Clouds FM yaishambulia JamiiForums

Clouds FM yaishambulia JamiiForums

Waje kwanza waangalie JF ina majukwaa mangapi,hapo ndio watakutana na jukwaa la ("CELEBRITIES") na watu wote wana uhuru wakuandika wanachotaka kuhusu hawa watu na wahusika wanaotajwa. Pia wana haki ya kuja hapa kupinga lolote baya lilozungumziwa kama sio kweli au kurekebisha tabia kama ni ukweli ili jamii isiwazungumzie maisha yao binafsi na pia wanaweza kuja kutoa shukrani wanaposifiwa.

Sijaona hapa mtu anazungumzia maisha ya jirani yake au rafiki yake, watu wanazungumziwa humu ni wale wanaigusa jamii yetu na ndio maana wanapofanya makosa watu watakuzungumzia kwa vile kazi yako inaigusa hio jamii. Gadner na Kibonde wanatakiwa wajue hilo swala kwamba hili swala sio Tanzania tu bali ni duniani kote.

Kwahiyo kama hawa wawili watakuja kusoma hapa nadhani watapata kujielimisha kwanini wanazungumziwa humu, na wajue JF sio kikundi bali ni watu binafsi tofauti ambao wanawasikiliza kila siku na wamepata uhuru wakutoa maoni yao na ni vizuri sana kwani kwa wao kulalamika imeonesha kwamba ujumbe umewafikia.
 
well said mkubwa wangu!!!

hawa jamaa sidhani hata kama wanajitambua wao ni nani na kazi yao ina impact gani kwa jamii........
are they proffessionals au ndo tuamini kuwa ni makanjanja tu kwa huu upuuzi wanaoufanya??
 
nadhani kisu kimefika kwenye mfupa.........

tutaona mengi...na tutasikia mengi.......hii ni 2010....msimu wa kula na kuliwa(courtesy mkuu wa kaya)
 
gadner kalalamikiwa na mkewe kama jf tunamfatafata,na mzee kuonyesha naye yumo akaenda kutunanga kwenye kipindi chake,huyo kibonde,ni kibonde kweli km jina lake,maana kwaakili yake anajua jf ni mwiba wa chama cha majambawazi,nayeye kashajiunga sasa anajipromote ili wampe ulaji wa kubwabwaja kwenye mikutano yao,wote wanatetea ugali wao tu hawana lolote,maana gadna mkewe akinuna inabidi alale sebuleni na kupelekwa outing hakuna.
 
kibonde ni mc wa kwenye maharusi na send-off parties hivyo kwa yeye kuongea ongea chochote ni kawaida yake!
wanajifanyaga wanajua sana!
halafu siku hizi nimegundua hawa watu maarufu wakitaka attention tu wanaitumia JF kusema sijui imenisema sijui hili na lile!
 
Mtu akilalamika hata ujinga ni haki yake kulalamika ni wakati wako wewe mlalamikiwa uangalie mbona unalalamikiwa jirekebishe au mwisho wako waja -
 
hao jamaa, hawana lolote la kuzungumzia jf kwa ubaya, vinginevyo wawe wametumwa

na jopo la mafisadi wa ufahamu wa akili za watu ili kuwafanya wapuuze umuhimu wa Jf

JF ina faida kubwa kwa jamii kuliko hata kituo chao cha radio,

shame to them...!!
 
gadner kalalamikiwa na mkewe kama jf tunamfatafata,na mzee kuonyesha naye yumo akaenda kutunanga kwenye kipindi chake,huyo kibonde,ni kibonde kweli km jina lake,maana kwaakili yake anajua jf ni mwiba wa chama cha majambawazi,nayeye kashajiunga sasa anajipromote ili wampe ulaji wa kubwabwaja kwenye mikutano yao,wote wanatetea ugali wao tu hawana lolote,maana gadna mkewe akinuna inabidi alale sebuleni na kupelekwa outing hakuna.

..........Mhhhhhhhhhhhhhh!!! Babu kijana unaua sasa.
 
well said mkubwa wangu!!!

hawa jamaa sidhani hata kama wanajitambua wao ni nani na kazi yao ina impact gani kwa jamii........
are they proffessionals au ndo tuamini kuwa ni makanjanja tu kwa huu upuuzi wanaoufanya??

Pole sana B, ....Naona jamaa wamekuchefua kweli kweli.

Mimi nilidhani Clouds wanashughulika na muziki (+ burudani nyingine na usanii sanii). Wameanza lini kujadili hoja? Hiyo ndo taabu ya kuingia uwanjani bila jezi wala mazoezi. Hata hivyo naungana na baadhi ya wadau kwamba tuwanange kiaina aina ili waende shule kwanza wajifunze jinsi ya kushusha nondo badala ya usanii 24/7.
 
Clouds FM ni brain washers,wamejaa vilaza watupu pale,wanadhani sisi ni vilaza kama wao. Muhimu sana jamani tuachane nao,ni watu wasio na umuhimu wowote kwenye jamii yetu zaidi ya WIZI WA KAZI ZA WASANII na ujanja ujanja mjini.

Tuachane "nao" wezi wa kazi za wasanii ama tuachane na hoja kuhusu "wizi wa kazi za wasanii?"
Na pia ni kweli kwamba hilo halina umuhimu wowote kwenye jamii?
 
hao ni kama kelele za vyula wa majini, ambazo haziwezi kutuzuia kulala usingizi
 
Bwana kama wao hawaoni faida ya jf basi ni wao km wao.mtu akishikwa pabaya hanabudi kulalama.so tuwaache walalame tu.
 
