Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

Zamani bibi zetu wakitusimulia hadithi na kutupa maonyo na mausia. Siku hizi wanafundishwa bongo flavor!
 
Yani ni udhalilishaji, sasa mantiki ya kipindi kama kile ni nini? si bora hata wangeandaa kipindi ambacho wanawakusanya hao mabibi na kusimulia watoto hadithi za zamani, angalau watapata cha kujifunza sio huu ----- wanaoufanya sasa hivi.

Hata mimi sijui mantiki na mafundisho ya kile kipindi hasa ni nini zaidi tu ya kuwadhalilisha bibi zetu.
 
Mimi nilikuaga mfuatiliaji mzuri sana wa vipindi vya clouds , lakini kipindi kama kile cha saa kumi cha kina kibonde kilinifanya niachane kabisaa na hiii radio, watu w azima kazi kuongea upuuzi na kucheka ovyo kama mashoga, yani wanaudhi sana, upuuzi ni mwingi sana kwenye vipindi vyao.

Neno la mwisho mwisho uliloandika (kama), liondoe na badala yake lisomeke (kwa sababu ni)
 
Can this prevent the humiliation of our grans? Read, digest and understand the post well before commenting.

The mental power by which one controls ones thought,actions and decisions..Do you believe in freedom of the will?
 
Na utashangaa vitu vinavyodhalilisha utu wa mwanadamu kama hivyo ndivyo vina mashabiki kibao....safari ya maisha ni ndefu na hauwezi jua litakalokufika huko mbeleni . .enyi vijana mnaotafuta hela na umaarufu kwa kudhalilisha wengine jueni kwamba kesho utakuja kudhalilika wewe kwa namna moja ama nyingine.
 
Mimi sio mtazamaji mzuri wa Clouds TV kwa kuwa vipindi vyake vingi ni vya ovyo--havina mvuto wala mafundisho ya maana. Jana, kwa bahati mbaya, nilitazama kipindi cha 'BIBI BOMBA' kinachorushwa na TV hiyo. Nimehudunishwa sana kuona jinsi bibi na mama zetu wanavyodhalilishwa hadharani. Bibi zetu huulizwa maswali ya kidhalilishaji.

Bibi mmoja aliulizwa kama aliwahi kula mboga inayoitwa 'Biology', akajibu 'ndiyo'. Hili ni swali linalohusu ufahamu na kwa wabibi wale ambao hawakwenda shule, hawajui biology ni nini. Si hivyo tu, hata wale walioishia la saba hawajui biology ni kitu gani. Kuwauliza mabibi swali kama hili ni kuwadhalilisha kitaaluma kwa kuwa tu hawakwenda shule.

Bibi mwingine aliombwa amtongoze kijana yule anayewauliza maswali hadi amkubali. Bibi akatekeleza agizo hilo laivu mbele ya skrini ya TV! Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.

Wizara ya jinsia inapaswa kukataza udhalilishaji huu wa kijinsia. Nasi wananchi tuache kushabikia upumbavu huu--tukatae kuwapigia kura bibi wanaoshiriki.

wanazingua nöma bb zetu
nacema haifai@
 
Bibi wa miaka 70 anapofundishwa apozi kama Black American thug na kuambiwa aseme "whatsup ma nigger" na kufanya ndio tangazo la mara kwa mara, huu ni udhalilishaji na ushenzi!!

Ni takribani wiki mbili sasa nilizungumzia hii kitu lakini kwa mshangao wa wachache, watu wengi sana tena wengine walijaribu kufananisha tamaduni za kimarekani na za kibongo.

Nazungumzia jinsi Mpoki alivyoendesha sherehe za kuwatuza wasanii wa muziki kwenye KTMA. Wengi walituponda (wale tulioona udhalilishwaji kwa watoa tuzo) eti hatuna exposure nk. Lakini huwezi kufananisha MTV,BET,Grammy Awards na KTMA na bado ikaziita kikwetu kwetu!!!

