tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,153
- 27,722
Mimi sio mtazamaji mzuri wa Clouds TV kwa kuwa vipindi vyake vingi ni vya ovyo--havina mvuto wala mafundisho ya maana. Jana, kwa bahati mbaya, nilitazama kipindi cha 'BIBI BOMBA' kinachorushwa na TV hiyo. Nimehudhunishwa sana kuona jinsi bibi na mama zetu wanavyodhalilishwa hadharani. Bibi zetu huulizwa maswali ya kidhalilishaji.
Bibi mmoja aliulizwa kama aliwahi kula mboga inayoitwa 'Biology', akajibu 'ndiyo'. Hili ni swali linalohusu ufahamu na kwa wabibi wale ambao hawakwenda shule, hawajui biology ni nini. Si hivyo tu, hata wale walioishia la saba hawajui biology ni kitu gani. Kuwauliza mabibi swali kama hili ni kuwadhalilisha kitaaluma kwa kuwa tu hawakwenda shule.
Bibi mwingine aliombwa amtongoze kijana yule anayewauliza maswali hadi amkubali. Bibi akatekeleza agizo hilo laivu mbele ya skrini ya TV! Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.
Wizara ya jinsia inapaswa kukataza udhalilishaji huu wa kijinsia. Nasi wananchi tuache kushabikia upumbavu huu--tukatae kuwapigia kura bibi wanaoshiriki.