Clouds management team ni wapuuzi sana kuruhusu kipindi kama hiki.Sizungumzii
TCRA kwa kuwa najua hawana ubavu wa kuipa ban radio/tv inayotumiwa kufanya kampeni ya nguvu kuwarudisha vijana kwenye chama chao.
Ni kama vile kipindi cha kumtafuta bibi anayevuta bangi sana au aliyechetuka akili kwa sababu ili bibi ayajue maujinga yale yaliyopewa jina la maswali,lazima awe msela mvuta bangi na mwenye akili zilizochetuka.
Idea yao eti ni kumtafuta bibi anayeenda na wakati na anayeweza kujua mambo ya vijana wahuni,wavuta bangi na waliokosa malezi mazuri.Sasa hii ni idea au kadhia?
Hawa jamaa huwa wanajifanya wenyewe wanaweza kila kitu kisa wameiweka mfukoni serikali ya "mshkaj" wao ambaye aliwahi kuwapigia promo dhidi ya redio zingine.
Kuna v2 vingi vya kupima IQ za mabibi hao lakini wenyewe "akina mzee wa king'oko" wamestick kwenye ile "bibi msela ndo mwenye akili"!Yani wanamuona bibi wa mfano ni bibi cheka kwa hiyo wanatamani mabibi wote wawe kama yeye!
Wanawadhalilisha hawa viumbe ambao jamii inapaswa ifaidike na uzoefu wao wa maisha.Badala ya kuwatumia hawa akina bibi kuipa jamii faida wao wanawatumia kuiathiri hasi jamii na kuleta utamaduni mwingine wa ajabu na kudhamiria kwa ari,nguvu na kasi zaidi kuupromote na kumpata mshindi atakayefiti kwenye hiyo definition yao ya "bibi bomba".
Msemaji wa clouds huku kwenye jf yule jamaa anayeishi ng'ambo na mwenye kupenda kuandika kiinglishi kuonesha mkwara mpaka sasa sijaona majibu yake.Kama kayatoa ni kwa kupitia ID nyingine sio ile ya kawaida.Huenda hata yeye kwa hili anashindwa atetee vp ingawa siamini sana kwa sababu jamaa ameshatetea vingi vya ajabu vya hawa wapuuzi.