Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

Huu usasa unaoletwa na clouds ni janga lingine la kitaifa!na nnachokiona kwa kizazi hiki cha leo na kijacho ni mmomonyoko mkubwa sana wa maadili.
 
Some Jerry Springer types of shows show the extent of freedom of expression, this freedom should reign supreme, as long as laws are not broken.

Kama hupendi usiangalie, watu wa kutosha wakiacha kuangalia Clouds wenyewe itabidi wabadili vipindi.

Clouds wanaweza kuendelea na vipindi kama hivi ikiwa tu kuna watu wanavipenda.
 
Sijawahi juta kuikosa clouds tv katika king'amuzi changu.
 
Niliona hiyo audition jana kwa mara ya kwanza. Na mimi nakubaliana na wachangiaje wengine, wanadhalilisha akina Bibi ambao ama kwa bahati mbaya hawakufanikiwa kupita shule na kuwa na ufahamu wa hayo wanayoyauliza.

Simuoni pia kama Babuu ni mtu mwerevu wa kuweza kuzungumza na watu wazima wale.
 
Oooh my God, cjawahi kuona kipindi cha ovyo kama hiki! Bibi anaulizwa mara ya mwisho kuhongwa lini, au amehonga lini? Nadhani halafu hawa vijana wanaofanya audition ndio tatizo kabisa, wanavaa kihuni, wanaongea kihuni, lugha mbovu, sauti mbovu, kila kitu matapishi tu aaagggrrril!
 
don't u ever watch that station again. u'll b angry every time.
 
msimu uliopita mabibi waliulizwa nana anaijua FACEBOOK
1.kajibu facebook ni kapu la kuendea sokon
2.mwingine akasema facebooki ni aina nyama inakatwakatwa vpande vidogodgogo
alaf mabibi nao wanakula bata bhasi ndo unawamaliza kabisaaaa
KIUKWELI NILIKUWA MDAU MKUBWA WA CLOUDZ BUT NOW KAMA HAMNA CHAKUANGALIA NATUNE CARTOONS CHANNEL YYTE
 
unashangaza.. sasa huyo bibi alieulizwa swali ambalo wala halijui.. kilichomfanya akubali kuwa alikula biology ni niniii?? maana huwezi kuitikia kitu usichokijua na kuwa ati umekifanya na kumbe hujawahi hata kukiona.. huu ni uzoba wa hao kina mama na wala tv haijawadhalilisha. alichotakiwa kufanya huyo mama alitakiwa ajibu kuwa sijawahi kula biology. na wala asingeonekana mjinga.

kuulizwa maswali ya kishule wakati hawakwenda shule, hapo bibi wanadhalilishwa KITAALUMA. the presenter's aim was to humiliate the grans academically--trying to make them fools and making that 'folly' known to their viewers. this's pure academic discrimation. kwa wale wenye utovu wa maadili mtaona ni sawa lakini huu ni udhalilishaji wa dhahiri.
 
Njaa nazo zinachangia WAKATAZEN BIBI ZENU WASIENDE

hata kama wana njaa, hicho hakiwezi kuwa kigezo cha kuwadhalilisha bibi zetu. TCRA wachukue hatua kukomesha udhalilishaji huu ikibidi Clouds TV wapigwe ban ya maisha. hakuna mtu mwenye akili zilizotimia anayeweza kutetea uhalifu kama huu.
 
Clouds TV (Ruge na team yake) mlipoanzisha shindano hili la BIBI BOMBA nilifikiri wanataka kuwatumia bibi hawa kwa ajili ya kutukuza uTanzania wetu, utamaduni wetu na mchango wao ili kufanya vijana wafahamu utamaduni wetu ambao unaanza kusahaulika katika jamii. Lakini tunachokishuhudia hivi sasa ni kinyume chake. Ni udhalilishaji usiovumilika wanaofanyiwa bibi na mama zetu. Haingii akilini kumuimbisha bibi wa miaka 65- 70 nyimbo za muziki wa kizazi kipya au kumvalisha suruali wakati tunazo nyimbo zetu za kabila mbalimbali na pia tunafahamu kabisa katika maisha ya kawaida bibi hao hawavai hivyo!

Ruge umekosea sana(wewe ndiye msimamizi wa TV yako kufanya marekebisho. Jipe muda fuaitili shindano hilo uone kama kuna lolote la maana jamiiinajifunza. Badili maramoja; itapendeza na kuleta maana zaidi kama bibi hawa watashidanishwa kwa mambo yenye maadili na kudumisha utamaduni wetu Watanzania


EJL

we ndo unaakili unatoa hoja ambayo inamaana bora wabadili mambo ynao fanyika ya kipuuzi.
 
Some Jerry Springer types of shows show the extent of freedom of expression, this freedom should reigns supreme, as long as laws are not broken.

Kama hupendi usiangalie, watu wa kutosha wakiacha kuangalia Clouds wenyewe itabidi wabadili vipindi.

Clouds wanaweza kuendelea na vipindi kama hivi ikiwa tu kuna watu wanavipenda.

hv unajua unachokiongea? here we are talking about discrimation--nothing to do with freedom of expression. kwa hivyo wewe mtu akikuuliza mbele ya hadhara kwamba ukienda haja kubwa huwa unajisikiaje, huo ni uhuru wa kujieleza au ni udhalilishaji? mazombi kama wewe ndio mnasababisha nchi hii ichelewe kupiga hatua za maendeleo.
 
Kweli aisee,yule jamaa anayeongoza auditions is unthinking,kipigwe ban mara moja
 
Ukweli hicho kipindi hakina maadili kabisa zaidi ya kutia aibu mama/bibi zetu.
 
Mi nasema hivi,wale watangazaji ni wapenda chini.Kama unataka kuwa na babu wa kufikia basi endelea kuruhusu bibi zenu kwenda.
 
Unauliza nini maana ya biology wakati unajua kuwa hawajui, yaani pale burudani ni jins wanavotoa majibu wrong, kweli huo ni udhalilishaji.
 
wamekosea sana clouds jipen mda mtafakari ubovu huu mjirekebishe
 
Vitu haramu haramu huwa vina uhusiano na ccm.
...nahisi hii clouds ina uhusiano fulani na ccm
 
Back
Top Bottom