Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

Wahusika tafakari chukueni hatua la sivyo badilisheni kiwe cha watoto show
 
I never knew kuna such program, but inategemea kuna soko lake, kila program in target viewers au listerners(sp) tofauti, nadhani ukichoshwa change channel,

I subscribe to 102.5 ni jamii ya clouds in the morning na jioni ni any radio that has DW dunia yetu !

TV on weekdays naangalia kwa nadra sana, I record all my favourite shows na kuzirudia weekend especially soapies omnibus, mengine yote nasoma magazetini
 
Clouds TV (Ruge na team yake) mlipoanzisha shindano hili la BIBI BOMBA nilifikiri wanataka kuwatumia bibi hawa kwa ajili ya kutukuza uTanzania wetu, utamaduni wetu na mchango wao ili kufanya vijana wafahamu utamaduni wetu ambao unaanza kusahaulika katika jamii. Lakini tunachokishuhudia hivi sasa ni kinyume chake. Ni udhalilishaji usiovumilika wanaofanyiwa bibi na mama zetu. Haingii akilini kumuimbisha bibi wa miaka 65- 70 nyimbo za muziki wa kizazi kipya au kumvalisha suruali wakati tunazo nyimbo zetu za kabila mbalimbali na pia tunafahamu kabisa katika maisha ya kawaida bibi hao hawavai hivyo!

Ruge umekosea sana(wewe ndiye msimamizi wa TV yako kufanya marekebisho. Jipe muda fuaitili shindano hilo uone kama kuna lolote la maana jamiiinajifunza. Badili maramoja; itapendeza na kuleta maana zaidi kama bibi hawa watashidanishwa kwa mambo yenye maadili na kudumisha utamaduni wetu Watanzania


EJL

Yaani mkuu hapo umenena kabisa nadhani kwa kutumia kipindi hiki labda tungejaribu kurudisha maadili ya kitanzania yaliyopote nadhani kingefanywa wakawa wanatuinyesha ujuzi wao waliokuwa nao wakiwa vijana maadili ya ndoa waliokuwa nao na walivyoishi na waume zao sio sasa hivi ruge omba maoni kwa watu nadhani ujumbe umekufikia kuna mambo mengi ya asili hawa kina bongo flava wa sasa hawajui kutwa wao Fb na wahats hata chakula cha mume kitapikwa fb
 
yaani hakuna kipindi kinachoniuzi kama hicho. ...kitendo cha kuwafanya watu wazima kama watoto wadogo ....eti wanapanga mstairi wanaimba kwaya. ...yaani nachukia sana. ...
 
Mm kwangu nimepiga marufuku kuangalia clouds maana nipo na bibi yangu alafu wanaonyesha huo upuuzi wao wa kunyanyasa bibi na mama za watu wapuuuuzi sana hawa clouds
 
zambada,kaiza sosa,mtumbaya,babuu wakitaa,mfalme mswati....mume wenu....majina kibao

we mkuda umepima?...au nimmoja kat yao alio wapitia tupe ushahidi wa uyanenayo...

ukimwi ni kitu cha kawaida sana mshikaji anakula arv mbona hata watu kibao wanao halafu mbona umeshtuka utadhani umetiwa kidole
 
Clouds imepoteza mwelekeo kazi majungu tu kama mashoga waliokosa mabasha...
 
ukimwi ni kitu cha kawaida sana mshikaji anakula arv mbona hata watu kibao wanao halafu mbona umeshtuka utadhani umetiwa kidole

Kweli uchoko.zi ndio kazi yako...huoni haya kumnnanga bwana wako..af madem kama nyinyi mmnamegwa na kuachwa

au unaendaga nae clinic Shost
 
clouds media wanyonyaji tu,.




Bado hamjawashtukia!!
 
Clouds Entertainment imepata umaarufu kwa kufanya mambo illegal-illegal so sishangai coz ndo style yao.Ndugu za hao mabibi nao ni wendawazimu ndo maana wanawaruhusu kwenda kujidharirisha
 
...dah mkuu,yaani kama ulikuwepo eneo ambalo tulikuwa nasi tunasikiliza hicho kipindi(nilikuwa kwa kinyozi),kiukweli nasi tulijisikia fedheha kubwa sana kuona bibi na mama zetu,kuulizwa maswali ya kijinga namna ile,

Labda nami niwaombe Viongozi wa Clouds TV kwanza wakiangalie vizuri hiki kipindi kwani kina makosa mengi ya kiitaaluma na ikiwezekana watafute mtangazaji mwingine wa kuendesha hiki kipindi,huyo Babuu wa Kitaa hafai,kwanza umarekani mwingi,maneno ya mtaani mengi na maswali ya kijinga.

Inasikitisha sana kwanini TCRA hawajaifungia hii TV na kuipiga faini kwa kuwadhalilisha bibi zetu mchana kweupe. Hivi watetezi wa haki za binadamu hawapo nchi hii? TAMWA mpo wapi bibi zetu wanadhalilishwa kijinsia namna hii? In fact, something must be done before the situation gets even worse. Wizara ya jinsia waamke na kuwatetea mabibi hawa kwa unyanyasi huu wanaopata.
 
Kumbe wengi tunaokerwa na huu ujinga

Hivi hawa Clouds TV hawana uwezo wa kuvumbia kipindi kingine badala ya hiki au ndio wameishiwa kabisa ubunifu? Na pia tuwashangae wale watu wanaoshobokea kipindi hadi kutuma sms kuwachagua mabibi--hawa watuma meseji ndio 'WADHAMINI' wa kipindi hiki na ndio hasa wanaosababisha kipindi hiki kiendelee kudunda! Kama ikiwezekana sote tukasusia kutuma hiyo mimesjei ya kipuuzi, kipindi kitakufa automatically.
 
Mimi sio mtazamaji mzuri wa Clouds TV kwa kuwa vipindi vyake vingi ni vya ovyo--havina mvuto wala mafundisho ya maana. Jana, kwa bahati mbaya, nilitazama kipindi cha 'BIBI BOMBA' kinachorushwa na TV hiyo. Nimehudunishwa sana kuona jinsi bibi na mama zetu wanavyodhalilishwa hadharani. Bibi zetu huulizwa maswali ya kidhalilishaji.

Bibi mmoja aliulizwa kama aliwahi kula mboga inayoitwa 'Biology', akajibu 'ndiyo'. Hili ni swali linalohusu ufahamu na kwa wabibi wale ambao hawakwenda shule, hawajui biology ni nini. Si hivyo tu, hata wale walioishia la saba hawajui biology ni kitu gani. Kuwauliza mabibi swali kama hili ni kuwadhalilisha kitaaluma kwa kuwa tu hawakwenda shule.

Bibi mwingine aliombwa amtongoze kijana yule anayewauliza maswali hadi amkubali. Bibi akatekeleza agizo hilo laivu mbele ya skrini ya TV! Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.

Wizara ya jinsia inapaswa kukataza udhalilishaji huu wa kijinsia. Nasi wananchi tuache kushabikia upumbavu huu--tukatae kuwapigia kura bibi wanaoshiriki.

Sijawahi kuangalia clouds tv tangu iwepo!
 
Siangaliagi tv japo ipo hm
Naenda kublock clouds tv kwenye kingamuzi kwa faida ya familia yangu. Thanx kwa aliyeleta hii habari katusaidia tusioangalia tv.
 
Bibi wa miaka 70 anapofundishwa apozi kama Black American thug na kuambiwa aseme "whatsup ma nigger" na kufanya ndio tangazo la mara kwa mara, huu ni udhalilishaji na ushenzi!!

Yaani yule mtangazaji anayeendesha kile kipindi ni mbumbumbu kuliko maelezo. Eti alimuuliza bibi aseme bhang magazine ni kitu gani. Bibi akawa amemsikia vibaya--akadhani amtetamka BAN MAGAZINE. Basi bibi akajibu "ban magazine ni gazeti lililopigwa marufuku (banned)--yaani ambalo halitakiwi kuwepo". Na lile litangazaji, likiwa kama MODERATOR wa kipindi, halikumsahihisha bibi--likamuacha bibi apuyange hivyo hivyo! Sasa bhang magazine na wabibi wapi na wapi? Litangazaji linauliza maswali ya kibangebange na ambayo hayana mwelekeo wowote! Hivi hawa watangazaji wa TV mbumbumbu kama huyu huokotwa wapi?
 
Back
Top Bottom