CLOUDS FM | Before & After...!

NDUKI

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
3,423
2,414
SALAAM...!

Natumai muwazima kabisa. Well...!

Clouds FM (CMG) ni Radio iliyoleta mapinduzi katika huu muziki wa kizazi kipya na hata miziki mingine, tangu ilivyosemwa kuwa muziki wa Bongo Flavor ni uhuni watu waliukataa. Ila niseme tu, ujio wa radio hii uliwaaminisha WENGI sana kuwa huu muziki sio uhuni na wala sio muziki wa wahuni hata kidogo, japo matendo ya wanamuziki hao yalionekana ni ya kihuni.

Kipindi hiko tukiskiliza Clouds FM tuliskia sauti za kina Bony Love (DJ BONNY) na K-Single (KIBACHA) Wa Kwanza Unit (K-U Crew) katika Daktari wa Midundo (DR. BEAT) kabla hatujaamshwa na FINA MANGO, MASOUD KIPANYA na GERALD HANDO,bila ya kumsahau BARBARA HASSAN katika POWER BREAKFAST.

Tuliendelea kuburudishwa na Dada Mkuu AMINA wa CHIFUPA A.K.A (AMINA MPAKANJIA) akiwa na ZAMARADI MKETEMA na GEAH HABIB katika (LEO TENA) huku JAHAZI likiongozwa na CAPTAIN GADNER G HABASH kabla ya kuingia OTHAMN NJAIDI kutoka MAWINGU BAND na Bugigo (DJ BOOGY MASTER) kwenye AFRICA BAMBATAA. Usiseme nimemuweka pembeni DJ SKILLZ na DJ MOOLY BLING BLING ( MOOLY B) ila kaa ukijua tu kuwa tunathamini michango yao. Bila ya kumsahau LADY JD.

Mdogo mdogo tulimalizia show na DJ BONNY LOVE bila ya kumsahau mdogo wake DJ BONNY VENTURE na mwisho wakitukabidhi FINA MANGO tulale nae mpaka mida mibovu baada ya kumaliza na EPHRAIM KIBONDE kwenye kipindi chake cha michezo akiwa na CYPRIAN MUSIBA au MUSIBA CYPRIAN kama skosei hata skumbuki aisee, usiku m-bovu tukiwa na DJ ELLY huku SEBASTIAN NDEGE akituliwaza na story zake za MATUMAINI kila JUMAPILI wakati Kaka BONDA akitulelea watoto wetu kila JUMAMOSI asubuhi kabla hajaingia K-SINGLE na BONNY kwenye kipindi cha BONGO FLAVA.

Lakini leo hii, siipati ile ladha ya Clouds kama Clouds niliyoizoea before. Clouds ya leo ina wakina Mwijaku...! KWELI...?

Hao wakina Babuu, Jose Mara, Kennedy na wengine siwajui nawaskia tu, therefore sina comments zao kihiiivyo coz imekuwa ngumu kuskiliza Clouds kama nilivyokuwa naskiliza zamani coz 'FLAVA'/'LADHA' niliyokuwa naipata mwanzo siipati tena.

Hivi kweli leo hii Clouds FM kama Radio Kongwe Tanzania inaajiri mtu kama Mwijaku, KWELI...? ILI IWEJE...?

Kwenye LOOPHOLE unawapa watu nafasi ya kupenya na wakishapenya inakuwa NGUMU sana kuwarudisha walipotoka. Hatukatai sawa biashara ni matangazo, ila SERIOUSNESS ndio KILA KITU. SIO UKATUNI..! SIO UTANI...!.

RUGE amekufa akiwa ameiacha Radio kwenye status nzuri sana, ila status ambayo ameiacha RUGE ukilinganisha na sasa siwezi ku-judge wala ku-compare. Lazma ukweli usemwe, kuna mtu kama Adam Mchomvu amefanya ujinga mwingi sana Clouds huku BIG JOE akimuangalia tu, siwezi juwa wana uhusiano gani na wala staki kujua ila, Brand itabaki kuwa ni brand tu daima milele.

Kwangu mimi afadhali ya ADAM kuliko huyu jamaa ambaye niliuliza, hivi huyu ni nani, watu wakaniambia ni mtangazaji wa Clouds FM. Nikabaki nashangaa, hivi ni kweli Clouds iliyokuwa inaibua watangazaji wanaojilelewa leo hii inaajiri watu wa aina hii, KWELI...?

Sina cha kulaumu wala kushauri ila nimebaki nikiwaza tu ilivyokuwa CLOUDS FM | BEFORE & AFTER.

NDIVYO ILIVYOTAKIWA KUWA SASA HIVI ILIVYO CLOUDS FM...?