Sasa angalau nashukuru watu wameanza kuliona hili kupitia shindano hili la bibi zetu. Shindano hili sijawahi liona zaidi ya kusikia komenti za watu. Hata hivyo maswali hayo yanawasaidia nini hawa bibi zetu na wale wanaotizama?

Isije ikafika siku tukaona bibi zetu waki parade na swim suits kwenye TV kwa dhana tu ya kwamba hata 'America's got talents' vibibi hujitokeza.
 
Clouds TV (Ruge na team yake) mlipoanzisha shindano hili la BIBI BOMBA nilifikiri wanataka kuwatumia bibi hawa kwa ajili ya kutukuza uTanzania wetu, utamaduni wetu na mchango wao ili kufanya vijana wafahamu utamaduni wetu ambao unaanza kusahaulika katika jamii. Lakini tunachokishuhudia hivi sasa ni kinyume chake. Ni udhalilishaji usiovumilika wanaofanyiwa bibi na mama zetu. Haingii akilini kumuimbisha bibi wa miaka 65- 70 nyimbo za muziki wa kizazi kipya au kumvalisha suruali wakati tunazo nyimbo zetu za kabila mbalimbali na pia tunafahamu kabisa katika maisha ya kawaida bibi hao hawavai hivyo!

Ruge umekosea sana(wewe ndiye msimamizi wa TV yako kufanya marekebisho. Jipe muda fuaitili shindano hilo uone kama kuna lolote la maana jamiiinajifunza. Badili maramoja; itapendeza na kuleta maana zaidi kama bibi hawa watashidanishwa kwa mambo yenye maadili na kudumisha utamaduni wetu Watanzania


EJL

EJL Kula like za kutosha. Sina cha kuongeza umemaliza kila kitu.
 
Siangaliagi tv japo ipo hm
Naenda kublock clouds tv kwenye kingamuzi kwa faida ya familia yangu. Thanx kwa aliyeleta hii habari katusaidia tusioangalia tv.

Kama hali ndio hii ya kila mtu kuona hawa jamaa ni shidah katika jamii, basi kuna umhimu wa TCRA kutazama upya kazi zao na vipindi pia.

Na jiuliza kitu kwanini station nyingi sijawaiona zikilalaimikiwa hapa kwa kazi kuna kitu hapa

cc; Ruge
 
Last edited by a moderator:
The mental power by which one controls ones thought,actions and decisions..Do you believe in freedom of the will?

,,,,and do you believe in humiliating someone because of some fake gains? Isn't that equal to breach of human rights and dignity?
 
Kama hali ndio hii ya kila mtu kuona hawa jamaa ni shidah katika jamii, basi kuna umhimu wa TCRA kutazama upya kazi zao na vipindi pia.

Na jiuliza kitu kwanini station nyingi sijawaiona zikilalaimikiwa hapa kwa kazi kuna kitu hapa

cc; Ruge

Asante sana mkuu, kwa kusaidia kufikisha ujumbe kwa wahusika (kama kweli akaunti hizo ni zao). Mimi sasa hivi nawaandikia LHRC, TAMWA, Wizara ya Maendleeo ya Jamii, WAMA, TAWLA na wadau wengine wanaoweza kutusaidia kusimamisha huu udhalilishaji.
 
Last edited by a moderator:
Ndio maana nasema hapa Tz tutaendelea kusubiri sana hasa nikilinganisha na wenzetu wa kenya wanavyoendesha vipindi vya TVs zao, angalia Citizen Tv, KTN, NTV wako mbele sana, ndugu wa hawa bibi ni WAPUUZI kuliko hao Clouds
 
Tamaa ya pesa ni mbaya sana sidhani kama wale mabibi wanaooneshwa kwenye hiki kipindi kama wana watoto au wajukuu.

Ni aibu kwa WaTz wote.
 
Back
Top Bottom