Laila, jini aliyenifundisha mapenzi nikiwa shule

Lior

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
766
1,957
Baada ya kushindikana kwenye shule moja ya jeshi iliyo mkoani. Brother akanipa second chance nikahamia shule moja binafsi mjini Dar. Nililazimika kurudia form 3 maana mwaka uliopita nilisoma miezi minne tu, na sikufanya mitihani ya mwisho. Kama mjuavyo akija mwanafunzi mgeni darasani watu wanakuwa attention kuona kama anajiweza au kilaza.

Baada ya siku 2 nikapata mwenyeji akanipa daftari zake ni copy notes, na akanisaidia baadhi ya nyingine kwa kuwa nilihamia hapo mwezi wa 3 wameshapiga hatua. Huyu mwenyeji wangu ndie hasa chanzo cha hekaheka. Alikuwa na dada yake wote wako darasa moja.

Huyu rafiki yangu (nitamuita Laila ) na dada yake (nitamuita Anabia) walikuwa ni waarabu. Laila alikuwa na mahusiano na jamaa mmoja (nitamuita Ivan.)(huyu Ivan nikimwelezea wengi watamjua maani ni maarufu yuko acapella group flani hivi maarufu.) kutokana na ugeni wangu sikuwa najua huo uhusiano, lakini kumbe ulikuwa unajulikana shule nzima. Laila alikuwa ni aina ya wadada mapepe, akiona mwanaume mgeni lazima ajilete ila dada yale alikuwa mpole sana.

Darasa letu tulikuwa mchanganyiko (mchepuo wa sayansi na biashara) kwa kuwa madarasa yalikuwa machache na wanafunzi wa hizo combination walikuwa wachache sana. Mwezi wa 4 tukapewa test ya geography, mtu wa kwanza nikawa mimi (nilikuwa nafanya marudio ya darasa) nikapata maksi 98% with well illustrations, aliefatia kapata 56% so mwalimu akasema 'Cotterpin ametengeneza marking scheme, kila mtu afanye correction kutumia hiyo paper yake.'

Nikapata marafiki wengi zaidi, hasa wadada tuliokuwa nao combination moja. Nilikua mzuri sana kwenye masomo ya biashara. Mpaka nahamia hapo niilishamaliza topics zote muhumu za BK na CM……

Baada ya miezi 6 nikaanza kupata changamoto pale shule, washkaji wakaanza kunitenga kimtindo, ukikuta wanaongea wakikuona tu wanabadili maongezi au wananyamaza. Baadae nikaambiwa sababu ni mimi kuchukua demu wa Ivan. Baada ya kujua chanzo nikamtafuta Laila na kumuuliza, akanizunga. Kumbe yeye alikuwa anawasimulia mabinti wenzake kuwa natoka nae na nina hela sana, kumbe uongo.

One day nikaamua liwalo na liwe, nikamtania tukitola shule twende nyumbani, akakubali. Sikuwa na shaka maana sikuwa nakaa mbali na shule, na pia nakaa na kaka yangu pekee amabe kurudi kwake home ni mida ya saa 3 usiku na kuendelea. Jioni tulipotawanyika, nikaondoka bila kumcheki tena Laila. Kumbe nae amempanga dada mmoja mnyakyusa nitamuita Irene, amsindikize.

Nikiwa njiani nikawaona wananifata nyuma ila hawataki kunikaribia, nikajua hawataki wanafunzi wengine wajue. Nikafika home, dakika 5 mbali wakagonga geti, kufungua niwao, nikawakaribisha ndani. Tumezuga pale kama dakika 5 hivi, nikawaacha wanaangalia Tv nikaingia chumbani, mara nasikia mlango unagongwa. Kufungua namkuta Laila, akaingia huku anajichekesha, Irene akabaki sebuleni.

Basi akanipa kadi na maua kama zawadi, akaomba kuondoka. Alikuwa ananukia sana udi na marashi flani mazuri sana,(mpaka wakati huu sikuwa nimemtongoza wala kuonyesha namtaka, ila yeye alikuwa anaonyesha wazi kabisa). Nikawaza kwa nini nisile hili apple limejileta lenyewe room kwangu, badae nikasema ataniona nina papara, acha nimtese kwanza, wakaaga wakaondoka.

Jumatatu iliyofata tukawa tumewapisha watu wa sayansi darasa, kipindi chetu mwalimu hakuwepo so tukaambiwa tukakae kwenye ukumbi flani hapo shule. Irene akaanza kunitania

Irene: nilizani mjanja kumbe ndio wale wale

Cotterpin: kwa nini

Irene: Ijumaa demu kaja mpaka room kwako lakini ukamuogopa.

Cotterpin: We ulijuaje nimemuogopa, labda nilimla.

Irene: Mimi ndie nilimwambia akufate chumbani na zile zawadi, akaniambia ulipokea lakini hukuomba hata denda wala kumshika.

Basi mpaka hapo nikaanza kuona hatari ya kuharibiwa jina pale shule, maana wameanza kunisema naogopa wasichana.

