DART yawasimamisha kazi Maafisa wa Mwendokasi walioshindwa kudhibiti vurugu zilizotokea Kituo cha Kivukoni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
WhatsApp Image 2024-03-28 at 15.51.10_0e223d14.jpg
Mnamo tarehe 26.03.2024 majira ya saa mbili usiku katika eneo la Kivukoni kwenye Kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (Mwendokasi), kulitokea hali ya vurugu kati ya abiria na madereva wa basi liendalo haraka lililokuwa linafanya safari kutoka Kivukoni Moroco.

Hali hiyo ilitokana na abiria wengi waliokua wanasubiria basi la kwenda Kimara kwa muda kuamua kuingia kwenye basi hilo la Moroco lililokua kituoni kupakia abiria wa Morroco na kumuamrisha dereva wa basi hilo akiwa na mwenzake kuwapeleka Kimara.

Madereva hao waliendelea kusimamia ratiba ya basi na kukataa kuwapeleka abiria hao Kimara hivyo kusababisha hali ya vurugu kati ya abiria na madereva hao na madereva hao kupeleka basi hilo Moroco:

Baada ya malumbano ya muda mrefu madereva wakaamua kuwarudisha abiria hao Kivukoni kitu ambacho sio busara kutokana na hali ilivyokuwepo na malumbano yalipozidi ndipo walipoamua kuwapeleka abiria hao Kimara.

Kutokana na hilo Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) inawasimamisha kazi watumishi Shabani Kajiru Msimamizi wa Kituo cha Kivukoni ambaye alipata taarifa hizi mapema na hakuzifanyia kazi na Brown Mlawa Afisa Ufuatiliaji wa Kituo kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kupisha uchunguzi wa kina.

Hali kadhalika Wakala unamuelekeza Mtoa huduma wa Mpito (UDART) kuwachukulia hatua stahiki ikiwemo kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi wa kina madareva Salehe Maziku na Chande Likotimo ambao walikua wanaendesha basi hilo kwa siku hiyo, msimamizi wa Kituo hicho Bw. Lameck Kapufi pamoja na Afisa Usafirishaji Bw. Erick Mukaro.

Aidha, DART inatoa ONYO kwa watumishi wake kuwa haitasita kuchukua hatua za haraka kwa watumishi watakao kiuka maadili ya utoaji wa huduma kwa wananchi wanaotumia usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka.

Vilevile Wakala unaomba radhi kwa kilichotokea na unaahidi kuendelea kuboresha huduma zaidi kwa wananchi; Pia tuwatake wananchi wanaotumia usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka kufuata utaratibu uliowekwa na Wakala pamoja na mtoa huduma ya usafiri na wasisite kutoa taarifa pindi wanapoona kuna suala ambalo haliendani na utaratibu uliopo ili Wakala aweze kuchukua hatua za haraka.

IMETOLEWA NA:- WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART)
Dr. Athumani J. Kihamia
MTENDAJI MKUU
TAREHE: 28.03.2024


Pia Soma
- DART kuchukua hatua dhidi ya Dereva na Wasimamizi wa Mwendokasi waliowapeleka Abiria Morocco badala ya Kimara

- Abiria wa Mwendokasi tuliotakiwa kutoka Kivukoni kwenda Kimara, Dereva katupeleka Morocco kisha akaturudisha Kivukoni
 
Anajisikia fahari kujitambulisha kama Dr. wakati hali ya usafiri wa mwendokasi ni hovyo kabisa, nina uhakika wapo wasio na kisomo wanaoweza kuyasimamia hayo mabasi vizuri sana
 
Gari za Kimara ni chache kuliko idadi ya abiria waliopo, unaweza kufika kituoni ukasimama (Maana sehemu za kukaa ni chache) hadi dk30-saa1 na Morocco zinakwenda gari nyingi kuliko idadi ya abiria.

Wakazi wa Kimara wanapitia wakati mgumu sana.
 
Anajisikia fahari kujitambulisha kama Dr. wakati hali ya usafiri wa mwendokasi ni hovyo kabisa, nina uhakika wapo wasio na kisomo wanaoweza kuyasimamia hayo mabasi vizuri sana
 
Mnamo tarehe 26.03.2024 majira ya saa mbili usiku katika eneo la Kivukoni kwenye Kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (Mwendokasi), kulitokea hali ya vurugu kati ya abiria na madereva wa basi liendalo haraka lililokuwa linafanya safari kutoka Kivukoni Moroco...
Wakupaswa kujiuzulu ni hao wakubwa wa UDART kwa sababu haya mazonge yanaanzia kwao kwa kutochukua hatua dhidi ya mrundikano wa abiria vituoni huku mabasi yakipita tupu kuelekea ama kutoka depo
 
Kwani basi zisibadilishe root kulingana na mahitaji..yaani haiingii akilini basi zinasubiria abiria wa Morocco wakati abiria wa Kimara wamejazana hapo zaidi ya saa zima. Madereva pia huenda siyo kosa Lao maana wao wamepangiwa nenda huku nenda kule. Hawajiamuliii pa kwemda. Hao maofisa ndo hopeless
 
Back
Top Bottom