Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

Swali tu...commercial break...

Hivi kila kipindi cha TV au redio au anything that goes public ni sharti kwamba kielimishe jamii? Seriously?

Na hizo educative programmes zina viewer base kubwa kiasi gani compared to the others?

Kwa hiyo kwenye public TV kunaweza kuonyeshwa ujinga wowote ule ilimradi una watazamaji wengi? Comrade, are you out of your mind or something else ails you? Suffering from DENGUE FEVER? Please seek medical attention promptly.
 
mtoa mada tupo pamoja hata nmechukizwa sana naamini hajat FaizaFoxy atasaidia kwenye kupaza sauti kwenye hili... na kaka yangu kahtaan tutaungana ktk hili
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo kwenye public TV kunaweza kuonyeshwa ujinga wowote ule ilimradi una watazamaji wengi? Comrade, are you out of your mind or something else ails you? Suffering from DENGUE FEVER? Please seek medical attention promptly.

Hawa ndo wale wa akili za "wengi wape".Yani kwa kuwa wengi wanapenda kitu flani basi kitu hiko ni sahihi!Hajui kama kila jamii ina utamaduni na ustaarabu wake.Utamaduni wetu sisi watanzania pamoja na mambo mengine,ni kuwaheshimu na kuwathamini wazee wetu.

Ni kwa sababu tunawaheshimu ndomana tunakemea wao kudhalilishwa na kushushwa thamani yao.Jamii ni muhimu ikaheshimu principles zake na ni matumaini ya wastaarabu wote kuwa mamlaka zinazohusika zitachukua hatua madhubuti ili kulinda utamaduni wetu kuhusiana na wazee.
 
Mimi sio mtazamaji mzuri wa Clouds TV kwa kuwa vipindi vyake vingi ni vya ovyo--havina mvuto wala mafundisho ya maana. Jana, kwa bahati mbaya, nilitazama kipindi cha 'BIBI BOMBA' kinachorushwa na TV hiyo. Nimehudhunishwa sana kuona jinsi bibi na mama zetu wanavyodhalilishwa hadharani. Bibi zetu huulizwa maswali ya kidhalilishaji.

Bibi mmoja aliulizwa kama aliwahi kula mboga inayoitwa 'Biology', akajibu 'ndiyo'. Hili ni swali linalohusu ufahamu na kwa wabibi wale ambao hawakwenda shule, hawajui biology ni nini. Si hivyo tu, hata wale walioishia la saba hawajui biology ni kitu gani. Kuwauliza mabibi swali kama hili ni kuwadhalilisha kitaaluma kwa kuwa tu hawakwenda shule.

Bibi mwingine aliombwa amtongoze kijana yule anayewauliza maswali hadi amkubali. Bibi akatekeleza agizo hilo laivu mbele ya skrini ya TV! Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.

Wizara ya jinsia inapaswa kukataza udhalilishaji huu wa kijinsia. Nasi wananchi tuache kushabikia upumbavu huu--tukatae kuwapigia kura bibi wanaoshiriki.

Wakulaumiwa ni hao mabibi na watoto au wajukuu zao waliowaruhusu kujiingiza katika huo ujinga.
 
Si ndio hawa hawa clouds ndio walikua wadhamini wa KANGA MOKO NDEMBENDEMBE??? Wanadharirisha sana Mama zetu...
 
Hawa mabibi nao wamedata sipati picha kwenye usichana wao walikuaje, hauwezi kumkuta bibi anaejiheshimu akubali kushiriki huu upuuzi.
 
Inabid ipigwe ban .

Sio mantiki ya kipindi hicho

Wanawafundisha uhuni wa kusema maneno kama nigga.

Mkuu hawa watu ni limbukeni.
Kulegeza suruali na kuwaiga wazungu weusi wanaona ndio maendeleo..
Na sio hao tu.

Kiko kile kipindi cha yule sijui Sister nani vile kwenye SALOON ANAVAA KAMA DUME na kuongea kwake kwa kutupatupa mikono KAMA wale WASAGAJI wa kimarekani.

Yule binti ANAJIFANYA DUME wakati kazaliwa MWANAMKE!

