Makaayamawe
Zitto sio msomi ila ameelimika. Mtu akiwa na degree moja hawi msomi kwani huo ndio (mwanzo - undergraduate) wa kuelekea kwenye usomi (graduate school, postgraduate degree n.k.).
Aende shule (ulaya au marekani) na asome kwa bidii kuelewa yanayofundishwa na sio kwa ajili tu ya kufaulu. Sijui alivyosoma UDSM, lakini nina wasiwasi hakuwa makini sana.
Pia anapoishi huko (ulay au marekani), atajifunza mengi ambayo hayafundishwi darasani na ni muhimu katika kuirekebisha nchi yetu.
Sio vibaya pia akafanya kazi ya kuajiriwa, biashara au vyote. Humo atajifunza sana uongozi na ubora/ubaya wa maamuzi afanyayo.
USOMI- Je tuna maana ya SCHOLAR ama INTELLECTUAL?
Nimjuavyo Zitto ni mtu anayependa sana kujisomea na hivyo kuongeza ujuvi wa mambo. Hii ni tabia ambayo amekuwa nayo tangia miaka mingi pale Mlimani. Kama kuna zawadi anayojua kununua na kuhakikisha anasoma Zitto awapo nje safarini ni vitabu na majarida. Hata ukipitia vitabu vyake utagundua kuwa kilisomwa kwa umakini mkubwa. Ni kweli hivi karibuni nimeshuhudia muamko mpya wa kujisomea miongoni mwa vijana wa rika lake, lakini bado naamini yeye ni mmoja wanasiasa wachache sana wanaojisomea sana…..
KUFUNDISHWA na sio kwa ajili ya kufaulu- Hapa nametetea kwani hata wakati wa enzi za mlimani kama kuna mapungufu aliyokuwa nayo ni kutotilia maanani mitihani yake. Zitto ni mfano wa wanafunzi wachache wanaoenda mlimani kuelimika na sio kutengeneza digree za kupata ajira BOMBA. Kwa hili namtetea asilimia 100%. Angekuwa ni mwanafunzi wa kufaulu tu basi kamwe asingemuona Chachage mwalimu wa SOCIOLOGY kuwa ni mwalimu wake wakati yeye alikuwa akisoma uchumi, Asingemuona Prof Shivji wa LAW, Prof Haroub wa Development Studies amd Dr Lwaitama wa Philosophy kuwa walimu wake wakubwa.....Alilazimika kuwajua na kuwa karibu nao wote hawa na wengineo wang kutokana na kutambua kilichompelek pale UDSM nacho ni kuelemika kwa mapana na marefu.
Nijuavyo Zitto alianza kusafiri nje ya nchi hata kabla hajamaliza chuo kikuu tofauti na ambavyo ilivyo kwa wengi wa watoto wa wakulima na wafanyakazi wa enzi zile kama yeye. Na aienda huko na hadi sasa ni mtu wa kujichanganya kabisa na maisha ya huko na kujisomea sana siasa za huko. Zitto ni mfuatiliaji sana wa mambo yanayoendelea nje ya nchi na bara letu. Ofcourse mengi ni ya masuala ya kisiasa na kiuchumi. Mambo ya kina TI na Rihana hapo utamuacha sana…
WildCard
Buzwagi hakuna alichofanikisha pale. Mkataba umebaki uleule uloosainiwa London. Raisi alipounda ile tume ya Jaji Bomani na yeye akawemo. Wakawa wanalipwa Shs 350000/= kwa siku. Ripoti yao imefanyiwa kazi kiasi gani sijui.
Ni vizuri ukafuatilia kujua nini kinaendelea katika sekta ya madini nchini. Kama unadhani ilikuwa ni busara kung'ang'ania suala la Buzwagi tu na kuacha nafasi ya kushughulikia sekta ya madini yote kwa mapana yake basi ni wazi huwezi ukamuelewa Zitto.
Ni vizuri pia ukajaribu kuuliza mchango wa Zitto katika kamati hiyo. Na pia kujua katika muswada wa sheria ya madini unaozunguka hivi sasa ni mangapi yalitakiwa yafanyika na kamati yamechukuliwa na mangapi hayajachukuliwa na kwa nini? Kiongozi mzuri ni Yule anayetambua majukumu, nguvu na mipaka yake. Kumbuka wao walitakiwa kuchambua sekta na kupeleka maoni yao kwa RAIS. Sasa kama ungependa na wao wajigeuze wabunge wetu ambao wanashindwa kutofautisha nguvu na majukumu yao katika suala la kushauri ama kushurutisha serikali, then hapo utakuwa unawaonea…..
