Clouds FM yaishambulia JamiiForums

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Nasikiliza kipindi cha Jahazi hapa cha Clouds FM, Ephraim Kibonde na Gadna wametumia zaidi ya dakika 5 za kipindi chao wakiponda na kulalamika kuwa JF inajadili mambo binafsi ya watu badala ya kuzungumzia hoja.

WanaJF mnachukuliaje mtazamo huu?

Je, ni kweli kuwa hakuna mambo ya msingi tunayojadiliana hapa jamvini au mwenzetu ni kipofu hatembelei JF zaidi ya kusimuliwa yanayojiri humu??
 
Huyo ndio maana anaitwa Kiponde wao comment zao na kujifanya wanajua kila kitu wanaboa sana, kupewa kuongea redioni siyo kuwa na ufahamu wa kila kitu
 
Waache wapige kelele hao makanjanja wanadhani tutawaogopa? Kwanza wamefanya vizuri manake jamaa ambao hawakuifahamu JF ndo wamefunguliwa macho. Si ajabu hawa walojiunga leo hapa jamvini ni baada ya kuwasikia kina Kibonde. Wafie mbali!
 
Mimi binafsi alikera majuzi, alipotoke kijani pale mlimani city.

Unajua unapokua mtangazaji/mwanahabari unawahudumia jamii kubwa ya watu ambao wapo wenye vyama, wengine hawana kabisa, hasa ktk mazingira haya ya bongo ambapo watu wengi tumechoka.

Sasa mwanahabari unapotokea kijani, hafu kesho tukakusikia redioni unaelezea mambo ya chama fulani, tutakuaminije, wakati wewe tunakujua ni wa kijani. Mimi nadhani haikuwepo sababu yoyote ya kuvalia kijani pale.

Hata kama ni mkereketwa wa Chama Cha Mafisadi (Richmond, Meremeta, EPA, n.k)
 
Hivi Ephraim na Gardner wana elimu gani(off topic)???,wanayo elimu ya Uandishi wa habari??...Sometimes tuwe tunaangalia na uwezo wao wa kielimu..Unaeza kuta si kosa lao....................
 
Kwanza huyo Kibonde na Abash wana elimu gani? Msije mkawa mnajadili watu waliofeli mitihani ya darasa la nne. Na wameingizwa humo radioni na masugar mamy.
 
Sishangai
maana hata shetani hupinga mipango na kuikandya ya Mungu.
 
Wapayukaji hao waache wapige kelele kama hawajaona hoja humu..basi vichwa vyao vimejaa maji.
 
Hawaja lolote tu kazi kupiga domo tu na huyo Garder anafanya promosheni za mke wake tu
 
Huyo kibonde haipiti muda atapelekwa Mirembe. Hivi siku hizi amechukua nafasi ya Chiligati? maana nimemsikia akiwashambulia wana ccm wenye mtizamo tofauti ikabidi nihamishe station kwenda radio one. Shame on him
 
kibonde ameajiriwa kama day worker,-part time wa clouds FM,jamani mwacheni amtumikie kusaga and clouds Media,kwani maisha dar ni magumu na hasa ukijua umuhimu wa kutunza na kulinda afya and diet.
in short kibonde can say anything as instructed by his bwana and bwanas freinds/associates.
TUMWACHE KIBONDE AMTUMIKIE ,I listend to his program everyday ktk traffic jams,to me its like listening to comedy,na vichekesho,FULL STOP.tuache kumpa chat kwa kumjadili humu,kipindi cha jahazi sio kipindi siriasi ni sawa na kusoma Cartoon ktk gazeti,unasoma after news na kucheka basi.so Kibonde and Co.tuwaaache,
kitu kizuri ametupa promo ya BURE kwa kutaja Jamii Forums ktk radio.
 
Kimsingi, Kibonde kuna baadhi ya vitu ana uelewa navyo, lakini kuna mambo hana uwelewa nayo kabisa lakini anang'ang'ania kuyaongelea na kuyashikia bango.

Sielewi kipindi chao kina maana gani kama mtu mmoja..Kibonde, ataanza kuwaeleza watu/umma wa wasikilizaji maoni yake binafsi, na kuyasisitiza kama vile maoni hayo ndo sahihi kabisa.

Kuvaa kwake kijani..........tunawajua, wanatafuta fadhila, wamedanganywa kwamba kwa vile wanajua kuongea upupu, basi wakiingia ccm watapita kwa njia ya vijana, the ubunge wa kuteuliwa....... Samahani, nilisahau kama Kibonde ni mwanaume.

Im otta here!
 
Hii ina maana JF inakua (growing), ila naona baadhi ya watu hapo juu wamekuwa wakali baada ya kukosolewa...Ni budi mkumbuke kuwa ni kweli baadhi ya thread humu zimeacha kujadili hoja na kukazania personality za watu. Kwa hiyo ni muhimu kama watu wazima tukubali kuwa hapo kuna kaukweli ndani yake, ingawa kwa kiasi kikubwa mijadala mingi ni kuhusu maswala muhimu.

Nakumbuka miaka ya chama kimoja Tz, CCM walikuwa wanadai kuwa kukosoa na kukosoana ruksa, ilhali hakuna aliethubutu kufanya hivo kwa viongozi wao. Hivyo mi naona sawa tu ingawa sikusikiliza hicho kipindi ila nakubali na niko muazi kwa maoni ya watu wote hasi au chanya, bring them on!! Tukumbuke kuwa kukosolewa ni mojawapo ya kusonga mbele kwa uhakika..
 
Wasitegemee kuwaeleza watanzania utumbo halafu watu wenye akili timamu wakakaa kimya.
 
kibonde ameajiriwa kama day worker,-part time wa clouds FM,jamani mwacheni amtumikie kusaga and clouds Media,kwani maisha dar ni magumu na hasa ukijua umuhimu wa kutunza na kulinda afya and diet.
in short kibonde can say anything as instructed by his bwana and bwanas freinds/associates.
TUMWACHE KIBONDE AMTUMIKIE ,I listend to his program everyday ktk traffic jams,to me its like listening to comedy,na vichekesho,FULL STOP.tuache kumpa chat kwa kumjadili humu,kipindi cha jahazi sio kipindi siriasi ni sawa na kusoma Cartoon ktk gazeti,unasoma after news na kucheka basi.so Kibonde and Co.tuwaaache,
kitu kizuri ametupa promo ya BURE kwa kutaja Jamii Forums ktk radio.

Vichekesho/Comedy/Cartoon/Udaku na vingine vifananavyo na hivyo Watanzania walio wengi wanavihusudu sana... WaTZ wamechoka na vitu serious... Bora tuna watu kama kibonde,Shigongo,Kipanya etc wanawapunguzia waTZ stress
 
Back
Top Bottom