Cotterpin: Siku ile nilikuwa naumwa kichwa, ila naomba uje nae Ijumaa, nitaomba get pass mapema tu so na nyie tafuteni namna ya kutoroka.

Irene: Hilo jambo dogo sana, ila ukimuogopa tena nitakudharau.

Basi ijumaa ilipofika saa 6 mchana, nikamfata mwalimu wa zamu nikajifanya naumwa sana, akanipa get pass (Bila get pass hupiti getini kabla ya muda unaotakiwa). Nikaondoka, Laila akatoka kwa kibali cha kwenda msikitini na Irene nae akaungana nao, (ijumaa wanaruhusiwa mapema kwenda kuswali).

Saa 7 wote tukawa sebuleni tunaangalia Tv na kunywa juice baridi. Sikuwa na hofu wala haraka, maana najua muda wa wanafunzi kutoka ni saa 10 na Kaka kurudi ni usiku. Nika weka movie inaitwa Troy (kuna prince alitorosha malkia wa nchi jirani akampeleka kwao.) Haukupita muda Laila akaomba abadili nguo (alikuwa anavaa hijabu juu ya uniforms akiwa nje ya mazingira ya shule) akazama room.

Irene akaniangalia sana, akacheka, nikaelewa namaanisha nini. Nikaingia room nikamkuta Laila amevua hijabu, kabaki na sketi ya shule kakaa kitandani. Nikamsogelea, nikamuinua na kumkumbatia, akatoa ushirikiano vizuri tu. Nikamjaribu denda akapokea. Basi tumechezeana sana ulipofika wakati wa kula apple akagoma

Laila: Cotterpin naomba isiwe leo, nitachelewa nyumbani, halafu sitaki Irene ajue.

Cotterpin: Yaani mpaka hapa uko hoi, acha tumalizie hautachelewa kuondoka. Kuhusu Irene mpaka hapa anajua kinachoendelea.

Laila: Sitaki asikie nikilia, halafu najua tutachelewa sana maana mimi nina bikra, mpaka ufanikiwe tutachua muda sana.

Kwa ujinga wangu nikakubaliana nae, tukapiga story na kuchezeana sana bila kumalizia tukio. Ikawa sasa ni kawaida yake, anakuja peke yake tunapeana denda, story ila apple anasema anaogopa tusubiri kwanza. Kutokana na umri na uzuri wake sikuona shida kufanya anavyotaka. Tulifanya huo ujinga mwezi mzima.

Kipindi hicho chote Laila alikuwa habanduki nyumbani, naweza muacha shule ila nikifika home dakika 5 nyingi geti linagongwa, nikifungua ni yeye. Aliniambia mama yake anafanya kazi bekari mmoja ya wahindi mjini, so akawa ananiletea zawadi nyingi sana za vyakula(keki, biscuits nk) na juices. Pia akawa ananipa sana hela na kuniiletea marashi ya bei mbaya sana.

Siku moja Irene akamsnich mwenzake, akaniambia anatembea na mahindi fulani alikuwa na internet cafe pale magomeni mapipa, ndie anampa hela anazonihonga mimi. Basi nikaona huyu ananizarau na kunidanganya kuwa bikra, kumbe ni malaya. Nikamuomba jioni aje home, kama kawaida yake huwa hakatai kuja. Alipofika nikamwambia achague moja, anipe apple lake au tuachane kabisa maana story zake ninazo. Nakumbuka alilia sana, akaniambia

Laila: Nakupenda sana Cotterpin, lakini kuna kitu kinanifanya nisikupe apple langu, japo toka siku ya kwanza nilitamani kukupa.

Cotterpin: Kitu gani hicho? Wewe unanidanganya naonekana mjinga kwa rafiki zako.

Laila: Cotterpin nisamehe, nilikudanganya, ila naomba ukijua ukweli usiniache, ukinidanganya na ukaniacha najiua.

Cotterpin: we sema tu hakuna kosa halisameheki.

Laila: Nakupa apple langu leo, utajua nilichokudanganya. Ila niahidi hutaniacha.

Cotterpin: Nakuahidi

Basi nikapewa apple, akilini nawaza namna ya kufanya timing ya kutoa seal 🤣 nikachezea akawa tayari. Ile napeleka kiuoga uoga, nashangaa napokelewa na bwawa fulani sigusi kingo. Nikakaza moyo nikapiga in out kadhaa lakini sioni dalili ya ugeni wa bibie, ndio kwanza ananikandamiza nizame mzima mzima. Kutokana na hasira ya kudanganywa siku last sana, nikafika bila yeye kupenda, nikatema bungo.

Tukaanza kugombana kwa nini hukuniambia ukweli toka silu ya kwanza na bla bla kibao. Tuli sort out akanipa hela na zawadi akasepa, akanipa ahadi ya kupewa zawadi kubwa kesho yake kwa kumsamehe. Niwe mkweli nilipanga kuachana nae siku hiyo hiyo maana sikupata radha yoyote kwenye apple lake, kifupi yalikuwa makapi tu.

