Hassan Mwakinyo: Siogopi mabondia wenye miili mikubwa hasa wapaka pico

franckkimm

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
440
852
BONDIA kutoka Tanga Hassan Mwakinyo ametoa maneno ‘mbofumbofu’ ( katupa jiwe gizani ) kwa kueleza kwamba haogopi mabondia wenye miili mikubwa na pia huwa anafurahia kuona ‘piko’ anazojichora bondia huyo.

Huo ni mkwara kwa moja ya mabondia Bongo ambao wana michoro kwenye miili pamoja na kuwa na umbo kubwa.

Mkwakinyo karusha jiwe gizani ambapo hajamtaja bondia ambaye wamekuwa wakiingia kwenye vita ya maneno mara kwa mara, kila mmoja akimtambia mwenzake.

“Siogopi mabondia wenye miili mikubwa ama michoro kwenye miili yao sina hofu katika hilo nipo imara,”.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vema angekaa kimya, kama hataki kupigana nae, hapaswi kuleta maneno maneno,
Mwakinyo alipata nafasi nzuri brand yake ikakuwa, lakini uswahili na kutokujielewa vinamshusha taraatibu.

Mara ya kwanza nilimuelewa saana alipokataa kupigana na kiduku(kwa sababu fulani fulani nilimuona yupo sahihi kabisa), akahamia marekani nikasema yes, sasa hivi wabongo titakuwa na professional boxer kweli kweli sio PROFESHNO BOKSA, Lakini toka auze pambano la uingereza, kisha huku analeta nyodo za kishoga naona anajiharibia tu.
 
Yaani huyo Mwakinyo akae tu kwa kutulia amalizie zile pesa alizohongwa akauza pambano. Yaani sala za watanzania wengi tuliokuwa tunamuombea ashinde lile pambano na uwezo alikuwa nao halafu mwenzetu kumbe kauza mechi. Nina hakika zile sala zimegeuka laana kwake ndio maana kila anachogusa sasa anakula za uso kabakia tu kuweweseka na mipasho mingi na anagombana na kila mtu. Yaani Mwakinyo bila kutubu kwa Mungu na kuwaomba radhi watanzania kwa kosa la kuuza mechi (tena aliuza kijinga kabisa kila mwenye akili akagundua) basi ngumi ndio bai bai atafute tu kazi/biashara nyingine ya kufanya.
 
Watanzania kwa umbea hayo mambo mabondia wanafanya maksudi ili ku promote mapambano yao ila watu wanayachukulia serious kuliko wahusika wenyewe.
Na ndio lengo la mwakinyo. Kauli yake iyo itaamsha mapromota wafikirie kuandaa pambano la hao wawili. Ingawa sina uhakika kama inawezekana nahisi kiduku yupo uzito wa juu kidogo
 
Ni vema angekaa kimya, kama hataki kupigana nae, hapaswi kuleta maneno maneno,
Mwakinyo alipata nafasi nzuri brand yake ikakuwa, lakini uswahili na kutokujielewa vinamshusha taraatibu.

Mara ya kwanza nilimuelewa saana alipokataa kupigana na kiduku(kwa sababu fulani fulani nilimuona yupo sahihi kabisa), akahamia marekani nikasema yes, sasa hivi wabongo titakuwa na professional boxer kweli kweli sio PROFESHNO BOKSA, Lakini toka auze pambano la uingereza, kisha huku analeta nyodo za kishoga naona anajiharibia tu.
Boxing lazima maneno majigambo yawepo

Ova
 
Anachokifanya mwakinyo ni kucheza na alama za nyakati. Wakati ule kiduku yuko hot mwakey alikua anamkataa kwa kigezo hapigani ngumi local, sasa hivi kiduku ame drop, si yule wa zamani ndio mshkaji anamchokonoa.
Umeona eee,sahv ameshaona ana mmudu ndo anajishebedua,zaman aliogopa
 
Boxing lazima maneno majigambo yawepo

Ova
Majigambo yanaenda na vitendo.. Mie binafsi nilimuelewa kipindi kile, baada ya kuibukia uingereza mapromota wakawa wanaleta shobo kumpiganisha na kiduku, wakati huo yeye akilinda kile alichokipata uingereza, kina kiduku walitaka kama ngazi kwa mwakinyo.
Ilitosha kumfungia vioo, ukiwa unaongea saana kwende na vitendo, kina Muhammad ali hawakuwa wanabwabwaja tu, wanaongea kisha wanafanya kweli.
 
Mwakinyo anajua biashara ya ngumi,, anachokifanya ni mkakati maana mtataka kufatilia nini anafanya kwakua mnamchukia, ikitokea akapata pambano litafuatiliwa sana kwa mashabiki wake na wanaomchukia,,,mimi naona yupo kibiashara zaidi na kujenga brand yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom