Elton Tonny
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 260
- 1,871
DYLAN
Story by Elton Tonny
Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa
(R-rated 18+)
WhatsApp +255 787 604 893
E-mail: eltontonny72@gmail.com
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA KWANZA
★★★★★★★★★★★★
2005
TANZANIA
Tunaona mvulana mdogo akiwa ndani ya chumba chake. Anatazama TV ndogo ukutani inayoonyesha filamu fulani kutoka kwenye deki inayomsisimua sana. Ameketi kitandani huku anaangalia kwa makini matukio ya kwenye filamu hiyo, na tabasamu lake linaonyesha wazi jinsi gani anavyofurahishwa na vitendo vinavyoonyeshwa.
Anashika rimoti ya deki, na kuanza kurudisha nyuma sehemu fulani ya filamu hiyo, kisha anaanza kuiangalia tena. Kila mara sehemu hiyo inapoisha, anairudisha tena na tena kuitazama kwa umakini. Sehemu hii inaonyesha watu wawili wakipigana, na chini yao kuna maji kiasi miguuni yanayotawala chumba walichopo. Pembeni yao kuna moto unaowaka kuwazunguka, nao wanapigana kwa mtindo wa kupeleka miili yao kwa sarakasi zenye ustadi sana.
"Dylan..."
Anasikia sauti hiyo anayoifahamu vizuri sana ikiita jina lake. Anageuka na kutazama upande wa mlangoni, na hapo anapata kumwona mama yake akiwa amesimama, huku anamwangalia kwa mshangao.
"...what are you doing? Kwa nini bado hujajiandaa?" mama yake anamuuliza.
Dylan anageukia TV tena na kuendelea kuangalia. Mama yake anamfata alipo na kumnyang'anya rimoti kisha kuisimamisha filamu hiyo.
"Aah..mama!" Dylan analalamika.
"Kimya. Una matatizo gani? Unajua nimekwambia ndege inaondoka mapema, halafu wewe umekaa kuangalia hiyo midude yako. Hivi kwanza umeipataje hiyo CD wakati nilikuwa nimeificha?" mama yake akamuuliza.
"Aheheheh...achana na mimi wewe!" Dylan akamwambia kiutani.
"Hebu acha sifa. Fanya haraka la sivyo utaona," mama yake akamtishia.
Dylan akaweka uso wa kununa.
"Jaquelin..."
Sauti hiyo ikasikika kutokea mlangoni, na wote wakatazama hapo. Ilikuwa ni baba yake Dylan.
"...simu yako inaita huko chini. Ni Alfred," akasema.
"Sa' siungeniletea?" mama yake Dylan akauliza.
"Aah..nzito bwana," mume wake akajibu.
Jaquelin akazungusha macho yake na kuanza kuelekea mlangoni. Alipomfikia mume wake akampiga kidogo kwa kalio lake kisha kuondoka, naye baba yake Dylan akatabasamu huku akiwa amekunjia mikono yake kifuani. Akamtazama Dylan, ambaye bado alikuwa anajifanya kanuna, kisha akamfata mpaka kitandani alipoketi na kukaa pamoja naye.
"Mama anasumbua eeh?" akamsemesha mwanae.
"Yaani!" Dylan akajibu.
"Ahahahah..unajua hiyo ni kwa kuwa yuko excited kwa sababu..."
"...ninaenda Brazil," Dylan akamalizia.
Baba yake akatabasamu.
"Baba, kwani lazima niende huko? Halafu nimesikia wanavuta mabangi sana kule, nikirudi mvuta bangi shauri yenu," Dylan akasema.
Baba yake akacheka na kuzungushia mkono wake begani kwa mwanae.
"Unataka kuwa mvuta bangi?" baba yake akamuuliza.
"Siyo mimi..ila inaonekana ndo' nyie mnachokitaka," Dylan akasema huku bado kanuna.
"Hapana Dylan. Tunafanya hivi ili uweze kuwa na maisha bora baadae. Na usiamini ulichosikia, kwa sababu wavuta bangi wako kila sehemu, lakini unanionaje mimi, navuta bangi?" baba yake akamuuliza.
Dylan akamgeukia, kisha akamnusa kwenye shati lake kidogo eti ili kuhakikisha.
"Siwezi kujua..huu utawala wa Kikwete labda kuna bangi zinanukia siku hizi!" Dylan akatania.
Wote wakacheka kwa pamoja na kuanza kusukumana kiutani, kisha Dylan akawa ameacha kununa sasa.
"Kuna nafasi nzuri hata zaidi ya wewe kupata mafanikio ukisomea kule. Fikiria, utajua lugha nyingine..." baba yake akasema.
"Boring..." Dylan akasema kivivu.
"Utakutana na watu wapya na kuona mambo mengi mazuri..."
"Boring..."
"Vitu vingi vizuri zaidi hata ya vya huku..."
"Boring..."
"Watoto wazuri..." baba yake akamtega.
Dylan akamwangalia usoni kisha akasema, "Cooling..."
"Ahahahah...kichwa chako!"
Wote wakacheka tena. Dylan alikuwa mvulana mwenye akili sana. Alianza kujifunza vitu mapema sana na kuingia shule akiwa na miaka mitatu na nusu tu. Kuanzia masomo ya awali mpaka ya msingi, kwenye masomo yote sikuzote alipata alama za juu, na alipenda michezo mingi na kujishirikisha nayo pia. Kutokana na werevu wake mwingi, baadhi ya walimu wake hata walimwita "Genius."
