Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,375
- 14,870
Nikweli nilikuwa mnywaji(sio mlevi) miaka 3 nyuma, nimeacha na sijawahi kukereka kwa chochote afanyapo mtu ambacho mimi sifanyi na hakivunji sheria. Nakushauri jali mambo ufanyao, ishu za watu wengine ambazo huzipendi lakini ni hali na hazi gusi maisha yako achananazo kwa ajili ya ustawi wa moyo na ubongo wako.
Na mimi sijamkataza na kamwe sitamkataza mtu kufanya chochote apendacho jinsi mimi siwezi kukatazwa kufanya chochote kisichovunja sheria lakini hawezi mtu YEYOTE kunizuia kutoa maoni, ushauri au hata onyo kwa ajili ya Watu wanaoweza kupokea mambo hayo na hapo halazimishwi mtu kufuata hayo maoni, ushauri nk,.
Hakuna mtu mwenye AKILI timanu atakayesema Pombe ni nzuri na ndio maana wewe ukaiacha, watu wengi wanakunywa Pombe lakini ndani ya nyoyo zao wangetamani kuacha lakini wanashindwa kutokana na addiction ---- kifupi ni kwamba Pombe ni mbaya hata katika Biblia na Qur'an kwa maana kwamba Mungu hataki watu tunywe pombe, kuichukia kwangu pombe ni kujaribu kutanabahisha umma kwamba pombe sio kitu kizuri, ama upokee au ukatae hiyo ni juu yako WALA SIJALAZIMISHA MTU.