DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Mwendokasi

Official Account
May 17, 2023
73
100
dart 1 (1)_1.jpg

DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, (X)TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
 
Asante kwa kuja.
Ni lini hayo mabasi mtayapeleka Mwanza pia ili wananchi wapate huduma ya usafiri..??
Sababu jiji la Mwanza limekua na tayari limechangamka na mkituletea hizo Bus zikaanzia route ya Kisesa, Igoma, Neshno, Buzuruga, Mabatini, Nata, Pepsi, Mkuyuni, Nyegezi, Buhongwa, Nyashishi hadi Usagara and Return.
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani

S.L.P 724, 16103

Ubungo Maji, Morogoro Road

Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Bila support yangu kama mshauri hamtoboi.
 
Wale walinzi mlio waweka vituoni kwenu ni bure kabisa sijui kwann mliacha kuwatumia jkt anway nyakati za asbh pale kimara mnapanga foleni kupanda mabasi kwa kua magari nimachache watu wanajaa vituoni walinzi wenu wanashindwa kudhibiti foleni inapelekea fujo hali hii ipo nyakati za jioni pia
hivi vituo vya barabarani(m/mapipa) abiria hawalipi nauli wanapitia kweny milango ya kushushia abiria na kupanda magari walinzi wenu wamekaa tu wana ongea habari za kina kajala

Sent from my SM-G950U using JamiiForums mobile app
 
Naomba muweke tangazo hairuhusiwi Kula au kunywa ndani ya vituo vya mabasi ya mwendokasi na ndani ya mabasi na walinzi wenu wasiruhusu mtu anaekunywa au Kula kuingia...hii itawasaidia usafi na kutupunguzia kero abiria ...hasa wanafunzi wa shule wanapanda mabasi huku wanakula maembe na ice cream na kutupakaza ...na kuchafua mabasi ...hili wala hakihitaji hela ..ni mabango na walinzi kusimamia
 
Back
Top Bottom