Kama upo Tanzania ama unaweza kwenda katika mitandao mingine zaidi ya jamiiforums basi nenda katika THE CITIZEN la jumapili upate jibu lako. Kama serikali ingekuwa na nia/uthubutu ya kununua mitambo ya DOWANS amabyo ukweli si CHAKAVU kama vijembe vya kisiasa visemavyo nina uhakika ingeweza kununuliwa hata kwa nusu ya thamani yake. Ukiangalia hali ya kisiasa na uwezekano na gharama pamoja na deni la mabilioni DOWANS wanayodaiwa na serikali ni wazi kukipataikana negotiators wenye mapenzi na uzalendo uliotukuka na nchi hii, mitambo hiyo inaweza kununuliwa hata kwa nusu ya thamani yake ambayo THE CITIZEN wanadai ni bilioni 60. Na hapo bado faida ya kuepuka ngarama za kuibadili kutumia gesi kwani tayari inaweza kutumika hivyo(kadiri nijuavyo mimi).
.Huku ndiko kunaitwa kujistukia. Ni lini Zitto amewahi kusema ama hata kuwataja hao kina Mwakyembe? Yaani waboronge kwa faida na nafasi zao kisiasa halafu waanze kutafuta mchawi wa makosa yao?
Yaani ninyi kama kitu hakijaandikwa magazeti basi ni lazima hakikufanyika? Uliwahi kuhudhuria vikao vya kamati yake na Tanesco ama Wizara ya nishati ama hata BOT na ukaona kuwa Zitto hajawahi kuhoji hayo maswali? Hivi pia unadhani matatizo tunayokumbana nayo sasa yataisha kwa kununua mitambo ya kuzalisha umeme halafu basi. Unajua mchakato wa ENERGY BILL ulivyokwenda na nini kinaendelea kuhusu NATIONAL ENERGY MASTER PLAN pamoja na masuala mengie ya KISERA? Je umejaribu kufuatilia nini mchango wa Zitto katika hayo yote?
Again, acha uzandiki na kujistukia....Lini alisema hayo? Yaani mtu kueleza hatari zinazokumba taifa na kutoa mawazo yake jinsi ya kulishughulikia suala hilo kama alivyofanya Zitto wewe ulichoweza kusikia ni maneno yasiyokuwepo.
Hivi kati ya Zitto na hao MASIHA FEKI wenu ni nani ameishia kuwa distraction? Yaani anayekuja na maoni ya jinsi ya kushughulikia tatizo na anayekuja na msemo wa tukae na giza ili mradi adui wao ndani ya chama chao asiweze kufurukuta kama wanavyodai wao, yaani nchi isimame hadi hapo watakapomalizana wao, ni nani anaplay politics of distraction?
Zitto has always been proactive on issues however controversial or risky they entail, kitu ambacho wengi wetu tumejengewa mentality ya kukiogopa ama kutokiamini......
Acha mitizamo ya kuna uwezekano, unashindwa kufanya utafiti wa kujua anayoyafanya, basi hata hili la kujua marafiki ama washauri wake unashindwa kulifanya? Do ur work ndugu, hapo ndipo tutakuwa na mamia ya kina Zitto ....
Sasa kama chama chake kimekosa uthubutu ama kimegubikwa na ugoigoi wa kimikakati ama wameamua kuchukua hoja nyepesinyepesi kama ufisadi tu ambayo tayari wameshanyang'anywa, bado tu unataka kumlazimisha asubiri misimamo yao.
Lakini pia una uhakika kuwa matamshi yake hayana mahusiano na chama chake ama mradi umesikia wenzake wachache wenye kuweka mbele tofauti zao binafsi na kuzifanya za kichama wanapodai kuwa huo sio msimamo wa chama basi ndio hivyo. Wakati alipoitisha mkutano wa waandishi wa habari hakuwa na watu wa chama chake? Hivi Tumbo sio mkurugenzi wao wa habari? ama mpaka akiwa na kina Mrema, Wilbord, Mbowe, Ndesamburo ndio utakuwa mtazamo wa CHAMA?