DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Mkiwa active mtapata mengi sana. Ila msije mkaja na mambo ya wenzenu TANESCO ya kupewa changamoto walizonazo, wao badala ya kuhangaika na changamoto hizo, wanaanza mambo ya kutaka mtu aandike namba yake ya simu, anakoishi na jina lake kamili..!!!
Tuko active na tunamaanisha na katika hili hatuna masharti kama wengine
 
Kuwepo na utaratatibu wa abiria kupangana ndni ya gari watu wanajazana mlangoni kiasi kwamba ni hatari, vibao vile vya location viboreshwe kama ni express iwe na alama ya kuonekana hata red n k

Wekeni fence kuzunguka kituo kama ilivyo kituo cha ubungo maji wote wapitie zebra
Magari yanayobeba samaki yawe special aisee magari ya kivukoni asubuh yananuka shombo
Wekeni utaratibu wa kupeana mizigo mfano mtu anampa mzigo kwa anaesafari na asiesafiri,(kama fees iwepo ndogo )
Walinzi wenu walipeni vizuri wanalalamika sana and low motivation,

All in all mradi ni mzuri ukifanyiwa kutatutwa changamoto zilizopo
Tunashukuru kwa ushauri wako wa thamani tunaahidi kuufanyia kazi
 
DART Mwendokasi Madereva wenu mlioanzanao mradi walikuwa vizuri kiasi fulani na kwa nini mmewaondoa karibia wote?

Na kwa nini hamtumii muda uliopendekezwa na wale wajenzi wa mradi (Strabug) kwamba kila baada ya dakika 5 gari litoke terminal na ata vituo vya kati kati pia linakuwa linapita bila kuchelewa kama inavykuwa kwa sasa?

Mfumo wa kadi kwa nini tokea watoke maxcom mpaka leo hamjaweza kuzitumia hizo mashine na zimenunuliwa kwa gharama kubwa sana je mmeona ni sahihi mpaka sasa ziwe kama maonesho tuu kwa abiria?

Nitarudi baadae yapo mengi sana yakuyasema humu.
 
Kingine anzisheni mwendokasi VIP anayeweza kulipa hata afu tatu, kuwe na AC Kwa wanaoenda maofisi maana ule mubanano ni kero nawahurumia raia wanaokaa kimara ndio maana watu wanaendelea kutumia private car
 
Duuh ubaguzi huu sasa

Af yaani efu tatu approximately ef 10 per day nauli tu si heri anunue tu gari 😂😂😂😂
 
Dart, kuna muhubiri yuko pale stendi ya mbezi luis, kila siku asubuhi kwenye kituo cha kupandia basi cha Dart mbezi luis,

Na anasimama katikati ya mistari ya abiria wanaotaka kupanda basi za kivukoni na gerezani, ni kila siku kila siku anahubiri pale asubuhi na kuomba sadaka kwa kutisha watu kuwa wasiotoa ni wabaya na wanahitaji kuokolewa

Ni analeta vurugu na kelele tu pale, hata Biblia inasema kila jambo na wakati wake. Asubuhi, yote yeye yuko pale anaomba sadaka badala ya kwenda kujenga nchi.

Sitaki kushauri aondolewe maana mambo ya imani ni rahisi kueleweka vibaya, ombi langu ni Dart waambieni watumishi wenu yule muhubiri wamuelekeze asimame pembeni sio kwenye mistari ya abiria wa kivukoni na Kariakoo.

Maana sidhani kama kitendo kama hicho kinawezekana kufanyika kwenye terminal nyenginezo Dart.
 
Duuh ubaguzi huu sasa

Af yaani efu tatu approximately ef 10 per day nauli tu si heri anunue tu gari
Unafikiria waliweka huo ki vip watu wanakuwa wanaacha magari Yao binafsi na kupunguza foleni ndio lilikuwa lengo, anaye weza ku afford anapanda. Abiria wakimara wanateseka sana loh
 
Utaratibu wa matumizi ya kadi ilisitishwa kutokana na changamoto mbalimbali za kiufundi, kwa sasa mpango wa kurudisha kadi unakaribia kukamilika na mtajulishwa matumizi yake yataanza lini na namna ya kupata kadi hizo.

1.Kadi yangu inapesa zaidi ya 50k, kutokana na kusitishwa kwa matumizi ya kadi hii pesa inamaana imepotea, ama nafanyaje ili niaipate hii fedha? Na je mlitoa taarifa rasmi kwa umma juu ya kusitishwa kwa matumizi ya kadi na suluhisho la wale ambao walishaweka hela nyingi kwenye hizo kadi?

2. Hivi zile camera matumizi yake ni nini? Wakati mradi unaanza madereva walikuwa wakiangalia kinachoendela ndani ya gari hasa kwenye usalama na kama yupo kibaka kamwibia mtu basi dereva anatoa taarifa!
Lakini kwa sasa matukio ya watu kuibiwa ndani ya mwendokasi ni mengi, na hakuna msaada wowote licha ya kuwepo kwa camera!

3. Wakati mradi unaanza vituo vilikuwa vikitangazwa ama ndani ya gani screen inaonyesha kituo kinachofuata, lakini kwa sasa matangazo ya vituo hayasikiki wala baadhi ya magari hayaonyeshi chochote kwenye screen!
Hii inasababisha watu kuvuka vituo na wengine kupotea na kuwasabishia usumbufu!
Hii hali ni kwa nini haitatuliwi???

4. Ni kwa nini huu mradi hauruhusu watu binafsi kuingiza magari yao sokoni ili kuongeza ushindani?
Inavyoonekana watu ni wengi, magari ni machache! Wapo watu binafsi wanaoweza kuagiza magari ya aina hiyo na kutoa huduma, kwa nini hawapati hiyo nafasi...!?

