DART: Sababu ya uhaba wa mabasi ya Mwendokasi Vituoni, ni hakuna mfumo rasmi wa kuongozea mabasi, Pia mabasi ni machache

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Willium Gatambi ameeleza sababu za msongamano vituo vya 'Mwendokasi' jijini Dar es Salaam Leo Oktoba 11, 2023.

Amesema tatizo hilo linasababishwa na watu wengi asubuhi kuelekea upande mmoja pia hakuna mfumo rasmi wa kuongozea mabasi hayo.

Gatambi ameongeza kuwa Serikali inaendelea na mchakato wa kuongeza idadi ya mabasi, ambapo amesema sio jambo la mara moja.


Pia soma;
- Dar: Abiria wateseka kwenye foleni kusubiri mabasi ya mwendokasi Kituo cha Mbezi Mwisho
 
Hahahahah moja watu wameongezeka ongezeni mabasi,hahahahahaha hakuna mpango wa kununua mabasi! Aisee
 
Hahahahah moja watu wameongezeka ongezeni mabasi,hahahahahaha hakuna mpango wa kununua mabasi! Aisee
Sema tu wahusika wenyewe hawako siriasi,wana mambo yao binafsi. Ukiangalia mabasi yaliyoharibika na kutelekezwa,unajiuliza hawa watu wana akili kweli?
Viti wameng'oa. Vilienda kuwekwa wapi! Kuna gari ilikuja bila viti!?
Injini ilishatolewa. Kama gari imepaki kisa mbovu,hiyo injini wamepeleka kwenye gari gani?
Af,unajiuliza. Aliyetengeneza hayo magari,hakutegeneza spea zake? Watu wameshafanya mradi shamba la bibi, sema tu hakuna wafatiliaji.
 
Maboresho yanayotakiwa kufanyika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka Bus rapid transit (BRT) jijini Dar es Salaam.


Nimebaini changamoto kadhaa zinazotakiwa kutatuliwa katika mradi huu.


Hivyo nimemshauri juu ya maboresho yanayotakiwa kufanywa katika mradi huu. Pitia katika link hii kusoma ushauri wote: Kwako Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART): Katatue changamoto zifuatazo….


Pia michango mbalimbali imetolewa na wadau wengine na wameshauri jinsi ambavyo mfumo wa uendeshaji wa haya mabasi unapaswa kuwa ili kwendana na ukuaji wa teknolojia:


Ushauri wote tumeuandika hapa: Kwako Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART): Katatue changamoto zifuatazo….
 
Back
Top Bottom