Wakati huu, alikuwa na safari ya kuelekea nchini Brazil, ambako shangazi yake, yaani dada mdogo wa baba yake aliishi. Alipendezwa sana na Dylan, hivyo akawa amewaambia wazazi wa mvulana huyu aende kusomea kule ambako angepata kujua mambo mengi na kupanua hekima yake hata zaidi kielimu na kitaaluma.
Hii ndiyo ilikuwa asubuhi ambayo Dylan alipaswa kupanda ndege ili aanzishe safari ya kuelekea kule, lakini yeye akawa anaangalia filamu ya The Protector aliyoipenda sana. Baba yake akachukua rimoti na kuiendeleza sehemu ile ambayo shujaa wa filamu alikuwa akipigana na adui yake. Dylan akaanza kuitazama tena kwa upendezi mwingi.
"Unampenda Tony Jaa?" baba yake akamuuliza.
"Ndiyo," akajibu.
"Mhm..naonaga unapenda sana kuiangalia hii sehemu. Unapenda anavyopigana hapo eeh?"
"Actually...naipenda hii sehemu kwa sababu ya adui yake, siyo yeye."
"Kweli? Kwa nini?"
"Angalia."
Akachukua rimoti na kurudisha tena sehemu hiyo, kisha kuanza kumwonyesha baba yake jinsi adui huyo alivyopigana kwa mtindo wenye ustadi sana.
"I just love it. Anavyofanya, kama anacheza muziki, lakini ni hicho ndiyo kinampoteza na kumchanganya huyu Tony Jaa," Dylan akaeleza.
"Yeah ni nzuri. Unajua hivyo vitu vimetokea wapi?" baba yake akamuuliza.
Dylan akatikisa kichwa kukataa.
"Hizo style zinatokea Brazil. Watu wa kule ndiyo wanaofanya sana mambo hayo na kuyasambaza kwa wengine ili wajifunze," akamtaarifu.
"Kweli?" Dylan akauliza kwa shauku.
"Ndiyo."
Dylan akatazama tena TV kwa kufurahi kujua hilo.
"Dylan, nisikilize. Kule unakoenda najua mazingira yatakuwa tofauti, na mwanzoni unaweza ukahisi labda..uko mpweke. Lakini..."
"Baba usikonde. Me ndiyo Dylan. Hanisumbui mtu kule," akajisifu.
"Ahahahah..safi sana. Ila kuhusu watoto wazuri, nilikuwa natania tu. Usije uka..." baba yake akaishia hivyo huku anamkata jicho.
"Aah..mimi tena? Wala hata usiwaze. Mtoto mzuri kule kwangu atakuwa ni ma'mdogo tu," akasema Dylan.
"That's my boy. Hop top..." baba yake akasema huku ananyanyua kiganja chake, kisha Dylan akakigongesha chake hapo.
"Dylan! hivi bado..."
Sauti ya juu ya mama yake ikasikika kutokea mlangoni akishangaa kuona Dylan hajajiandaa bado. Hapo hapo Dylan akakimbilia bafuni na kujifungia humo, akimwacha baba yake anacheka.
"Beatrice amejifungua!" Jaquelin akamwambia mume wake.
"Wow...kweli? Saa ngapi?"
"Alfred ameniambia usiku wa saa 10. Amejifungua kavulana."
"Ahah...inapendeza sana."
"Inabidi tumwahishe huyu ili tuelekee hospitali kumwona."
"Sawa."
Baada ya Dylan kumaliza kujiandaa na kuvaa vizuri, walimpeleka mpaka uwanja wa ndege na kumsihi awe makini mpaka atakapofika kule. Wakiwa nje ya sehemu ya kuingilia ndani kule, mama yake alirudia mara nyingi maneno yale yale aliyokuwa amekwishamwambia, na Dylan akawa ameshaelewa kuwa mama yake alikuwa na huzuni kiasi kumuacha. Hivyo akamkumbatia na kumkonyeza baba yake aliyekuwa amesimama nyuma ya mama yake, kisha akaanza kuelekea sehemu ya ndani ya uwanja wa ndege. Alikuwa mwenye kujiamini sana Dylan, na wazazi wake walijivunia sana kuwa naye kama mwanao.
Wazazi wake waliendelea kusimama hapo mpaka ndege ilipopanda angani, Dylan akiwa amewaacha kuelekea kwa shangazi yake.......
2021
Tunaingia moja kwa moja mpaka kwenye kampuni moja kubwa sana. Kampuni hii ni ya kisasa, inayohusiana na masuala ya ujenzi na ukandarasi (construction company) wa majengo, miundombinu mbalimbali, na masuala mengi kuhusiana na ukandarasi. Ni kampuni ambayo imekuwepo kwa miaka mingi, na imepatwa na panda shuka nyingi inapokuja kwenye suala la maendeleo.
Kampuni hii ilianzishwa na kuundwa vyema na baba yake Dylan. Ilianza kama duka la vifaa tu vya ujenzi na ukandarasi, na mwishowe ikakua kutokana na watu wengi kuvutiwa na huduma za haraka na zenye kutegemeka kutoka hapo. Wakati huu, kulikuwa kumezuka suala ambalo lilileta utata juu ya uendeshaji wa kampuni hii, kwa kuwa washiriki wakubwa waliowekeza hisa zao nyingi kwenye kampuni walihisi mafanikio yameanza kurudi nyuma.
Akishirikiana na mke wake, baba yake Dylan alijitahidi sana kuongoza kwa njia ambayo ingewahakikishia washiriki hao kuwa kampuni haingeporomoka, ijapokuwa mambo mengi yalionekana kwenda mrama.
"...ahadi nyingi unazotoa zinafanya matumaini yao yanyanyuke. Unafikiri itakuwaje wakipata kujua pesa zao hazifanyi kazi kama matarajio yao yalivyo, na zinaishia kupotea tu wakati hatupati faida kubwa?" akawa anafoka mwanaume mtu mzima ofisini kwa baba yake Dylan.
"Baba! Tafadhali...ninajua ninachofanya. Naomba uache niongoze kampuni kwa njia nayojua kuwa bora," baba yake Dylan akasema.
"Bora? Its more than obvious kwamba productivity levels within the company zinafeli!" akamfokea.
"NAJUA!!!" baba yake Dylan akafoka pia akiwa amenyanyuka kutoka kwenye kiti chake.
Wote wakawa wanatazamana kwa hasira sana ofisini hapo. Mzee wake baba Dylan alijua sana pia masuala mengi kuhusiana na kampuni hii, naye alikuwa mmojawapo wa wawekezaji wakubwa hapo. Alikuwa mwenye hasira kumwelekea baba Dylan na kila wakati angetafuta sababu za kumfanya ajihisi hawezi kushughulikia mambo kikamili.
"Basi jamani..mpaka mgombane?" akasema mama Dylan (Jaquelin), ambaye pia alikuwa hapo ofisini.
"Hauna adabu wewe. Unafikiri tu kwa sababu wewe ndiyo raisi wa kampuni basi haupaswi kuambiwa unapoboronga?" mzee akamwambia baba Dylan.
"Ninajua kinachoendelea. Ninaijua kampuni yangu vizuri, sihitaji uniambie vitu hivi. Kama hauwezi kunisaidia kutafuta suluhisho na kukaa tu unalalamika, ni bora uondoke!" baba Dylan akamwambia kwa ukali.
"Gilbert, hebu acha basi!" Jaquelin akamwambia baba Dylan.
Mzee wake akamsonta Gilbert na kidole huku amemkazia macho, kisha akaondoka ofisini humo kwa hasira. Gilbert akajishika kiunoni, na kuanza kuzunguka huku na huku akihisi ghadhabu kubwa pia. Kisha akachukua vitabu kutoka kwenye maktaba ndogo humo na kuvitupa chini kwa nguvu; akiitoa hasira yake namna hiyo. Jaquelin alikuwa anamwangalia tu kwa uso wa kutojali, kisha akazungusha macho yake kwa kejeli na kupigia mtu fulani simu. Akamwita aje ofisini hapo, kisha akakata simu.
"You and your dad acting like ten year olds (wewe na baba yako mlivyo kama watoto wa miaka kumi)," Jaquelin akamwambia Gilbert.
Gilbert akawa tu anaangalia nje ya kioo kipana cha jengo hilo huku amekunja sura yake kwa kuudhika.
"Mkutano unaofuata ni lini?" akamuuliza.
Gilbert akaendelea tu kukaa kimya.
"Si nakuuliza swali?" Jaquelin akasema kwa ukali.
"Kesho," Gilbert akajibu kibaridi tu.
"Ahah...umeshaandaa cha kuwaambia hao makolo au ndo' utakaa kuwatupia vitabu na wenyewe?"
"Jaquelin please...naomba uniache. Siko kwenye mood."
Ni hapa ndipo aliingia mwanaume fulani kijana ofisini humo baada ya kupiga hodi na kukaribishwa.
"Madam, nimefika..." akasema.
"Robert, chukua hayo mafaili uyasambaze kwa department zote ghorofa ya tatu, umeelewa?" Jaquelin akamwambia.
"Ndiyo madam. Zinahusiana na nini?" akamuuliza.
Jaquelin akamwangalia kwa ukali mpaka jamaa akajing'ata.
"S..sorry. Ngoja niwahishe," akasema huku anayachukua mafaili hayo, na kisha kuondoka.
"Pesa za kampuni unazotumia kuwahonga wanawake ndiyo zinaleta haya matatizo," Jaquelin akasema.
"Una uhakika gani ninahonga mwanamke pesa, Jaquelin?" Gilbert akauliza huku anamtazama.
"Ahahahah...just kidding. Najua hauna hayo masuala ya mahawala," Jaquelin akasema.
Ijapokuwa alionyesha kwa mume wake kwamba alitania tu, moyoni mwake alijihakikishia kwamba alichomwambia kilikuwa kweli. Kwa muda mrefu sasa, ndoa yao ilikuwa ikisumbuliwa na visa vya kutoaminiana kutokana na kila mmoja wao kudai mwenzake anatoka kimapenzi na mtu mwingine, lakini walijitahidi kuendelea kuisongesha kwa ajili ya kampuni na sifa yao ya hadharani (reputation).
"Kwa hiyo utafanyaje?" Jaquelin akamuuliza.
"Just give me until tommorow, I'll think of something (niache tu mpaka kufikia kesho, nitafikiria cha kufannya)," Gilbert akajibu.
"Wazo langu ulilitilia maanani, au ukali-bullshit tu?"
"Nini? Wazo...kuhusu..."
"Ndiyo."
"Jaquelin, sidhani kama itakuwa busara kwa sababu yeye hataki kujihusisha na haya masuala. Na mimi sitaki kulazimisha."
"Yaani unavyosema hivyo utafikiri hata umeongea naye."
"Ndiyo amerudi juzi tu. Hana mambo mengi anayoyajua kuhusu hapa. Sitaki kumbebesha mizigo ambayo hataki kubeba."
"Hataki? Unajuaje hilo? Imani yako yote uliyokuwa nayo kwake imeenda wapi? Gilbert, Dylan ndiyo anayeweza kuwa suluhisho letu. Usikae kusingizia kwamba hataki wakati unaogopa tu kwa sababu ya hisia zako za hatia..."
"Jaquelin..."
"...haihusu, Gilbert. Dylan ana uwezo wote wa kuhandle suala hili na kulitatua. Acha kuigiza kama haujui hilo. Ongea naye, na mimi nitaongea naye. Usipofanya hivyo kwa sababu ya kiburi chako, you'll get to see your own downfall..I promise you," Jaquelin akasema kwa mkazo.
Gilbert akawa kimya tu akitafakari maneno ya mke wake.
Jaquelin akamwacha ofisini humo na kuelekea kwenye ya kwake. Alipofika na kuketi kwenye kiti chake, akatoa simu na kumpigia Dylan, lakini hakumpata. Akajaribu mara nyingi sana bila mafanikio, kisha akaiweka simu mezani kwa hasira huku amekunja sura yake kwa kukosa subira.
"Ameenda wapi huyu?" akajiuliza.
★★★
Tunakuja moja kwa moja mpaka sehemu fulani ambayo iko mbali kwenye msitu mkubwa. Imejificha mno kutokana na watu walio huko kutotaka ijulikane kwa watu wasioruhusiwa kuingia. Kuna watu kadhaa ambao huwa wana kawaida ya kwenda hapo kwa ajili ya kujitumbuiza; kwa njia fulani ambayo siyo ya kawaida kama vitumbuizo vingine vinavyokuwa.
Ni sehemu maalumu kwa ajili ya mapigano ya mieleka ambayo hayatambuliki kisheria na ni haramu (illegal). Watu hutoa pesa za bahati nasibu (bet) kupitia mtandao fulani ambao umefichwa kisiri na wataalamu wa programu hiyo inayofanywa kwa ajili ya kuingiza pesa. Hii inamaanisha kwamba, mtu anaweza ku-bet kwa mpiganaji mmoja, na ikiwa atashinda, basi anapata kiasi fulani cha pesa kwa makubaliano aliyoweka.
Kunakuwa na wapiganaji ambao wanadhaminiwa na mtu fulani mwenye pesa, hivyo wao wanapigana mechi ambazo zinaonwa kuwa kubwa sana, na atakaeshinda anapata pesa nyingi sana ambazo zinaenda kwa anayemdhamini; yeye akilipwa kiasi alichoahidiwa. Wanaojua kuhusu jambo hili ni wale wenye mtandao huu, na wanapolipa wanaweza kuangalia mapambano haya hewani (online). Kwa kuwa hakuna ujuzi wa ni wapi yanapofanyikia, haiwi rahisi kwa vyombo vya usalama kutambua walipo ili wachukuliwe hatua.
Kila mpiganaji anakuwa anavaa kiziba uso (mask) ili kuficha utambulisho wao. Wanapewa majina ya sifa kuweza kuwatambulisha kwa mashabiki wao na wanaowadhamini. Kufikia wakati huu, mapambano haya yana wapiganaji 20 ambao wanafahamika kwa majina yao ya sifa, bila watu kujua kihalisi wao ni nani.
Mpiganaji anayependwa zaidi na watu, anajiita "Killmonger," jina linalofanana na mhusika fulani wa filamu ya kimarekani inayoitwa Black Panther. Anapendwa sana kutokana na mtindo wake wa kupigana ambao uko tofauti na mitindo mingine wapiganaji wanayotumia. Na kinachoongeza upendo wa mashabiki kumwelekea ni kwamba tokea alipojiingiza kwenye mashindano haya wiki tatu tu zilizopita, amepigana mara 9 na wapiganaji tofauti, na mechi hizo zote alishinda.
Wakati huu sasa ilikuwa siku ya pambano kama kawaida. Ikafika usiku wa saa 4, nayo ikawa ni zamu ya mpiganaji mmoja aliyejiita "Kishoka," pamoja na Killmonger. Wahuni walimwaga pesa kwenye mtandao huo ili kupata burudani maana Kishoka na Killmonger wote walikuwa hatari sana. Wadhamini wa Kishoka waliweka bet kubwa kwa Killmonger kushindwa, lakini kwa upande wa Killmonger, ilikuwa ni mashabiki tu; yeye hakuwa na wadhamini.
Wote wakaingia kwenye kiwanja cha vumbi kilichokuwa kimezungukwa na camera kadhaa juu na pembeni yao, zilizofuata nyendo zao ili kuwaonyeshea mashabiki waliotazama mtandaoni. Kuuzungukia uwanja huu, waliketi watu muhimu hapo waliouendesha mchezo huu na wale waliodhamini wapiganaji; watu wenye pesa.
Killmonger alikuwa mwenye kujiachia sana. 'Mask' aliyovaa ilimziba usoni kufikia puani, hivyo mdomo wake ulikuwa wazi. Alipendelea kutabasamu na kuchukulia kila kitu kimasihara sana. Alikuwa mrefu kiasi, mwenye mwili uliojengeka vizuri, na alipendelea kuvaa suruali ndefu na pana ya kimichezo kila alipopigana na kuacha kifua chake kikiwa wazi. Alikuwa na nywele ndefu zilizotengenezwa kwa mtindo wa rasi kichwani, naye alizibana kwa nyuma.
Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Kishoka na Killmonger kupambana, hivyo watu walikuwa na hamu kuona ni nani angeibuka mshindi kati yao. Kabla pambano halijaanza, kulikuwa na mwanamke fulani mzungu aliyevalia nguo nyeusi yenye kumbana vyema, na viatu virefu chini, aliyeketi upande wa juu wa watu waliodhamini wapiganaji. Alikuwa akimtazama kwa makini Killmonger; jinsi ambavyo alionyesha uchangamfu kuelekea pigano hilo.
Kengele ilipogongwa, Kishoka alikunja ngumi na kusimama kwa pozi la utayari wa pambano. Yeye alivaa 'mask' iliyofunika kichwa chake chote na kuacha macho wazi, kama jasusi. Alikuwa na mwili mkubwa pia, na alipenda kuvaa T-shirt nyeusi iliyombana pamoja na suruali nyeusi pia. Mabuti yake yalimfanya aonekane kama jasusi kweli.
Lakini Killmonger hakuwa ametulia. Alicheza-cheza sana; akipeleka kichwa na mgongo wake huku na huku, akizungusha-zungusha miguu yake na kuwa kama anacheza muziki wa dansi kwa mtindo huo. Ilikuwa ndiyo njia yake ya kupigana iliyofanya watu wampende sana, maana sikuzote hakutabirika kuhusu chochote ambacho angefanya (mtindo huu wa kupigana huitwa Capoeira).
Kishoka akamfata kwa kasi na kurusha ngumi nzito ili impige, lakini Killmonger akafanya kama anataka kuruka sarakasi ya nyuma ila akazungusha miguu yake juu na kuukunja mmoja uliokipiga kisogo cha Kishoka na kumfanya akaribie kuangukia mbele. Killmonger alijirusha-rusha sana kwa sarakasi, mara huku, mara kule, mpaka Kishoka akawa anashindwa amfate vipi. Lakini mara tu alipoona amepata nafasi, akamrukia tena, lakini Killmonger tayari alikuwa ameshaona angekuja vipi, hivyo akamkwepa kwa sarakasi nyingine yenye utundu.
Alikuwa akiruka sarakasi nyingi na kurusha mateke yaliyompata Kishoka sehemu kadhaa. Ilikuwa ni kama Killmonger hakuguswa kabisa na Kishoka, kwa sababu aliendeleza michezo yake huku akimdukunyua hapa na pale jamaa. Baada ya kuanza kuona Kishoka anafanya mambo kwa hasira badala ya akili, Killmonger akajiachia ili jamaa ampige. Huu ndiyo ulikuwa mchezo wake. Alipenda kumfanya mwenzake apate matumaini, ili alegeze kidogo sehemu aliyoona kuwa na udhaifu, kisha autumie kummaliza.
Kishoka akampiga Killmonger tumboni jamaa alipokuwa amesimamisha mwili kichwa chini miguu juu huku ameweka mkono wake mmoja tu chini, naye akaanguka na kulala chini. Kisha, kwa ujanja, Killmonger akawa anajifanya ameumia hivyo ni ngumu kwake kunyanyuka, na hapo Kishoka akaanza kumfata taratibu huku anajisifu. Wadhamini wake walikuwa wanapiga kelele kwake kuwa ammalize Killmonger, huku yule mwanamke akimtazama kwa makini Killmonger pale chini.
Kisha wakati Kishoka aliposogea na kutaka kumkanyaga jamaa chini, Killmonger aliuzungusha mgongo wake kwa ufundi sana hapo chini, huku mikono yake ikimnyanyua juu kadiri alivyoendelea kuzunguka. Hii ilimshtua Kishoka, naye akashindwa kuelewa mwili wa adui yake ulikuwa katika mtindo gani. Hapo Killmonger akawa anazunguka kwa mikono yake kwa kasi sana, kisha akaushusha mguu mmoja akiwa ameunyoosha na kuupiga wa Kishoka kwa nguvu.
Kishoka alidondokea kisogo chake na kukibamiza kwa nguvu sana, huku Killmonger akizungusha mwili wake ukiwa umenyooka kwa kuweka mkono mmoja chini, na kuendelea kufanya hivyo kimasihara. Yule mwanamke akatabasamu baada ya kuona utundu huo mwingi wa jamaa, na sasa Killmonger akatua chini na kusimama kwa miguu huku anatabasamu.
Kishoka akajitahidi kusimama huku anaweweseka, lakini Killmonger akajirusha sarakasi hewani na kumtandika teke la shavu jamaa na kumfanya adondoke chini kama zigo zito. Akaja mwamuzi na kumwangalia Kishoka, kisha akamfata Killmonger na kuunyanyua mkono wake kuonyesha ndiye mshindi. Watu kadhaa waliokuwepo pale walimshangilia na kuanza kuimba, "Killmonger, Killmonger, Killmonger..."
Wadhamini waliopoteza pesa kwa sababu yake walikasirika sana, kwa kuwa kwa mara nyingine tena Killmonger alithibitisha hakuna anayemweza. Baada ya pambano hili, mtandao ulifungwa kwa wakati huo mpaka pambano lingine, hivyo kwa eneo hilo walilokuwepo wapiganaji, watu walianza kuchangamka ili waondoke. Killmonger alikwenda na kunywa maji, kisha akaja mtu fulani ambaye ndiye aliyemsaidia mpaka akaweza kufika kwenye mapambano haya.
"Oya mwanangu, safi sana. Umeua show na leo tena kama kawaida yako. Pesa imeingia bro, kama vipi tukapate bata club au siyo?" akamwambia.
"We nenda tu, Bosco. Me nna mambo mengine," akajibu Killmonger.
"Aaaaa...mbona unazingua kaka? Au unaogopa nitakuvulisha mask ukilewa?"
"Ahahahah..hicho hicho."
Wakaanza kufika baadhi ya watu sehemu hiyo na kumpongeza Killmonger kwa ushindi wake. Kisha akafika mwanamke fulani mwembamba na kumnong'oneza kitu fulani Bosco. Bosco akaweka uso wa kushangaa kiasi, kisha akamvuta Killmonger pembeni.
"Oya..zari baba," akamwambia.
"Tatizo nini B?" Killmonger akauliza.
"Huyo hapo demu, ametumwa na Queen, anasema anakuita," akamtaarifu.
"Ananiita ili iweje?"
"Sijui. Ila nafikiri anataka kuongea nawe kuhusu jambo la muhimu."
"Mwambie kibaraka wake sina huo muda. Nawahi nyumbani, sikuacha hela ya matumizi," Killmonger akatania.
"D...Killmonger...nisikilize. Hapa hauwezi..."
"Bosco, nimekwambia nawahi nyumbani. Kama alikuwa anataka kuongea na mimi si angeniita kabla mchezo haujaanza? Dada, nenda kamwambie nimeshaondoka," Killmonger akasema kwa kujiamini.
Kisha akachukua begi lake na kuliweka mgongoni na kumwambia Bosco anaondoka na angemjulisha wakati ambapo angepatikana tena. Ile anageuka kutaka kuondoka, akakuta wanaume wawili wenye miili mikubwa wakiwa wamesimama mbele yake. Aliwatambua haraka, nao walikuwa ni mabaunsa waliofanyia kazi hapo. Walikuwa kama wanamzibia njia asipite, lakini akapiga hatua kwa ujasiri ili awapite, na wao wakamzibia hata zaidi.
Mmoja akamshika begani ili kumlazimisha aende upande aliotaka yeye, lakini Killmonger akaushika mkono wake na kuubana kwa mtindo uliomuumiza baunsa huyo. Ndipo yule baunsa mwingine akatoa bastola kiunoni na kumnyooshea Killmonger, naye Bosco akaanza kumwomba asimdhuru na kumsihi jamaa aende walipotaka. Akamsihi Killmonger amwachie mkono baunsa yule, naye akauachia.
Yule dada mwembamba akampita Killmonger na kutangulia mbele yake, hivyo jamaa akaanza kumfata akisindikizwa na mabaunsa kwa nyuma. Hakutaka hata kidogo kwenda kwa "Queen" huyo, lakini hali ikamlazimu. Walifika kwenye chumba fulani na kuingia ndani humo. Killmonger akawa anaangalia mazingira ya humo na kuona kwa kiasi fulani yalipendeza; kumfaa mwanamke. Mbele yake alikuwa amesimama mwanamke yule mzungu huku ameshikilia glasi yenye wine mkononi. Akamgeukia Killmonger na kuachia tabasamu hafifu huku akimtazama kwa madaha.
"Unataka nini?" Killmonger akamuuliza.
Mwanamke huyo, Queen, akawafanyia kwa ishara mabaunsa wake kuwa waondoke, nao wakatii na kutoka, wakiwaacha Killmonger na Queen mzungu peke yao.
"Same thing as always (jambo lile lile kama sikuzote)," Queen akasema.
"Not interested (sina haja nalo)," akajibu Killmonger kwa uthabiti.
"Do not be such a sour puss. Unaweza kupata pesa nyingi zaidi. Take my offer," Queen akasisitiza.
"First off, huwa sifanyi hii kitu kwa sababu ya pesa, nimeshakwambia karibia mara 126. Pili, nahitaji kuondoka sasa hivi, kwa hiyo ikiwa ni hayo tu, baadae," Killmonger akasema.
Akageuka na kutaka kuelekea mlangoni, pale alipopigwa na machale ya haraka kuwa kuna hatari nyuma yake. Kutokea upande aliohisi hatari hiyo inatokea, alijipinda kwa kurukia upande mwingine kwa sarakasi na kukwepa kisu kilichomkosa shingo na kupiga mlango kwa nguvu. Alipomwangalia Queen hiyo, alikuwa anatabasamu kwa upendezi mwingi kumwelekea jamaa.
"That's what I like about you. You're so fast (hicho ndiyo nachokipenda kutoka kwako. Una kasi sana)," Queen akamsifia.