5. Kuna baadhi ya vitua magari hayasimami na wala abiria hawakai katika vituo hivyo, mfano Jangwani na Kkoo maeneo ya msimbazi kuna vituo viwili kimoja hakitumiki mara kwa mara!
Hivi vituo inamaana haikuonekana ni hasara baada ya kuvitengeneza...? Hivi vituo vya aina hii vipo kwa maslahi gani?

6.Zipo taasisi zilifungua akaunti huku mara ya kwanza zikaja kwa mbwembwe kwamba zitajibu kila hoja lakini mwisho wa siku zikatelekeza akaunti!
Watu wanatoa madukuduku yao kwenye nyuzi zilizoanzishwa na hizo taasisi lakini hamna majibu, ama hoja zinajibiwa baada ya mwezi na sio zote! Je DART Mwendokasi
si mtafuata nyao kwa kuukimbia huu uzi, maana watu wameshaanza kufunguka yao hapa ila hujibu kila mmoja, unajibu baadhi tena majibu mepesi amabyo kimsingi hata hayaridhishi!
 
Tumieni radio call systems ni mfumo wa wazi,reachable na accessible na efficient. Maana organization ni finyu kwa sababu communication ni shida.

Yule kijana wa kule kivukoni anaechana tkt za mbezi hana adabu. Anahisi kama anaperform stejini halafu abiria ndio mashabiki wake.
 
Kingine anzisheni mwendokasi VIP anayeweza kulipa hata afu tatu, kuwe na AC Kwa wanaoenda maofisi maana ule mubanano ni kero nawahurumia raia wanaokaa kimara ndio maana watu wanaendelea kutumia private car
Katika mipango yetu ya baadae suala la VIP litazingatiwa , hii ipo kwenye mipango ya mabasi mapya yatakayokuja
 
Hayo mabasi wakopeshwe wenye daladala wa sasa. Kika mmoja aawe na lake au yake.

Kiwepo chombo cha kusimamia ubora wa mabasi, usalama, vituo na huduma.

Mfuno uwe first in first out kwa rwtiba unayopangiwa awali.

Nje ya hapo ni wizi mtupu.
 
Tumieni radio call systems ni mfumo wa wazi,reachable na accessible na efficient. Maana organization ni finyu kwa sababu communication ni shida.

Yule kijana wa kule kivukoni anaechana tkt za mbezi hana adabu. Anahisi kama anaperform stejini halafu abiria ndio mashabiki wake.
Tuvute subra tu wakati tunakamilisha kuleta kadi mpya suala la tiketi za karatasi litakuwa historia, hata hivyo kwa sasa unaweza pia kupakua Mwendokasi app kwenye playstore na android ili uweze kununua tiketi yako ya safari kwa kutumia mtandao. Kuhusu mawasiliano mfumo mpya wa Inteligency Transport System na wenyewe uko kwenye hatua za kupatikana huu utakuwa mwarobaini wa matatizo yote ya mawasiliano na uongozaji wa mabasi kwa ujumla.
 
DART Mwendokasi Hamuwezi kuwa na utaratibu wa gari kuwepo kituoni kila baada ya say robo saa? Wakati mwingine watu wanasubiri gari haziji na zikija zimejaa. Hamuwezi ondoa hiyo kero kwa kuhakikisha kila baada ya dk fulani gari inapita kituoni?
Kwa mujibu wa design tunatakiwa tuwe na basi kila baada ya dakika tano ,kwa sasa kwakua tuna upungufu wa mabasi ndiomaana hali haiko kama inavyotakiwa kuwa , lakini juhudi zinafanyika usiku na mchana na serikali yenu sikivu ya awamu ya tano kuhakikisha mabasi ya kutosha yanapatikana kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili kule Mbagala ambayo iko katika hatua za mwisho za umalishaji.
 
Tuvute subra tu wakati tunakamilisha kuleta kadi mpya suala la tiketi za karatasi litakuwa historia, hata hivyo kwa sasa unaweza pia kupakua Mwendokasi app kwenye playstore na android ili uweze kununua tiketi yako ya safari kwa kutumia mtandao. Kuhusu mawasiliano mfumo mpya wa Inteligency Transport System na wenyewe uko kwenye hatua za kupatikana huu utakuwa mwarobaini wa matatizo yote ya mawasiliano na uongozaji wa mabasi kwa ujumla.
@
DART Mwendokasi Madereva wenu mlioanzanao mradi walikuwa vizuri kiasi fulani na kwa nini mmewaondoa karibia wote?

Na kwa nini hamtumii muda uliopendekezwa na wale wajenzi wa mradi (Strabug) kwamba kila baada ya dakika 5 gari litoke terminal na ata vituo vya kati kati pia linakuwa linapita bila kuchelewa kama inavykuwa kwa sasa?

Mfumo wa kadi kwa nini tokea watoke maxcom mpaka leo hamjaweza kuzitumia hizo mashine na zimenunuliwa kwa gharama kubwa sana je mmeona ni sahihi mpaka sasa ziwe kama maonesho tuu kwa abiria?
 
Hayo mabasi wakopeshwe wenye daladala wa sasa. Kika mmoja aawe na lake au yake.

Kiwepo chombo cha kusimamia ubora wa mabasi, usalama, vituo na huduma.

Mfuno uwe first in first out kwa rwtiba unayopangiwa awali.

Nje ya hapo ni wizi mtupu.
Itaondoa dhana ya mass tránsit, itakuwa daladala sasa
 
Back
Top Bottom