Usiku nikiwa nikaota ameniletea simu nzuri sana, halafu akawa anag'aa kama mbalamwezi. Baada ya kunipa simu na zawadi zingine, akanipa tena apple lake. Kulipokucha sikwenda shule (kaka anaondoka saa 11 kwa hiyo hajui kama naenda shule au laa). Kufika saa 2 geti likagongwa, nikafungua nikamkuta Laila, amevaa kama nilivyomuona ndotoni, uzuri wake umeongezeka sana.

Nikamkaribisha ndani, akatoa vitu alivyobeba. Akanipa simu nzuri sana ya Nokia kama ya ndotoni, baada muda akanipa apple lake hapo hapo sebuleni, surprisingly apple lilikuwa tight kiasi, na radha yake itawa tamu sana sio kama jana yake. Nikabaki nashangaa unakuwaje awe na mabadiliko hayo kwa haraka vile, basi alinifanyia vitu na styles za ajabu ajabu sana mpaka nikachoka ila yeye hachoki. Nikamwambia tupumzike, akanijibu jana uliniumiiza moyo wangu kuniambia sina jipya na wala sina utamu wowote, leo nataka ujue kuwa sikupenda, wewe lala tu niachie hi kazi. Basi Laila akageuka mpeleka moto mimi nimelala chali anajipimia.

Nakumbuka baada ya kumalizana nae nilioshiwa nguvu, nikawa natembea kama mlevi, nikanywa lita nzima ya maziwa fresh😃 kama vile nilihisi nimepewa sumu. Baada ya dakika 5 nikatapika sana, nikaenda kuoga nikalala. Nililala tola saa saba mpaka saa 11 ndio nashtuka nakuta mwili una nguvu kiasi ila kichwa kinagonga sana.

Baada ya hapo tukawa kama mke na mume kuanzia shule mpaka home. Apple linaliwa kila siku tukujisikia. Akawa anaonyesha mapenzi na wivu hadharani bila kujali walimu wala wanafunzi. Home kaka alijua maana kuna siku hakwenda kazini, Laila akaja kama kawaida yake (hakuwa akitoa taarifa ya kuja), akamkuta kaka, nae ni mzungu tu, akamwambia nimeenda sokoni anisubiri sitakawia. Pale home tulikuwa na vyumba viwili na sebule, kaka akamwambia akaribie tu room kwangu (nilikuwa naenda na rafiki zangu kufanya group discussion pale room kwangu). Maana alimwambia kuna maswali amekuja nimsaidie.
*****

Baada ya miezi mitatu ya penzi zito, shule ikaandaa study tour kwenda Bagamoyo. Mimi binafsi sikutaka kwenda, nikajifanya sina hela ya kulipa, kumbe sikutaka kumuacha jamaa yangu mmoja alikuwa mwanangu sana na alikuwa kwao hawako njema kiuchumi. Nikawa msaada mkubwa kwake kuanzia chai asubuhu, chakula mchana na jioni, sometimes vinauli vya hapa na pale alikua anakaa sinza. Laila alinilipia mimi na huyo jamaa yangu, japo sikuwa nimemwambia kabla, nikamuulza amejuaje kama nilitamani kumlipa yule rafiki yangu, akaniambia ' ukimpenda sana mtu, utaweza kumsoma mawazo yake' (hapa sikumuelewa kabisa ila nikala pini tu)

Study tour Bagamoyo.

Siku ya safari kulikuwa na coster 2. Nikakaa na rafiki yangu coster ya kwanza, Laila akajikuta costa ya 2 siti moja na Ivan. (Hii tuliichezesha tu ili nisiwe nae gari moja).

Tumefika bagamoyo, tukaanza tembezwa. Tulipofika kaburi la 'wapendanao' nikiwa na mwanangu, watu wakapiga picha. Kawaida yetu tulikuwa watu wa nyuma nyuma tu, so wengine walipoondoka tukabaki nyuma tunapiga picha na rafiki yangu, ghfla Laila huyu hapa anataka picha. Alikuwa ameshaondoka na wenzake wako mbali, ila mara tu tunuona karibu yetu anaomba picha.

Kwenye kundi letu tuliluwa na dereva wa gari yetu, alikuwa ananuka pombe, hiyo hali ukamfanya Laila awe mbali na sisi japo kila mara alikuwa ananiangalia sana namchunia.

Mida ya chakula akamuita yule rafiki yangu, akamwambia tusiende kula hotelini, ametuletea chakula. Mimi nikamwambia mwanangu twende tu bila kumuaga. Tukafika wa mwisho kule hotelini (baadhi walibeba vyakula vyao hawakwenda), tukakosa chakula. Nikamwambia mwanangu twende dukani tuchukue soda na keki tukalae beach tule, tukaenda madukani cha ajabu hatukupa soda wala keki😂 hapa wanasema hawana chenji kabisa, wengine wahana soda wala keki. Tukaona sio kesi, twende zetu baharini tukale upepo, chakula tutakula tukirudu dar.

