitto na Buzwagi na Ufisadi ni signature ya Dr.Slaa pasipo kutambua kwamba huu sii mchezo wa sinema au kuigiza kumtafuta starring na vlilian!. Nyote mnachezea maslahi ya Taifa zima na hakika maelezo yako yameonyesha wazio jinsi watu wasivyokuwa na uchungu zaidi ya NAFSII zao..
Zitto aliaminiwa na wananchi na ndio maana alipata hizo nyaraka za Buzwagi na Dr.Slaa na hao kundi la Wapiganaji pia waliaminiwa na wananchi kuweza kuzikwaa hizo nyaraka za Ufisadi, hivyo kuwafanya nyote kuwa wawakilishi wa wanung'uniko yao, adha zao vilio vyao leo nyote mnasahau kazi mlokabidhiwa!..Hii sii vita ya Zitto vs Chadema au Mkapakieleweke, huu ni Ubarubaru wakuu zangu, watu wazima wenye upeo mkubwa kisiasa hawafanyi hivyo, dhamana mlokabidhiwa na wananchi inatangulia ugonvi wenu na dhamana hiyo ndio itawajenga kisiasa..
Haya Zitto kashindwa kuimaliza kazi ya Buzwagi leo hii wananchi wa Buzwagi wanafukuzwa kama mbuzi... siiZitto aloshindwa vita ila wananchi wote Tumeshindwa..hilo ndilo lipo machoni mwetu na sii vita baina yake na Chadema. Nao kina Dr. Slaa wameshindwa kumwajibisha Mkapa au kupambana na Ufisadi kiasi kwamba hata wale wa CCM waliodandia bus baada ya mkorogo ndani ya Chadema nao mnawapiga vita.. Kina Mwakyembe, Anna Kilango na wengineo wote leo hii ni wachawi vile vile... Ushindi kwa Mafisadi...Nchi imetekwa na raia wameingia utumwani for your own greed ya madaraka.
To me inaonyesha wazi mapungufu makubwa ya vijana wetu kisiasa hasa mnaposhindwa kufikia mahala mkaiweka ilani ya chama mbele ya maamuzi yenu binafsi, inaonyesha wazi kwamba hata ndani ya Chadema hakuna MIIKO na MAADILI ya viongozi wake.
Hadithi nzima inajieleza wazi kabisa kwamba siasa za Tanzania ni KILA MTU na LWAKE.. Chadema wameshindwa kuungana na CUF, TLP na NCCR kwa sababu hiyo ya Ubinafsi, Matokeo ya Wangwe, Kabourou na sasa Zitto ni dalili mbaya sana za uongozi na imani za watu ndani ya chama hicho..
Siwezi kumnlaumu Mbowe hata kidogo kwani yeye ni mwenyekiti tu ambaye hawezi kuchukua hatua ambazo zitakisambaratisha chama. Kujiunga kwa wote hawa iwe Zitto au wagonvi wake ni mchango mkubwa kwa chama kizima. Kuondoka kwa mtu mmoja ni pengo kubwa kwa wanachama na wananchi hasa pale msukumo wa matatizo yote haya yanatokana na UBINAFSI.
Ndugu zangu muda unayoyoma, CCM wanatafuta popcorn tu sasa hivi na Mafisadi ndio kwanza wanacheza dhumna, ishindi ni wao kwa sababu za kijinga sana.. yaani inachekesha sana kuona kwamba wananchi pamoja na juhudi zao zote watashindwa na nguvu ya UKOLONI mambo leo..Na kibaya zaidi hakuna kiongozi hata mmoja aliyejitoa mhanga kama kina Mandela au Steve Biko akaondoka na heshima za wananchi..Tunashindwa kwa sababu kila mmoja wenu ametupa silaha yake na kucheza kati kwa maslahi binafsi..
Hakika leo nimeondolewa nguvu yote ya Upiganaji, nimeondolewa tumaini kubwa nilokuwa nalo na viongozi walioppo na ndio maana siku zote nimeomba vyama vya up[inzani kuunga nyuma ya Salim au Dr. Slaa ili kuleta ushindani mkubwa kwa JK lakini ndoto hiyo imeondoka. Kilichopbakia nitarudi kwa JK na kuendelea KUOMBA na KUTUMAINI kwamba silku MOJA ataamka na kumrudia MUNGU wake.. Siku ambayo ataweza kuweka kipaumbele maslahi ya Taifa mbele ya MAFISADI kwani yeye ndiye mwenye nguvu kubwa ya kiutawala ili kuliokoa Taifa.
Amini maneno yangu sintamsikiliza mwanasiasa yeyote tena iwe Chadema, CUF,TLP au NCCR - Mageuzi kwani mchezo huu wadanganyeni WADANGANYIKA na sii mimi.. and for that I will stand behind WAPIGANAJI ambao kidogo ninayo HOPE hata kama ni ya muda mfupi while I still breath.
Maasalaam.