WildCard
Umimi. Anajiimarisha yeye zaidi kuliko chama chake. Hili halitamfikisha popote zaidi ya kupata UMAARUFU. Awaulize akina Mrema waliotumia staili hii walikofikia.
Bongolander
Lakini alivyoiyumbisha Chadema ameonesha kuwa he is somekind of an opportunist and somekind of self centred politician.
Mtu kama huyu akipewa kiti kikubwa anaweza kuburuzwa na kuyumbishwa, au anaweza kufanya mengi ya ajabu ambayo ni unpredictable.
Mimi naomba ufafanuzi wa hii issue ya Zitto kuyumbisha CHADEMA. Hivi ni Zitto ndiye ameyumbisha CHADEMA ama CHADEMA kama asasi ndio kimeyumba kwa kukosa ukomavu? Hivi kati ya Zitto aliyetumia haki yake na utashi wake kisiasa na kichama kuomba ridhaa ya kuwa kiongozi wao na wale waliotumia ………….kumzuia asitumie haki hiyo ni nani aliyumbisha chama. Kwa wale wanaofuatilia mchezo wa Second Chance (ni wa kijinga lakini hata ujinga una mengi ya kuelimisha) wataweza kujua jinsi ya mwanamama REBECA na Yule mwenziwe aliyekuwa Head Butler jinsi walivyokuwa wakilaumu maswahiba yote yanayowakuta ambayo ukweli ni kuwa yalitokana na ujinga, chuki na tamaa zao wenyewe halafu wakiamini kuwa hayo yote yanatokana na kina Salvador na wengineo hapo. Nadhani hii issue ya kumlaumu Zitto kwa kuyumba kwa CHADEMA inaendana na ule mchezo. Tukubali kujikosoa ili tujisahihishe.
Na opportunist ni yupi? Yule aliyetayari hata kutumia siasa chafu za kuvunja chama kwa ajili ya kulinda nafasi yake ama Yule aliyetayari kulaumiwa na kutoeleweka na wafuasi (political base yake) kwa kujitoa katika kinyang'anyiro ili kulinda maslahi/umoja wa chama hata kama wengi hawakuwa tayari kuliona hilo?
Kuhusu
umimi kwa kweli hapa mnamuonea kabisa Zitto. Wenye umimi si mnawaona wamefikia hata hatua ya kuhalalisha uozo wa posho mbili/takrima/itifaki ili mradi walinde nafasi na maslahi yao kisiasa. Kwa yeyote anayemjua vizuri Zitto ni wazi atakubaliana na mimi kuwa ubinafsi sio sehemu yake. Zitto nimjuaye mimi ni yule ambaye huona faraja sana kujitoa kwa kusadia wengine kuliko kitu kingine chochote. Ofcourse kwa utanzania wa aina ya usasa, ni vigumu wengi kuamini kama kuna mtu ambaye anapenda kujitolea kusadia wenziwe kwa kile kidogo alichonacho na sio "kujijenga" yeye binafsi...
Na kuhusu CHADEMA, hivi mna uhakika kuwa Zitto hajitolei huko ama mnabeba porojo za kina Mengi na wenzake magazetini? Hivi mnawauliza hao kina…….kutoka CHADEMA kuwa nini mchango wao uliozidi ule wa Zitto mpaka wawe na audacity ya kusema kuwa Zitto ana umimi? Kama umaarufu hivi Zitto alijipa huo umaarufu? Mnataka awamegee kidogo huo umaarufu wake? Fanyeni naye kazi nanyi mtambulike sio kila siku kuwa mstari wa mbele kuhalalisha majungu na uchafu wa hao kina Mwakyembe na wenzake ambao wangependa kuona kuwa kila mwanasiasa nchini atatumia ABCDs zao kisiasa.
Kama CHADEMA wameshindwa kufaidika na umaarufu wa Zitto, kama waonavyo wao, then hilo ni tatizo la Zitto ama la CHAMA? Ni mangapi Zitto ameyaibua huko anapoyaibua ambao wengi wenu hamna hata guts za kufika, na akaishia kuyahakiki na kuwapa viongozi wenzake CHADEMA wayafanyie kazi bila ya yeye kutaka kuwarecognised? Mengineyo mnayakimbia na kuyageuza geuza kwa manufaa binafsi nay a muda mfupi mkiacha kuyatumia ipasavyo. Sasa bado mdai kuwa ana umimi?
Mtanisamehe nimeamua kuyasema haya kwani nimjuavyo Zitto anaweza akaacha huu uzandiki na muono potofu juu yake uendelezwa bila ya yeye kujitetea kwa kutokana na hulka yake ya kutopenda kuonekana anajikweza........