tajiri tumbo kubwa
JF-Expert Member
- May 27, 2021
- 429
- 567
uko na upungufu mkubwa sana wa kufikiri na kutafakari mamboMnashangaa kitu gani?
Kwani kusoma chuo kikuu mpaka usome Form Six?
Prof Mwandosya Mark J, hakusoma Form Six, Bali alisoma DIT Halafu akaenda udsm baadae Aston university
Wahindi kule Posta watoto wao wanasoma ulaya vyuo vikuu vya dollar 50,000 kwa mwaka walisoma form Six?
Wahindi wangapi wanafanya kazi Agha khan na Muhimbili tena mabingwa lakini mbona hawakusoma Form Six
Kenya wanaishia Form Four na kwenda chuo kikuu
Mimi niliwahi fanya kazi nikiwa mwaka wa pili chuo Kikuu na Nilimpata ajira rasmi bila hata matokeo ya mwaka wa pili,
Watu wanaangalia uwezo wa Mtu sio cheti
Kuna vyuo unafanyishwa mitihani kabla ya kuingia ukiweza hata ukiwa darasa la saba Unaanza masomo
Elimu hii ya Form Six ni kuwapotezea watoto muda na maisha ya kutafuta Pesa tu
Miaka miwili Form Five na Six, Mtoto anaweza kujifunza utaalamu wa programming na akawa nguli
Miaka miwili inatosha mtoto kusoma Software mbalimbali na kuwa nguli
Form six ni mfumo wa Uganda na Tanzania wa kishamba sana
Ukiwa na pesa na upo vizuri mtoto unamsomesha kuanzia chekechea ulaya unalipa dollar 60,000 kama Milioni 120 Kwa mwaka
Ukiwa na pesa huna haja ya kusoma elimu yetu hii ya kitanzania ya kupotezeana muda,
Mtoto akimaliza Form Four unamtafutia College Marekani au Uingereza anajifunza mambo ya maana hata mwaka baadae unamlipia chuo kikuu huko huko
Angalia wahindi kule Posta na ni matajiri jinsi watoto wao wanavyokuwa smart kichwani baada ya Form Four, Mtoto anapelekwa college ulaya bei dollar za kutosha
Wabongo tatizo pesa, Watanzania wachache wana uwezo wa kumlipia mtoto ada Milioni 200 kwa mwaka au Milioni 100 kwa mwaka
Watanzania Tuendelee na Bodi yetu ya mikopo huku tukilia lia Retention fee
Ahaaaa