Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

wanawavalisha vibaya, wanawadhalilisha, how much do they pay them? ni mshindi tu anapata hela masikini, wanawadhalilisha in the name of money...
 
Ovyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
Seriously hiki kipindi kinadhalilisha mabibi, nadhani kuna haja sasa ya wadau kujitokeza na kukemea kipindi kiki.


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Hivi nikisema mama yake Ruge Mutahaba yuko Bomba nitakuwa nimeongea vizuri ?

...jina la kipindi tu ni la kidhalilishaji kabisa.

TUHESHIMU WAZEE WETU TAFADHALI !!!!!
 
mbaya sana,yaan mama amtongoze mwanae? tatizo letu tunafagilia sana vitu vya kipuuzi,fikiria ingelikuwa mama yako,au bibi yako au shangazi yako! huu ni upuuzi. umaskini wetu sijui utaisha lini MUNGU wangu?
 
Tanzania kila siku wanaunda tume tume za kijinga ambazo hazifanyi kazi, tume za kuunda ni za kushughulikia mambo kama haya, kukagua vipindi vyote vya kwenye TV na maadili, kuvipiga ban visivofaa...
 
Mimi sio mtazamaji mzuri wa Clouds TV kwa kuwa vipindi vyake vingi ni vya ovyo--havina mvuto wala mafundisho ya maana. Jana, kwa bahati mbaya, nilitazama kipindi cha 'BIBI BOMBA' kinachorushwa na TV hiyo. Nimehudhunishwa sana kuona jinsi bibi na mama zetu wanavyodhalilishwa hadharani. Bibi zetu huulizwa maswali ya kidhalilishaji.

Bibi mmoja aliulizwa kama aliwahi kula mboga inayoitwa 'Biology', akajibu 'ndiyo'. Hili ni swali linalohusu ufahamu na kwa wabibi wale ambao hawakwenda shule, hawajui biology ni nini. Si hivyo tu, hata wale walioishia la saba hawajui biology ni kitu gani. Kuwauliza mabibi swali kama hili ni kuwadhalilisha kitaaluma kwa kuwa tu hawakwenda shule.

Bibi mwingine aliombwa amtongoze kijana yule anayewauliza maswali hadi amkubali. Bibi akatekeleza agizo hilo laivu mbele ya skrini ya TV! Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.

Wizara ya jinsia inapaswa kukataza udhalilishaji huu wa kijinsia. Nasi wananchi tuache kushabikia upumbavu huu--tukatae kuwapigia kura bibi wanaoshiriki.

Clouds walinikera walijitoa kwenye receiver za mpg2. Kipindi kile walipokuwa huko walifuatiliwa na watu wengi hata wale wa vijijini ambao wengi wanatumia receiver za mpg2
 
Back
Top Bottom