DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Binafsi naona hata mfumo wa ukataji ticket umekaa kiupigaji sana, Kuna baadhi ya vituo ticket zinatumika zaidi ya mara 2 au 3 kwa abiria mmoja.

Nashauri uwekwe mfumo wa kutumia N-CARD yaani pesa iwe inakatwa direct kutoka kwenye card kwa kadri ya destination ya abiria, kama inavyofanywa pale kivukoni.

Pia magari yenu mengi ni mabovu, yaani idadi ya gari zilizo barabarani ni chache kuliko zilizobaki yard, fanyeni maboresho ya magari
 
Mradii wa mwendokasiii nao UMEKUFAAAAA...!! Yani hii nchi sijui tutaweza nini zaidi ya wiziiii
 
Bila support yangu kama mshauri hamtoboi.
Hawa walisema wameingia Mkataba na Emmirates Group Limited tangu 2021 mzew Baba alivyoacha jamaa walete Mabasi yao sasa imekuwa kila siku danadana na mara kila simu mikataba mipya na hii ji mara ya tatu yokea wanasaini mikataba na hao jamaa. Sijui ndio wanasubilia uchaguzi waje waseme tumeamua kuwaleta watu ili kura zipatikane.

Mwambieni Mama huu muda wote watu wanaumia na wanamachungu na hata uchaguzi ukifika kwa ufahamu wa wananchi bado watu watakuwa na kinyongo kutia saini katika kile kidubwasha
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, (X)TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Fikisheno mabasi

Dar hadi chalinze
Dar hadi Bagamoyo hadi msata
Dar hadi kisarawe.

It's possible play your part these places is connected already
 
Hawa walisema wameingia Mkataba na Emmirates Group Limited tangu 2021 mzew Baba alivyoacha jamaa walete Mabasi yao sasa imekuwa kila siku danadana na mara kila simu mikataba mipya na hii ji mara ya tatu yokea wanasaini mikataba na hao jamaa. Sijui ndio wanasubilia uchaguzi waje waseme tumeamua kuwaleta watu ili kura zipatikane.

Mwambieni Mama huu muda wote watu wanaumia na wanamachungu na hata uchaguzi ukifika kwa ufahamu wa wananchi bado watu watakuwa na kinyongo kutia saini katika kile kidubwasha
Lini wameanza kuogopa wapiga kura, wakati mwenyekiti wa tume anawatangaza TU washindi hata kama hawajachaguliwa!?
 
Kazi iendelee, Leo tarehe 22/4/2024 shehena kubwa ya Mageti Janja (smart gates) kwa ajili ya kufunga vituoni ili kufungamanisha na mfumo wa matumizi ya kadi janja (smart cards), inaendelea kushushwa pale Gerezani, watumiaji wa Mabasi Yaendayo Haraka muendelee kuwa na imani na Serikali yenu, changamoto zote za Mradi wenu zinaendelea kutatuliwa kwa awamu, kuhusu kuongeza Mabasi kaeni mkao wa kula kuna jambo tutawaarifu muda sio mrefu.
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, (X)TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Mama amefanya mambo makubwa hakuna rais aliyefanya toka tupate uhuru lakini Magari hamjaweka mabango ya rais.
Wekeni mambango ya kuonehsa kazi njema za mama.
 
Wekeni hayo mabasi yenu AIC maana madirisha Huwa madogo na watu wanakuwa wengi sana jambo ambalo ni hatari.
Hafu kingine kwanini mabasi yenu mengine hupita vituoni matupu bila kusimama au kuchukua abiria hamuoni mnafanya biashara kichaa
Asee ata mimi uwa nawashangaa sana na uwa nabaki najiuliza huyu mtu anatoka kimara mpaka Posta bus tupu halina abria anatumia mafuta au maji,hayo mafuta hesabu yao uwa ikoje?
 
Mradi umemshindeni bora mfanye kazi na wapiga debe na mateja....mnatia aibu wakulungwa
 
Kazi iendelee, Leo tarehe 22/4/2024 shehena kubwa ya Mageti Janja (smart gates) kwa ajili ya kufunga vituoni ili kufungamanisha na mfumo wa matumizi ya kadi janja (smart cards), inaendelea kushushwa pale Gerezani, watumiaji wa Mabasi Yaendayo Haraka muendelee kuwa na imani na Serikali yenu, changamoto zote za Mradi wenu zinaendelea kutatuliwa kwa awamu, kuhusu kuongeza Mabasi kaeni mkao wa kula kuna jambo tutawaarifu muda sio mrefu.
Bila picha ni uongo
 
Hizo card hakikisheni ni N card sawa na za Taifa, na Kivukoni. Msije kuja na kadi zenu binafsi. Mzigo. Imagine na Magufuli stendi wakaja na kazi zao.
 
Back
Top Bottom