Killmonger akajinyanyua huku akiwa ameudhika. Kisha Queen akamfata aliposimama akitembea kwa maringo. Alipomkaribia, akaweka kiganja chake usoni kwa jamaa akitembeza vidole vyake kwenye 'mask' yake, kisha akashika nywele yake moja na kuichezea-chezea kwa vidole.
"Hii ndiyo itakuwa offer yangu ya mwisho. Usikae kupoteza kipaji chako huku chini wakati kuna sehemu za juu zaidi unaweza kukitumia na kufanikiwa zaidi," Queen akamshawishi.
Killmonger akamsogelea usoni zaidi na kunong'oneza, "Sitaki."
Queen alionekana kuudhika sana. Killmonger akageuka kwa mara nyingine ili aondoke, lakini mzungu huyu akataka kumpiga teke mguuni kwa hasira. Killmonger kwa ujuzi wake tayari alijua Queen angekuja vipi bila hata kumwangalia. Akamkepa, na hili likafanya Queen ateleze kidogo kutokana na kiatu chake kirefu, hivyo Killmonger akamwahi kwa ustadi na kukishika kiuno chake ili asidondoke chini. Kisha akamvuta na kuubana mwili wa bibie kwenye wake; nyuso zao zikiwa karibu sana sasa.
"Easy..." Killmonger akasema kumtuliza.
Tokea Killmonger alipojipatia umaarufu kwenye mtandao huo, Queen alikuwa akijaribu sana kumshawishi ajiunge naye, yaani amdhamini ili aweze kumtumia katika mashindano yenye kufanana na hili, nje ya nchi. Alikuwa akimwambia mara kwa mara kwamba angepata pesa nyingi zaidi huko kwa kuwa alikuwa mwenye ufundi sana, lakini sikuzote Killmonger alimwambia hakutaka jambo hilo hata kidogo. Kihalisi, mwanamke huyu alikuwa mwenye uzoefu sana na mambo haya, na hata mchezo huu kuendeshwa kisiri nchini kulichangiwa hasa na yeye; yaani katika waanzilishi, yeye pia alikuwemo. Alijua ikiwa Killmonger angekubaliana na ofa yake angepata faida nyingi, lakini jitihada zote za kumshawishi jamaa ziligonga mwamba kwa kuwa Killmonger hakulegeza msimamo.
Queen akawa anamwangalia sana jamaa mdomoni na machoni alipokuwa ameendelea kumshikilia vile, naye Killmonger akatabasamu kimajivuno kumwelekea. Kisha kwa makusudi, jamaa akalamba shavu la bibie na kumfanya ashtuke, kisha akacheka na kumwachia. Queen alijifuta shavu lake huku anamwangalia Killmonger kwa kutomwelewa, na hapo mwanaume akatoka na kuondoka zake akimwacha Queen anashangaa.
★★★
Ni nyumbani kwa wazazi wake Dylan, na sasa yapata saa 6 na dakika kadhaa usiku. Gilbert ameketi sebuleni pakiwa na giza kiasi, akionekana kuzama kwenye fikra za mambo fulani. Nyumba yake ilikuwa kubwa na pana sana kwenye eneo lililokuwa limejitenga na nyumba zingine. Ilikuwa na ghorofa moja refu na pana kuzunguka umoja wa nyumba yote. Vyumba vyake vilikuwa vingi, na vitu kwenye nyumba hii vilikuwa vya gharama na vya kisasa.
Mlango wa kuingilia ndani hapo unafunguliwa, kisha anapita kijana fulani na kuufunga. Anaanza kuelekea sebuleni lakini upande wa ngazi ili apande kuelekea juu.
"Dylan..." Gilbert anaita kutokea hapo alipo.
Kijana huyu ni Dylan. Naye amekuwa mtu mzima sasa mwenye mwonekano wenye kuvutia wanawake wengi (na hata wanaume mashosti). Anasimama baada ya kuwa amemsikia baba yake anamwita, naye anatazama upande huo alioketi. Baba yake ananyanyuka na kuanza kumfata polepole. Dylan anaangalia pembeni akiwa ameweka uso wenye kuudhika kiasi.
"Ulikuwa wapi?" baba yake akamuuliza.
"Misele," akamjibu kimkato.
Gilbert akasbusha pumzi na kuangalia pembeni.
"Umefikiria kuhusu tulichoongea?" akamuuliza.
"Hapana."
"Dylan...najua mambo mengi kati yetu hayajakaa sawa lakini...tujaribu kuyaweka pembeni yetu kwanza. Wewe ndiyo nguvu yangu Dylan. Ninajua kwa pamoja tunaweza kupata ushindi. Tafadhali..." Gilbert akamwomba kwa sauti ya upole.
Dylan akamwangalia kifupi, kisha akapanda ngazi kuelekea juu kwenye chumba chake. Baada kuufunga mlango, akatikisa kichwa chake akiwa amefumba macho kwa kusikitika, kisha akaingia kwenye bafu la humo na kujimwagia maji. Gilbert alibaki kule chini akiwa na huzuni sana. Uhusiano wake pamoja na mwanae ulikuwa umebadilika mno, na haikuonekana kama mambo yangerekebika hivi karibuni.
