Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Mtendaji Mkuu wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Athuman Kihamia amesema:
“Nilipata taarifa ya tukio hilo kutoka kwa kiongozi wa juu ambaye alipewa taarifa kutoka kwa Abiria aliyekuwa kwenye gari, nikafika eneo la tukio lakini kwa kuchelewa kidogo na hivyo kukuta wameshamaliza changamoto iliyotokea.
“Nimepata ripoti ya kilichotokea na imebainika Derev ana Wasimamizi hawakutumia busara katika kufanya maamuzi na kuhudumia Abiria, mwisho wake wakaanza kujibizana nao na kuwatelekeza kituoni hapo badala ya kuwapeleka Kimara.
“Kuna tukio lingine linalofanana na hilo pia limetokea Kimara, tunatarajia kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika wote wanaofanya vitendo kama hivyo.
“Unapokabidhiwa huduma hiyo unatakiwa kuwa na nidhamu kwa sababu hiyo miundombinu ni ya Wananchi wao ndio wameiweka Serikali madarakani na wanahitaji huduma nzuri na wao ndio Wapiga kura.
“Tunatrajia kuchukua hatua kali ndani ya siku mbili hizi na tutatoa tamko dhidi ya Dereva aliyehusika pamoja na Wasimamizi ambao walikuwepo wakati wa tukio ili iwe fundisho kwa wengine wenye utovu wa nidhamu kazini.
“Kuna malalamiko mengi ambayo tumeyapata kuhusu huduma zetu, tunayafanyia kazi taratibu.”
Dkt. Athuman Kihamia aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika nafasi hiyo akichuku nafasi ya Dkt. Edwin P. Mhede ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Hoja ya Mdau hii hapa - Abiria wa Mwendokasi tuliotakiwa kutoka Kivukoni kwenda Kimara, Dereva katupeleka Morocco kisha akaturudisha Kivukoni