Kuna mambo mengine ni bora kuyaacha yalivyo...Kibonde na Gadner wana nini cha kuizima JF? Hawa wababaishaji na mambo yao ya vijiweni wanayoyaongea kwenye vipindi vyao?Kama tunataka kujenga Tanzania kwa mambo ya mizaha mizaha kama ya kipindi cha jahazi basi tumeliwa.
Na kwa mara nyingine, tuwaache wafu wawazike wafu wenzao.
 
Ephraim na Gardner wana elimu gani???,mwenye kujua anijuze

Najua ni off point, lakini hata mimi nilikuwa na hamu sana ya kujua hili, hasa baada ya wiki iliyopita nilipomsikia huyo Gardner akirudia zaidi ya mara tatu kusema mkoa wa Moshi.
 
Nasikiliza kipindi cha Jahazi hapa cha Clouds FM, Ephraim Kibonde na Gadna wametumia zaidi ya dakika 5 za kipindi chao wakiponda na kulalamika kuwa JF inajadili mambo binafsi ya watu badala ya kuzungumzia hoja.

WanaJF mnachukuliaje mtazamo huu?

Je, ni kweli kuwa hakuna mambo ya msingi tunayojadiliana hapa jamvini au mwenzetu ni kipofu hatembelei JF zaidi ya kusimuliwa yanayojiri humu??

Much as i would like to be neutral nadhani clouds wanasahau kwamba kushindana na JF ni sawa na kupaka rangi upepo

i am sorry kibonde uko uchi ingawa hujijui and you are my very good friend, sasa chutama!! gardner, rudi getini breweries kama umeshindwa kuelewa kwamba lila na fila havitangamani!!!

sick and sick dont make it well being
 
Nlifikiria mletaji wa post hii angelituwekea hicho walichosema hasa. Mimi nahisi kuna ukweli wa waliyoyaongea kwa kiasi hicho hicho mleta post hii alichotujuvya.

Na majibu yaliyofuata baada ya post hii, mengi yao yameakisi kule kule kwanye madai ya walalamikiwa ie Kibonde na Gadna, watu badala ya kujadili uhalali wa madai yao, wamekwenda kwenye vitu visivyonamsingi wowote kwenye hoja yao au malalamiko yao, masuala ya elimu, nani kawatafutia kazi za utangazaji, itikadi zao za siasa hazihusu kitu kwenye mada hii au madai waliyoyatoa zaidi ya kuthibitisha kile wanachokilalamikia humu jamvini. Hayo ndiyo yale mambo binafsi wanayolalamika kuwa jamvini humu yanashikiwa bango kuliko hoja za maana.

Sote tunakumbuka majadala wa kipuuzi uliowahi kuletwa humu jamvini kuhusu "ukabila" wa mwanamziki nguli, Lady jaydee. Mjadala ule ni wazi kuwa uligusa maisha yake binafsi zaidi kuliko mambo mengi ya maana ambayo unaweza kumuongelea mtu kama Jay dee, ukabila wa mtu ni mambo yanayomhusu mwenyewe unless otherwise, ameyaweka mwenyewe katika mjadala wazi unaoleweka na siyo mtu akurupuke tu kuja na mada ihusuyo mambo ya mtu kujisifia tu kwa raha zake.

Nionavyo, watu humu wabadilike, waache kujifanya kujuwa kwingi na kudhihirisha kuelimika kwao kudogo, ambako wao wanakuona kukubwa, kwa kuacha kujadili "issues" na kujadili watu, hayo ni mambo ya walioishiwa na hoja kama vile mwanamme mpumbavu anaposhindana na mwanamke kwa maneno, mwishowe akishindwa anaamua kurusha ngumi. Tubadilikeni jamani! na si kila anayesema ukweli zidi yetu aonekane adui au haipendi JF, sisi si malaika kama kila kitu tupo sawa, tunakosea na tunawakosea watu, kama waungwana na wasomi kweli, tunavyojidai, basi tukubali kujisahihisha tunapoikosea, siyo kupayukwa payukwa pale ukweli unapotugusa.
 
Nimesikiliza na nimesoma. Kwa muda mrefu kumekuwa na dalili za wazi kuwa hiki kipindi chao kina mlengo fulani.

Katika hoja yao leo wamesema kuwa " CCM wametangaza kampeni yao na kama wewe una kampeni yako peleka pale watatangaza" ninalotaka kujua ni kwamba jana jioni Kibonde alikuwa anaongea na nani aliyemharibia jioni yake ambaye ni mwana JF? Jitokeze na utueleze hoja yenu ilikuwa kitu gani mpaka leo tutukanwe kiasi hiki na hiki kibwana mdogo ambacho tukiamua leo kinarudi kijijini Tukuyu kwa miguu.

Angalia sana kijana hapa kuna watu wanaokupa mkate wako wa kila siku acha kutukana jamii yote. Nimechukizwa sana na maneneo yake na ni vyema atumie njia ileile kutuomba radhi sisi.

Najua pale Clouds halipwi zaidi ya posho kazi tunazompa sisi ndizo zinampa kiburi, tukifunga bomba umekufa njaa kaka. OMBA RADHI HARAKA.
Huwezi jua bwana labda nao ni makada wa chama ila hawataki kusema waziwazi. Kitu kibaya kabisa itakuwa ni kujaribu kutufanya wote wajinga ili malengo yao binafsi yatimie
 
Jamani Clouds wannataka umaarufu kupia JF kwani radio yao hata Masebe kwa akina Kibonde haifiki ilihali JF ni ya dunia nzima bana
 
Unawezaje kutenganisha Hoja na Watu? Unawezaje Kutenganisha Mafisadi na Ufisadi? Unawezaje Kutenganisha Uzinzi na Wazinzi? Unawezaje Kujadili Wizi kama hmna Wezi
 
jamaa pale wanaangalia pesa tu,hawana maslahi kwa taifa..ni kupoteza muda kuwajadili humu..
 
Back
Top Bottom