Tukiwa njiani tukakutana na Laila akatucheka kwa kukosa chakula. Akasema tutangulie beach anafata begi lake anakuja. Mara akaja na mfuko una soda, keki na chips mayai na kuku. Tukala tukiwa watatu kwenye kundi letu, (kulikuwa na vikundi vikundi kulingana na urafiki wao). Laila akaomba tukaogelee sisi tukakataa kabisa, rafiki yangu anaogopa sana , mimi siogopi maji ila sijui kuogelea, kwa nini nipate aibu mbele ya vidada vya Dar vimezoea kukata mawimbi.

Muda wa kuondoka kila mmoja akae gari alilokuja nalo, Laila kumbe ameshafanya yake tuko wote gari moja tena nyuma ya siti yangu. Njiani akaanza nichokoza anajificha, basi tukafika shuleni saa 11: 30 nikapewa mfuko mkubwa umejaa biscuits na keki, karanga, soda za kopo nk, nikaeda home na yule mwanangu.

******
 
Laila akaanza kuwa mtu wa ajabu sana, tukigombana haondoki mpaka nimsamehe, na ili ajue nimemsamehe lazima nile apple lake, bila hivyo haondoki hapo nyumbani. (hiyo hali ikanifanya niwe mtumwa kwakwe, maana ili kaka asikute ugonvi lazima nimsamehe na kula apple lale).


Kuna siku tumegombana, nikajifanya mbabe na sitaki msamaha, akaenda washroom akajichanja na viwembe mikononi akakaa chini anavuja damu. Baada ya kuona kimya nikamfata nikakuta amelala chini mikono inavuja damu, ikabidi hasira ziyeyuke, nikambembeleza sana, akawa anasema anafanya vile kwa kuwa mimi simpendi wakati yeye anaipenda sana, bora afe tu kuliko kunikosa. Ikabidi nifanye juhudi sana akakubali nikamfunga yale majeraha, akawa amelegea sana kama mgonjwa wa muda mrefu, tukarudi room akataka nile apple ili msamaha ukamilike. Ikabidi nile, kisha akaondoka.

Kesho yake akaja asubuhu kama saa 3 hivi, amechangamka sana, jambo la ajabu hana makovu yoyote yale. Nikamuuliza umekuwaje hana vidonda wala makovu wakati jana yake ndio ametola hapa home ameumia? Laila akasema penzi lako ndio dawa. But how? Wazo likaja potezea. Basi baada ya Laila kuona namsubua na maswali mengi, kuna jambo alifanya kwenye ufahamu wangu.

Nikiwa peke yangu napata mawazo na maswali ya kumuuliza, na napanga kabisa akija nakinukisha, but surprisingly nikiwa nae tu sikumbuki chochote, akiondoka nakumbuka. Huo ukawa mchezo wake na maswali yangu kwake yakaishia hapo.

Kuna kipindi nasikia geti linagongwa ila nikienda kufungua nakutana nae nje ya mlango wa chumba changu, nikiuliza amepitaje getini anasema amekuta liko wazi. Wakati najua kabisa lile geti haijawahi achwa wazi hata siku moja.

Laila akaanza kuwa mbabe kwangu, akawa nani treat kama mume wa ndoa, sina haki kuongea na mwanamke mwingine yoyoye. Akawa ananionya siku akinikuta na mwanamke atanifanya kutu mbaya sana na huyo mwanamke ndio utakuwa mwisho wake. Pamoja na vitisho vyote na ubabe, yule binti hakuacha nipenda, kunipa hela, kifupi kunihudumia, na mimi sikumchukia, nilimpenda zaidi.

Siku moja nilikuwa naenda magomeni usalama, kuna barabara fulani imenyoka unaweza ona mita 50 mbele. Nikiwa natembea mbele yangu naiona morogoro road, hakuna mtu wa gari mbele yangu ila dada mmoja akawa anakuja upande wangu. Mzuri tu, nikamsemesha akasimama. Kumbe ni jirani yetu, basi nikazuga kwa salamu tukaachana, ila kabla ya kuachana nilisikia harufu ya marashi nunayoyajua, huwa ananukia Laila.

Kama baada ya hatua 4 ghafla nikageuka kumwangalia yule dada akawa anaenda tu bila kugeuka, ile nageuka tu shabashi Laila huyu hapa. 😢 Ni kitendo cha sekunde chache sana mita 50 mbele yangu hakuuwa na mtu, kutendo cha kugeuza shingo Laila yuko mbele yangu tena umbali wa mita 10 tu.

Laila: Naona umempenda yule dada, vipi nikufanyie mpango!? Au umechukua namba? (akawa anacheka cheka)

Cotterpin: Sijamtamani tumesalimiana tu ni jirani yangu.

Laila: Mbona umegeuka kumwangalia wowowo. (akaonyesha hasira )

Cotterpin: Ina maana ukigeuka kuangalia nyuma ni lazima uangalie wowowo la mtu!?

Laila: Kumbuka Cotterpin, nakupenda sana, uko moyoni mwangu ndio maana najua mawazo yako. Sitaki kushea penzi langu na kima yoyote, sawa? (akaongea kitemi)

Cotterpin: Usijali sina huo mpango, wewe unanitosha.

Kiukweli lengo la kumsimamisha yule dada ni kumtongoza, niliahirisha baada ya kumtambua ni mke wa jirani yetu. Lakini Laila amejuaje nilikuwa na wazo la kumtongoza yule dada? Hapo natamani kumuuliiza lakini mdomo mzito, na ametokeaje ghafla mbele yangu. Penzi likazidi kukolea sana, lakini mimi furaha na amani vikaanza tupotea kwangu. Nikiwa mbali na Laila namchukia na kutamani kuacha nae, ila nikimuona tu hasira, chuki vinayeyuka kabisa, namuona ni sehemu ya moyo wangu.

Mara kwa mara tulikuwa tunaenda mikadi beach kuogelea, alikuwa anapenda sana maji. Tunatoka kwa taxi magomeni mpaka mikadi, siku za kazi huwa hakuna watu, ni mmoja mmoja tu. Tunaogolea, nakula apple lake mpaka nakinai, lakini yeye kila saa anataka. (alikuwa mtaalam sana wa mapenzi, mwepesi sana, anajua utundu mwingi sana, anajua kukufanya ujione umebahatika sana).
 
Safari ya Arusha.

Mwaka wa mwisho form 4, nilikuwa nimezidiwa na penzi la Laila, nikaanza kuwa mtu wa ajabu ajabu. Niko very cool sitaki story na mtu. Bahati nzuri nilikuwa vizuri kichwani japo sikuwa na muda wa kusoma, muda mwingi ni kula apple la Laila na starehe zingine. Nilikonda sana japo nilikuwa napewa pesa nyingi tu na vyakula kila aina naletewa home. Ila mwili ukagoma.

Kuna siku akaniambia ana mimba yangu, nikaogopa kufukuzwa shule. Nikamuliza tunafanyaje sasa, akanijibu jambo dogo hilo kwake ila nisije achana nae tu. Akaniambia ana rafiki yako sinza, ameongea nae amekubali aende ampeleke kwa Dr. Amtoe mimba. Akataka nimpeleke, kufika sinza kumbe huyo rafiki yake ni mwanaume.

Akampa chumba cha uani ilikuwa jioni, ili kesho yake saa 4 akafanyiwe abortion. Usiku kama saa 2 Laila akaniambia anaenda kuongea na huyo rafiki yake atarudi, nikabaki peke yangu, cha ajabu alirudi saa 4 usiku. Nikamuliza kwa nini amechelewa akasema Ilibidi wakamuone Dr. Usiku huo huo ila rafiki yake hakutaka nijue. Akanipa tena apple lake tukalala.

Kesho yake wakaenda kwa huyo Dr. Mimi nikarudi nyumbani, kufika home nikamkuta kaka. Jambo la ajabu kaka hakuwa sawa, akaninyang'anya simu na kunifungia room kwangu. Mimi nikiwa sielewi kinachoendelea, nikasikia anaongea na simu.

Kaka: Dogo karudi mida hii peke yake

Upande wa piłi: (sikusikia )

Kaka: nimemfungia room simu yake ninayo.

Basi nikawa nimeanza kuhisi sababu ni Laila kutorudi kwao jana. Baada ya dakika 40 nikasikia geti linafunguliwa, halafu wakaja kufungua room yangu. Mimi nimejilaza tu kitandani, kipindi hicho sumu imejaa kifuani, siogopi mtu wala sina hofu na mtu yoyote. Akaingia kaka na kufatiwa na mhindi fulani. Basi akanisalimia,

Mhindi: Cotterpin hujambo

Cotterpin: Sijambo

Mhindi: mke wangu yuko wapi?

Cotterpin: mke wako? Alikwambia anakuja kwangu?

Kaka: Mdogo wangu acha dharau, mjibu vizuri usitafute matatizo.

Mhindi: Wewe unatembea na mke wangu siku nyingi tu nafahamu, mara kadhaa huwa namleta hapa kwa gari langu na akitaka kuondoka hunipigia namfata, jambo moja ambalo sikuwa najua kabla ni aina ya watu wanaokaa nyumba hii, yeye alisema ni rafiki yake wa kike anaishi hapa. .

(mpaka hapo nikawa nimemfahamu ni yule mmiliki wa Internet cafe, na gari jeusi kweli nimeliona likiondoka mara kadhaa ninapomfungulia geti Laila )

Cotterpin: Anaitwa nani?

Mhindi: Laila

Cotterpin: Sikuwahi jua kama ameolewa, na pia kwa nini umeoa mwanafunzi wakati bado yuko shule.?

Mhindi: Mke wangu hasomi, alikwambia anasoma shule?

Cotterpin: Nasoma nae darasa moja, tuko form 4. (Hapa yule Mhindi alitabasamu tu kama vile anajua jambo fulani)

Kaka: Au labda mnaongelea watu wawili tofauti. Maana ninaejua anatembea na huyu mdogo wangu ni binti mdogo tu anasoma nae. Mara nyingi huwa namuona na uniforms za shule hiyo.

Mhindi: ni mke wangu huyo ila hasomi. Yuko wapi sasa hivi?

Cotterpin: (Ghafla nikaanza kusikia marashi ya Laila mule ndani) Yuko sinza.

Kaka: Sasa inabidi twende sinza, tumchukue halafu tutafute ukweli wa hili jambo.

Mhindi: Sawa, ila hakikisha mdogo wako hatukimbii kamba ya kumpata mke wangu.

Kaka: Dogo hili ni jambo dogo, usihofu akimpata mke wake unakuwa huru.

Cotterpin: Sina wazo wala sababu ya kumkimbia mtu. (nikasikia kisi shavuni lakini mtu haonekani).

Tukaingia ndani ya hiyo gari (Toyota balloon) ikiwa gari ya maana sana kipindi hicho. Safari mpaka sinza, kufika tukamkuta Laila kwenye kile chumba tulilala jana yake. Laila hakuonyesha kushtuka hata kidogo, tukaondoka nae mpaka magomeni (home)

Jambo la kushangaza, baada ya yule mhindi kumuona mke wake, akawa mpole sana, maswali hana. Kufika home yule mhindi akaniomba niachane na mke wake basi, mambo ya kujua kama anasoma au laa yakayeyuka vichwani mwetu. Nikasema sawa lakini Laila akaniangalia jicho baya sana, akasonya wakaondoka.

Kaka akanipa nasaha, niachane n yule binti, nipambane na kitambu nifanye paper maana ni mwezi wa 5 huo. Lakini moyo ukaanza kuuma kuachana na Laila, nikaa ndani siku nzima bila amani, usiku Laila akanijia ndotoni, akanionya kuhusu kumuacha, akaniambia anataka kunipeleka sehemu special sana hivyo nisimkasirishe nitajuta. Asubuhi nikamwambia kaka, siwezi muacha huyu binti, bora nife tu. Basi kaka akaniambia nivumilie tu nitazoea hiyo hali, ikabidi aombe ruhusa kazini maana alipata hofu kuniacha pale home peke yangu, alihofu naweza jiua.

Ilipofika saa 6 mchana, nikasikia kaka anaongea na simu. (kumbe Laila amemtoroka tena mhindi) baada ya muda mfupi mhindi akafika nyumbani ameiva. Akanitolea bastola nimwambie mke wake ameenda wapi. Kaka akanitetea kuwa sina simu na sijatoka hapo nyumbani kwa hiyo sijui.

Jamaa akapoa kidogo, ila hakuna mwenye uhakika mwanamke yuko wapi, na je mimi najua au sijui. Basi wakaamua wanipe simu maana lazima yule mwanamke atanitafuta tu. Kidogo Laila akapiga simu, nikapokea huku jamaa wamenisimamia.
 
Aliongea kama mtu anaetuangalia kwenye Tv vile, wakati tuko peke yetu, sijui alijuaje kuna watu wanasubiri ile simu

Laila: Wela loudspeaker niongee na hao watu. (nikaweka)

Akaanza Ashrafu, usirudie tena kumsumbua Cotterpin. Wewe ulinioa kwa kuwahonga wazazi wangu, sikukupenda hata kidogo ila kwa Cotterpin nampenda sana. Ndie nimemchagua awe mume wangu. Wewe ulivunja uaminifu wangu kwako. Nakuonya chochote utakachomfanya cotterpin utakijutia maisha yako yote.

Ashrafu: (akabaki kimya tu )

Kaka: Laila uko wapi? Kwa nini usije tuyamalize haya?

Laila: Wewe unatumika kutaka kunitenganisha na mpenzi wangu, hutaweza. Nakustahi kwa kuwa ni kaka wa mume wangu mtarajiwa, nakuomba usije anzisha vita na mimi, niache niishi na Cotterpin wangu. Mdogo wako ni mali yangu, tena peke yangu kumbuka hilo siku zote.

Wote kimya..

Laila: Cotterpin mume wangu, usiwasikilize hao, hawawezi kututenganisha. Kumbuka kiapo changu kwako ni cha damu. Hakuna mwanadamu anaweza kuitenganisha damu yangu toka kwenye damu yako. Wewe ni mali yangu.

Baada ya maongezi hayo, simu ikakatwa na Laila. Wote tulikuwa na hali mbaya lwa tulichosikia, ila yule mhindi alikuwa na hali mbaya zaidi. Akaishiwa nguvu akaa chini. Baada ya muda mchache akaondoka zake. Kaka hakusema kitu, akatoka kwenda town.
Muda wote tangu mhindi anaingia pale ndani mimi nilikuwa nasikia marashi ya Laila na nahisi uwepo wake.

