Mbunge Wanu Ameir awaahidi wanafunzi wa skuli ya Hasnuu Makame watakaofaulu shahada ya kwanza kupata Scholarship

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

MBUNGE WANU AMEIR Awaahidi Wanafunzi wa Skuli ya Hasnuu Makame Watakaofaulu Shahada ya Kwanza Kupata Scholarship

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kusini Unguja na Mwenyekiti wa Mwanamke Initiative Foundation (MIF), Mhe. Wanu Hafidh Ameir tarehe 09 Machi, 2024 amefika Shule ya Hasnuu Makame inayopata msaada kutoka Mwanamke Initiative Foundation na kugawa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kidato cha Nne.

Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) chini ya Mwenyekiti, Wanu Hafidh iliandaa sherehe za kuwapongeza wanafunzi waliofaulu kidato cha Nne wa Skuli ya Hasnuu Makame ambao walipata matokeo mazuri ya kuanzia Division one na Division two ambayo ilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari Bibi. Asya na Mwenyekiti wa MIF, Mhe. Wanu Hafidh Ameir na viongozi wengine wa Mkoa na Wilaya.

Mhe. Wanu Hafidh Ameir aliwazawadia Wafaulu bora wa mwanzo 1,500,000 Laptop na Vifaa vya Shule. Wafaulu wengine walizawadiwa 500,000 na vifaa vya shule (mabegi ya shule, madaftari, Rula na Peni). Walimu wa kidato cha Nne walizawadiwa 500,000 kwa kila mwalimu.

"Mwaka 2021/2022 kabla ya MIF kuanzishwa, wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha tano ni asilimia 9 tu na waliopata Sifuri ilikuwa ni asilimia 31. Mwaka 2022-2023 baada ya MIF kuanza kazi zake wanafunzi waliofaulu kidato cha tano ni asilimia 19. Mwaka 2023-2024 waliofaulu kidato cha tano ni asilimia 21.6 na waliopata Sifuri ni asilimia 8.4 kwa Mkoa mzima wa Kusini Unguja" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir, Mbunge wa Viti Maalum na Mwenyekiti MIF

"Skuli ya Hasnuu Makame, baada ya kuanza kupata msaada kutoka Mwanamke Initiative Foundation (MIF), mwaka 2022-2023 waliofaulu kidato cha tano ni asilimia 98 na Mwaka 2023-2024 watakaoenda kidato cha tano ni asilimia 100. MIF inasema historia imeandikwa" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kusini Unguja na Mwenyekiti MIF

"Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) itawapa Shule ya Sekondari Hasnuu Makame magodoro 52 ambayo yatatumika katika Skuli. Natoa wito kwa wanafunzi wanaoanza kidato cha Tano wajitahidi katika masomo yao ili waweze kufaulu katika mitihani ya kidato cha sita na waweze kuanza shahada ya kwanza" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kusini Unguja na Mwenyekiti MIF

"Nawaahidi, tutafanya jitihada kwa kadri ya uwezo wetu kama MIF kuhakikisha wanafunzi watakaomaliza kidato cha sita wanapata Scholarship. Wanafunzi mliofaulu ni kazi kwenu kupambana kidato cha tano na kidato cha sita, ukipasua Scholarship ipo" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kusini Unguja na Mwenyekiti wa MIF

Mgeni Rasmi katika sherehe hizo, Bibi Asya aliishukuru Taasisi ya MIF kwa jitihada zake katika kutokomeza Sifuri katika Mkoa wa Kusini na kuelezea hali ilivyokuwa mwanzoni kabla ya kuanzishwa kwa taasisi hii na hali ya matokeo ilivyo sasa. Hafla hiyo iliambatana na chakula cha mchana.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-03-10 at 23.18.12.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-10 at 23.18.12.jpeg
    94.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-10 at 23.18.12(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-10 at 23.18.12(2).jpeg
    115.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-10 at 23.18.13.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-10 at 23.18.13.jpeg
    122.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-10 at 23.18.13(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-10 at 23.18.13(2).jpeg
    95.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-03-10 at 23.18.14(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-10 at 23.18.14(1).jpeg
    130.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-03-10 at 23.18.14(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-10 at 23.18.14(2).jpeg
    82.4 KB · Views: 3
Mnaingiza siasa kwenye elimu sio? kutoka ufaulu wa 10% mpaka kufika ufaulu wa 100% ndani ya huo muda wa miaka miwili matokeo ya hicho mnachokifanya mtayashuhudia huko mbeleni..
 
Back
Top Bottom