Cyprian Musiba Anadaiwa zaidi ya Tsh13 bilioni kwa amri za Mahakama Kuu, iwapo atashindwa kulipa ni nini hatma yake?

Naunga mkono hoja , halafu ile taasisi inayochapisha magazeti yake itoe bil 5 za serikali halafu zilizobaki nyinyi chawa wake muimalizie
 
Leo ni siku ya giza katika ulimwengu wa uhuru wa habari. Musiba hilo deni ni dogo sana katika watu wanaoamini katika uhuru wa habari na kujieleza. Wape namba marafiki zako wakubwa waanzishe kampeni mitandaoni ya kuchangia faini.
Ebu imagine vigogo hawa waanzishe kampeni mitandaoni ya kumchangia mwandishi Musiba aliyepigwa faini sababu ya kufanya kazi yake ya uandishi. Lissu, Fatma Karume, Maria Sarungi, Zitto, Jenerali Ulimwengu,Msigwa, Lema, Mnyika,Mange Kimambi, Kigogo, Kubenea,Mbowe atume mwakilishi, Maxence Melo, Membe mwenywe, bwana mdogo Nondo. Hakika hata msaa 10 HAYATAPITA HELA ITAKUWA IMEPATIKANA NA DEMKRASIA ITAKUWA IMELINDWA NCHINI
Wewe unamchangia kiasi gani tuanzie hapo kwanza.
 
Haki ya nani Membe kwa kumkomesha atalipa hizo gharama za jela. Membe Kwa hasira aliyo nayo nakwambia atalipa wala hakamati Mali. Musiba ana Mali gani za billion 6. Karume naye 7.5 BN na Prof Tibaijuka 80m za mboga.

Hapa iwe funzo kuwa kukubali kutumika kisiasa iko siku utatembea ni vijambo na ushuzi tu vinatoka. Huyu Musiba alijuona Mwamba. Waliomtumia ni wengi tu siyo yule aliyekwenda zake tu Bali wako wengine. Mbona hatusikii wakimtetea? Kawaida toilet tissue ukishaitumia inatupwa. Tujifunze na tujifunze tena.

Mwendazake hawajawahi kumtumia hata siku Moja. Ni hisia zenu mbofu tu.
 
Duniani tunapita
obama.png
Yap!
 
Hiki kipengele cha pili ni cha ajabu kweli, kwa nini isingekuwa afungwe gerezani na kufanya kazi za umma mfano kufagia barabara, kufyeka majani na kukata miti/matawi, kusafisha vyoo vya umma kwenye maofisi ya umma, mahospitali etc etc??
Anayekudai sasa atanufaikaje na hizo shughuli za kijamii utakazofanya, atapataje pesa yake kwa njia hiyo.
 
Kwenye hizi Kesi za madai inaweza kuwa hivi Kama mdaiwa hajalipa:-

1. Unaomba Mahakamani kukazia hukumu huku ukiambatisha Mali unazozijua za mdaiwa ili mahakama iziuze ili ulipwe fedha unazodai.
Mahakama itazikamata Mali hizo kwa kutumia mabroker wake na kuziuza ili ulipwe.

2. Kama Hana Mali zozote unaweza kuitaka mahakama iamue mtu huyo unayemdai akae jela kwa gharama zako hadi atakapokulipa fedha unazomdai
Kama atakaa jela na kashindwa Kabisa kabisa kulipia bilioni 6 ,Sheria inasemaje?
 
Back
Top Bottom