Baada ya siku mbili, Laila akaniambia nijiandae na safari maana kuna mtu anataka kunidhuru. Basi nikaandaa nguo zangu kimya kimya bila kaka kujua. Kesho yake mchana Laila akanifata akiwa na taxi, tukaondoka kwenda magomeni makuti kulikuwa na guest nzuri, tukalala pale. Asubuhi taxi ikaja tukaenda ubungo, tukapata tiketi ya bus la Arusha linaitwa 'Ngoria'. Sababu ya kwenda Arusha, ni mimi kumuomba twende huko kuliko Zanzibar alikopendekeza yeye. Pia kulikuwa na dada mmoja ni rafiki yangu alipangiwa kazi huko, akatupokea pale Sanawari tukapandisha kwenda Sanawari ya juu.

Yule dada alikuwa mstarabu sana, akatuachia kitanda alale chini maana ni chumba kimoja. Nikaona sio poa, basi ikabidi wote tulale kitanda kimoja Laila katikati. Kufika usiku Laila anataka nile apple lake, ikabidi nimwambie tukalale chini tusimtese dada wa watu. Basi tukahamia chini, kumbe dada anatusikia na yeye hisia zinapanda ila anaogopa kuonyesha. (nilikuja kujua hakuwa na mpenzi kwa muda mrefu sana). Tulikaa wiki kwa yule dada, nikawa natoka naenda mjini kutafuta kazi japo hela za kutumia napewa na mpenzi wangu.

Nikaona sio poa kukaa pale tunamtesa yule dada, nikamwambia Laila inabidi tukapange chumba. Akasema hakuna shida ngoja akaongee na rafiki yake atanijibu. Sikujali sana, akatoka. Mchana karudi, akaniambia amepata chumba sehemu inaitwa 'kimandoru' huyo rafiki yake amemkopesha pesa na ameshanunua vitu vya ndani. Tukamsubiri mwenyeji wetu arudi, tukamuaga na kuondoka. Kufika kimandoru nikakuta chumba kizuri tu na vitu ndani, basi tukaanza maisha mapya.
******

Laila MALAYA

Tulikaa pale kimandoru kwa amani kiasi, ila Laila alikuwa na tabia mara kwa mara anaondoka bila kuaga, akirudi anarudi na ndizi nyama choma. Ila hiyo tabia haikuwa inanikera, nikaona kawaida tu. Yule dada alikuwa ananilisha vizuri sana kitu kilichonisaidia kuto dhoofika mwili kwa kula apple lake kila mara. Tabia ya kutoroka ikakomaa sana…

Siku moja akaniambia anataka anionyeshe uwezo wake, nikamwambia huna uwezo wowote. (kama utani tu) Akasema ninao uwezo mkubwa sana ila kwanza nataka tufunge ndoa ya damu.

Cotterpin: ndoa ya damu ndio ndoa gani!?

Laila: Tunachanganya damu zetu na kula kiapo cha kuishi pamoja siku zote.

Cotterpin: (Nikajua ni utani tu) hakuna shida mimi ni wako tu.

Basi akachukua wembe akajichanja kiganja cha mkono wa kushoto, akanichana na mimi, kisha akakinga damu kwenye kisosi. Akawasha mshumaa akachoma karatasi lililuwa na maandishi ya kiarabu mekundu. Ukatoka moshi mweupe na harufu ya marashi mazuri sana. Jivu la ile karatasi akaweka kwenye ule mchanganyiko wa damu zetu. Akachanganya, kisha akachovya kwa kidole akanipaka kwa duara kidore cha pete, akaniambia na mimi nifanye kama alivyofanya, nikafanya.

Laila: Kuanzia leo wewe ni mume wangu wa ndoa, na mimi ni mke wako wa ndoa.

Nikajua ni utani tu nikakubali.
Basi akaachoma ubani na kupulizia yale marashi yake, mara akaanza kung'aa sana. Akawa mzuri zaidi ya nilivyo mzoea, akaonekana amevaa mavazi mazuri sana kama malikia.

Laila: Mimi ni jini, naitwa Laila, natoka uko wa Peri. Nimekupenda toka siku ya kwanza nimekutana na wewe nje ya mipaka ya ulimwengu (nilikuja kujua baadae maana ya hii kauli) . Ili kukuvutia nilikufumbua macho uuone uzuri wangu huu wa leo, hatimae ukavutiwa na uzuri wangu.

Naomba nikutoe hofu, kuanzia sasa nizoee kwa huu mwonekano wangu, sitakudhuru wala hakuna mtu anaweza kukudhuru isipokuwa ukivunja kiapo chetu

Majini hatupendi kuudhiwa au kudharauliwa, tunaweza kuwa na kiburi na kuchukizwa na watu wanaotudharau au kutuchezea.