Hivi hana wazazi yule?
 
Unaweza kukukuta watoto wao na wajukuu zao wanafurahia kweli huu upuuzi.
 
ukimwi ni kitu cha kawaida sana mshikaji anakula arv mbona hata watu kibao wanao halafu mbona umeshtuka utadhani umetiwa kidole

Nimeogopa,nitabaki njia kuu daima,inshallah na mwenzagu nae abaki nja kuu,Babuu anaonekana bomba
 
Wakulaumiwa ni hao mabibi na watoto au wajukuu zao waliowaruhusu kujiingiza katika huo ujinga.

When there is market failure, a call for government intervention is justifiable. I doubt whether terms of references of this program is clear and well understood by parties. Should be banned
 
Hii tv bado hawana vipindi vya maana na si wao tu hata radio...kidogo ktk tv ni kile cha sports ...wameegemea zaidi ktk matangazo kuliko kupasha habari!!
 
Mkuu, unaweza kutuambia kipindi cha BIBI BOMBA kina manufaa gani kwa jamii au kinatoa mafundisho gani kwa watanzania? Kwa hivyo kama sio kila kipindi kinapaswa kuelimisha jamii kwanini video za ngono hazionyeshwi kwenye TV? Usitetee ujinga kwa maneno makavu bila kuujengea hoja huo ujinga unaoutetea. Acha kufikiri kwa kutumia tumbo, tumia kichwa.

Kwa hiyo kwenye public TV kunaweza kuonyeshwa ujinga wowote ule ilimradi una watazamaji wengi? Comrade, are you out of your mind or something else ails you? Suffering from DENGUE FEVER? Please seek medical attention promptly.

Hawa ndo wale wa akili za "wengi wape".Yani kwa kuwa wengi wanapenda kitu flani basi kitu hiko ni sahihi!Hajui kama kila jamii ina utamaduni na ustaarabu wake.Utamaduni wetu sisi watanzania pamoja na mambo mengine,ni kuwaheshimu na kuwathamini wazee wetu.

Ni kwa sababu tunawaheshimu ndomana tunakemea wao kudhalilishwa na kushushwa thamani yao.Jamii ni muhimu ikaheshimu principles zake na ni matumaini ya wastaarabu wote kuwa mamlaka zinazohusika zitachukua hatua madhubuti ili kulinda utamaduni wetu kuhusiana na wazee.

Hayaa! Mmeniskia nikienda for or against anything hapa? Ni swali nimelitoa, jijibu na uchambue mwenyewe kwamba kwanini kipindi kipo hewani na kinaonesha walakini. Kama una shida sana kawaulize clouds.

Halafu haya makitu ya kutoa irrelevant examples?! Its known kwamba pornography na nudity are directly and explicitly illegal kwenye mass communication (sijui ndo mnavoiita). Kipindi kipo hewani kwa sababu hakijavunja sheria husika. Thats what happens mnapotaka kila kitu kitawaliwe na sheria.

N.B: I am not for or against anything here. Na kabla vidole vyako havijapandisha ashki, husisha kichwa.
 
Kwa hiyo kwenye public TV
kunaweza kuonyeshwa ujinga wowote ule ilimradi una watazamaji wengi?
Comrade, are you out of your mind or something else ails you? Suffering
from DENGUE FEVER? Please seek medical attention promptly.

Si lazima kila kinachorushwa na TV yoyote kielimishe, kuna content nyingine huwa zinakuwa intended kuchekesha without necesarily educating the viewers bali kuburudisha.
Tatizo la clouds TV ni kukosa creativity kwa upande wa kubuni kitu kinachochekesha. Inawezekana hawana vyanzo vizuri vya ideas au wanawategemea watu fulani pekee ambao wana mawazo mgando, wasio na taaluma(makanjanja), wako out of touch na jamii ya Mtanzania wa kawaida, hawana sense of humour bali wana sense of dark humour katika kubuni vichekesho na matokeo yake wanakuja na vichekesho visivyochekesha bali vyenye kudhalilisha kama si kuudhi.
 
Back
Top Bottom