Azam Tv kupita channel ya sinema zetu, wawaombe msahama walimu kwa kuwadhalilisha

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
Nipo zangu home nimetulia naperuzi kutafuta channel nzuri ya kuangalia nikatua channel ya sinema zetu Azam Tv namba 103 wanaonyesha movie inaitwa simuulizi, Introduction kabla movie yenyewe kuanza.

Picha inaanza mabinti wako kisimani wanateka maji, wakaanza kubishana kuhusu Mwalimu mkorofi shuleni kwao, mmoja akaanza kufanya demonstration ya huyo Mwalimu jinsi anavyofundisha quadratic equation kama vile wanakejeli, baada ya Hapo wadada wote wakacheka, mmoja kati ya wale wadada akasema "MSINIFANANISHE NA HUYO MWALIMU WENU MJINGA MJINGA".....

Mimi kama mdau mkubwa sana wa Elimu hii haiko sawa aisee, Mpwayungu Village hivi huko shuleni Kuna walimu wajinga wajinga? Kwanini vitu vyote vibaya anatupiwa Mwalimu? Kwanini walimu hawapewi heshima? Mpaka hao waigizaji wapumbavu wanapata nguvu ya kuwadhalilisha Walimu kweli?

Azam Tv na nyie mnaruhusu kutuma picha/movie bila ya KUFATILIA maudhui yaliyomo? "Je ni sahii kwa hao waigizaji viazi kutumia kauli ya kumdhalilisha Walimu na ikawa sawa"? Inabidi mtoke muombe msamaha waziwazi.

Ni wakati Sasa kada ya ualimu kuheshimiwa na kuchukuliwa kwa uzito mkubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom