101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,040
- 2,121
TAARIFA KWA UMMA
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) unawaarifu abiria wetu wa usafıiri wa Mabasi Yaendayo Haraka maarufu Mwendokasi, kuwa leo Novemba 5, 2023 Saa 6:30 Mchana, barabara ya Morogoro eneo la Jangwani imefungwa.
Changamoto hii inasabishwa na Mvua kubwa inayoendelea kunyesha Dar es Salaam, na hivyo kusababisha barabara katika eneo la Jangwani kujaa maji. Hivyo kwa sasa Mabasi Yaendayo Haraka yanaendelea kutoa huduma kupitia barabara ya Kawawa inayopita eneo la Kigogo na Karume mpaka pale hali itakavyokua shwari. Wakala wa DARTunaomba radhi abiria wote kutoka na changamoto hii inayowaathiri kutokufika kwa wakati maeneo wanayokwenda.
Aidha, huduma za mabasi yetu katika Njia Mlishi ya Kimara hadi Mbezi, Kimara hadi Kibaha, Kimara hadi Mloganzila na Muhimbili hadi Gerezani zinaendelea kutolewa kama kawaida.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka - DART
Novemba 5, 2023
View attachment 2804767