Dylan alikuwa amerudi kutokea Brazil miezi michache iliyopita baada ya kumaliza chuo kikuu kule. Alikuwa amesomea masuala ya Civil Engineering na kupata tuzo ya juu ya kuhitimu. Kule, aliishi na shangazi yake yule mdogo kwa miaka mingi, na alizoea maisha ya kule na kupata marafiki wengi. Watu wengi waliofahamu jinsi alivyokuwa na akili nyingi walimshawishi afatilie miradi mikubwa ambayo ingemwingizia pesa nyingi sana, lakini yeye akaamua kurudi nyumbani ambako hakuwa amekanyaga muda mrefu.
Kwa sababu nyingi sana za mambo yaliyoendelea miaka mingi ambayo alikuwa kule, zilifanya uhusiano wake mzuri aliokuwa nao na baba yake ushuke sana kwa kiwango kikubwa. Hawakuongea tena kama zamani, Dylan angefanya mambo yake tu, hata kama angeambiwa hivi na vile na baba yake angepuuzia, yaani kiufupi hawakupatana vizuri tena. Gilbert alijua vizuri kuwa Dylan ana uwezo mkubwa wa kusaidia kampuni yao ipambane na vikwazo vilivyokuwepo na kuvishinda, lakini bado kijana huyu hakutaka kujihusisha na kampuni hii.
Wakati huu alikuwa anajenga mgahawa wa kisasa kwa ajili ya kupata watu ambao angewapatia milo mingi tofauti-tofauti, kwa kuwa alipenda sana masuala ya misosi. Mama yake alikuwa amepinga sana wazo hilo, akisema anapaswa kufanyia kazi kile tu alichosomea, lakini Dylan aliendelea na mpango wake huo ambao kwake aliona ungempa furaha.
Miaka kadhaa aliyokuwa Brazil, alifanya kazi sehemu nyingi za vyakula, hivyo pesa aliyojitunzia ndiyo ambayo alitumia kujenga mgahawa huu mpya. Ijapokuwa angeweza kutumia pesa za familia, hakutaka kufanya hivyo. Alikuwa mtu mwenye kujiamini kama alivyokuwa wakati yuko mdogo, na alionyesha wazi kwamba alitumaini kwa uhakika kuwa wazo lake lingemletea faida kubwa.
Ilipofika asubuhi, kama kawaida wazazi wake walielekea kwenye kampuni yao. Leo ndiyo ilikuwa siku ambayo mkutano na viongozi mbalimbali ungefanywa kuanzia mida ya saa 3 asubuhi. Gilbert alijiandaa vyema ili kuwapa maelezo ya kuwahakikishia alikuwa na suluhisho la tatizo lililoiandama kampuni hii. Mkutano ulianza, naye Gilbert akatoa hotuba yake yenye kuchochea fikra sana. Aliwaonyesha maeneo mbalimbali ambayo wangeweza kufanya maendeleo zaidi ili kuiinua kampuni yao juu zaidi.
Baadhi ya washiriki wengi waliongelea shida zilizokuwa zinaikabili kampuni hii na kuuliza maswali mengi ambayo yalimzidi nguvu Gilbert kwa kadiri fulani. Jaquelin alikuwepo pia, naye alijitahidi kusaidia upande wa Gilbert, ijapokuwa lawama hazikuacha kuongezwa. Hata mmoja wa washiriki hao wa hii kampuni akapendekeza kubadili uongozi wa kampuni hii, kwa kuwa kulikuwa na viongozi hapo waliokuwa na mapato/hisa kubwa zaidi ya kuweza kuchukua madaraka.
Gilbert akaendelea kuongea, "...na ndiyo bila shaka tunaelewa kuwa hali inazidi kuwa tete. Lakini ikiwa wazo langu lingefanyiwa kazi mapema, tusingeface..."
"Haipatani na akili kufikiri kwamba teknolojia inaweza kusaidia masuala ya construction. Sisi tunadili na mambo physically. Hicho unachojaribu kusema hakitafanya kazi kwa upande wetu, kila mtu anajua hilo," mshiriki mmoja aliyeitwa Mr. Bernard akamkatisha.
Wengi wakatikisa kichwa kukubaliana nae. Ilionekana kama Gilbert alikuwa ameanza kupoteza mwelekeo kwao, na ijapokuwa alikuwa raisi wa kampuni, bado nguvu ya viongozi wengi hapo ilikuwa kubwa. Jaquelin akamwangalia kwa wasiwasi baada ya kuona anahangaika kutafuta kitu kingine cha kuweza kuwaambia ili awashawishi.
"Kilichopo hapa, ni kugawanya shares za juu za kampuni ili kuanza kufanya kazi collectively," akasema Mr. Bernard.
"Kwa nini unasisitizia jambo hilo sana Mr. Bernard?" Jaquelin akamuuliza.
"Kwa sababu ndiyo njia pekee iliyopo ya kuweza kuinua tena kampuni hii. Kazi zinazoendeshwa kwa njia mbovu hapa ni kwa sababu tumeshindwa kuchukua hatua za jambo hilo mapema, siyo masuala ya technology," akasema Mr Bernard.
"Hapana. Ni kwa sababu experienced workforce kubwa hapa ni ya watu ambao umri wao umesonga."
Wote waligeukia upande ambao sauti hiyo ilitokea. Jaquelin aliachia tabasamu la furaha, huku Gilbert akibaki kupigwa na butwaa baada ya kumwona Dylan akiwa amesimama mlangoni hapo.
★★★★★★★★★★
ITAENDELEA