Tunakasirishwa na uvunjifu wa sheria zetu au kukiuka taratibu za kutuita au kutuhudumia. Hatupendi harufu mbaya au uchafu, napenda mazingira safi na yanayokuwa na utaratibu, Kuanzia leo huna ruhusa ya kuwa na mwanamke mwingine, kula nyama ya nguruwe, kunywa pombe wala kuvuta sigara, ukivunja kiapo hiki utajuta.

Hatupendi kufichuliwa au kutambulishwa mbele ya watu wengi. Tunapendelea kubaki sirini na kutenda mambo yetu kwa faragha.

Ukiwa mwaminifu kwangu, nitakulinda, nitakupa mali na nitakupeleka kwetu ukapaone.

Binafsi sikuwa na hofu na maelezo yake, kwani hakuwa na umbo la kutisha, bali ni mwonekano wa kug'aa sana na uzuri wake.
 
Maisha yakasonga nikiwa najua uhalisia wa Laila, alikuwa anapenda ngono sana, alinifundisha mambo mengi kitandani. Alikuwa msafi mno, huwezi sikia hata harufu ya jasho tu mwilini mwake. Tuliishi jirani na club Afriko. Tabia ya kuondoka bila kuaga hakuacha.

Siku moja akaniambia kuna mzungu anataka kunipa kazi (aliniombea kazi) , ila ameomba waonane kwanza hapo club Afriko hivyo anaomba niende nae. Basi tukaenda, kufika kweli kuna wazungu wawili na mwafrika mmoja wako meza moja, sisi tukakaa meza ya peke yetu, mhudumu akaambiwa atupe huduma. Wale jamaa hawakuja kuongea na sisi pale, baada ya dakika 30 Laila akaniambia tuondoke pale, tukaondoka bila kuaga. Njiani akawa amekasirika, kufika home akaniambia wale wazungu hawajapenda mimi kwenda na wewe pale.

Kumbe Laila alikuwa anajiuza kwa watu wenye pesa, kuna dada mmoja akaniambia huyu mkeo ni malaya, anajiuza, sikuamini. The same day Laila akanionya kuhusu huyo dada, akaniambia ni mshirikina nikae nae mbali. Kweli yule dada hukuwa anataka hata tupishane njiani, akiniona nakimbia, nikajua Laila amesha fanya yake.

Siku moja nikamtembelea yule dada ali etupokea arusha, nilienda peke yangu, katika maongezi akaniambia kuwa makini na Laila.

Dada: kuwa makini na Laila, ni muhuni

Cotterpin: muhunu kivipi?

Dada: hivi hujui alikuwa anakuacha hapa anafatwa na gari ya tours karibia kila siku?

Cotterpin: mbona muda mwingi huwa niko nae hapa?

Dada: majirani waliniambia hivyo, tena hapo nyumba ya pili alikuwa anatembea na kijana wa hapo akampa simu ya Sony Ericsson. (hiyo simu kweli alinipa akasema kampa rafiki yake)

Cotterpin: sio chuki za watu kweli?

Dada: mimi sina uhakika, ila huyo kaka wa hapo jirani nilimuuliza akasema ni kweli ila hakuwa anajua kama ni mpenzi wako.

Cotterpin: sawa nitamchunguza nione.

Yale maneno yalinifanya nimkumbuke yule dada wa kimandoru, siku hiyo nikaamua kumkorofisha ili nijue ukweli. Nikanunua kitimoto kwenye baa ilikuwa inaitwa chini ya mti pale Sanawari mataa, nikala nikaenda home. Sikumkuta Laila, akarudi amechukia sana. Kufika tu akafunga mlango, akaniambia kwa nini umenichukiza?
*****


Cotterpin: kwani nimefanya nini mpenzi

Laila: umekula uchafu gani huko? Sikukukataza?

Cotterpin: samahani mpenzi, nilikuwa na njaa nikasahau.

Laila: hujasahau umefanya kwa kukusudia baada ya kuambiwa mimi ni malaya.

Cotterpin: Ni kweli, nataka kujua kama mmeo, unafanya umalaya?

Laila alinikazia macho, akakunja sura yake, ghafla akaanza kubadilika na kuwa kiumbe cha kutisha, nikaogopa sana. Akaniambia

Laila: kwa kuwa umevunja makubaliano yetu, nakupa adhabu, tena ulistahili adhabu kali sana, ila kwa kuwa nakupenda sana, sita kudhuru.

Cotterpin: nisamehe mke wangu, nakupenda sana ndio maana nikachukia kusikia unafanya umalaya. Nakuahidi sitavunja tena makubaliano yetu.

Laila: msamaha wangu ni huu, hutaniona kwa siku tatu, mpaka huo uchafu uliokula ukutoke, utakasike. Huna ruhusa ya kwenda popote.

Baada ya kuongea vile alitoka nje na sikumuona tena kwa siku tatu. Siku ya tatu akarudi na furaha sana akiwa na zawadi nyingi kwa ajili yangu. Akaniambia alienda kwao.
****
 
Back
Top Bottom