KWELI...?

KIND REGARDS.

Hii redio 2014 kurudi nyuma kwangu mimi ilikuwa bomba sanaaa burudani na mizaha ya kipindi kile ili nibamba sana tofauti na sasa hv 😆🤣😂
 
Mkuu unaonekana ni mtu wa kitambo sana na hii radio, niwe mkweli tu sio wa kitambo hivyo! Lkn sjawahi kuwa na wakati wa kupenda kusikiliza radio kama nilivyopenda vipindi hivi vya Clouds:-

JAHAZI
Ile ya kina Efraim Kibonde, Wasiwasi Mwambulambo na Arnod Kayanda aisee ilikuwa ikifika saa 10 jioni lazima nisikilize radio

AMPLIFAYA
Kipimdi kile inaanza ilikuwa ya moto sana, nimesikiliza jana kama dakika 2 tu nikazima radio haina content tena vitu vya kipuuzi kabisa anaulizwa Dogo Janja ashauri Fid kushirikishwa na Chino wana man amapiano yaani story za kubishana vijiweni ndio inakuwa content radioni, ilikuwa kidogo nilete thread humu niulize au mimi umri wa hivyo vitu umenitupa mkono

SPORT XTRA
Ile ya 2014 kurudi nyuma, japo inawezekana kupungua kwa ladha ya mpira hasa hasa EPL imenifanya nisiwe mfuatiliaji sana wa vipindi vya mipira

Upande wa tv (Clouds tv) Clouds 360 ile ya kina Babie Kabae, Hassani Ngoma na Sam Sasari ilikiwa inanibamba sana pia

Sasa hivi sio kuisikiliza Clouds tu sisikilizi kabisa radio karibia zote vipindi ni kama wamepewa content na mtu mmoja asubuhi ukiwasha radio karibia zote vipindi ni vile vile ikifika saa 8 mchana wote wana vipindi vya bongo fleva, jioni na usiku ni vile vile imefikia wakati watangazaji nao kama wanaigana style za kuongea

Yote kwa yote kuna yule wa wasafi fm ambae kila siku lazima atamke neno "stuff like that" kama mara 10 hivii sjui the mvp the half man duh! Tuna safari ndefu sana
 
Mtu mmoja, Mwijaku unatumja kama mfano wa kuisema clouds imekosa Ladha. Una conflict of Interest. Zama zinabadilika kama umezeeka we tulia, sisi generation yetu tunaenjoy kina mwijaku we usilazimishe tupende ladha za generation zako.

Ata bongo fleva ya zamani sio ya leo bongo fleva ya sasa imetawaliwa na Mapiano.
 
Hii redio 2014 kurudi nyuma kwangu mimi ilikuwa bomba sanaaa burudani na mizaha ya kipindi kile ili nibamba sana tofauti na sasa hv 😆🤣😂

Sasa hivi imepoteza uelekeo haijui NJIA ipi ya kuelekea na hao ndio watangazaji walio nao mkuu.
 
Mkuu unaonekana ni mtu wa kitambo sana na hii radio, niwe mkweli tu sio wa kitambo hivyo! Lkn sjawahi kuwa na wakati wa kupenda kusikiliza radio kama nilivyopenda vipindi hivi vya Clouds:-

JAHAZI
Ile ya kina Efraim Kibonde, Wasiwasi Mwambulambo na Arnod Kayanda aisee ilikuwa ikifika saa 10 jioni lazima nisikilize radio

AMPLIFAYA
Kipimdi kile inaanza ilikuwa ya moto sana, nimesikiliza jana kama dakika 2 tu nikazima radio haina content tena vitu vya kipuuzi kabisa anaulizwa Dogo Janja ashauri Fid kushirikishwa na Chino wana man amapiano yaani story za kubishana vijiweni ndio inakuwa content radioni, ilikuwa kidogo nilete thread humu niulize au mimi umri wa hivyo vitu umenitupa mkono

SPORT XTRA
Ile ya 2014 kurudi nyuma, japo inawezekana kupungua kwa ladha ya mpira hasa hasa EPL imenifanya nisiwe mfuatiliaji sana wa vipindi vya mipira

Upande wa tv (Clouds tv) Clouds 360 ile ya kina Babie Kabae, Hassani Ngoma na Sam Sasari ilikiwa inanibamba sana pia

Sasa hivi sio kuisikiliza Clouds tu sisikilizi kabisa radio karibia zote vipindi ni kama wamepewa content na mtu mmoja asubuhi ukiwasha radio karibia zote vipindi ni vile vile ikifika saa 8 mchana wote wana vipindi vya bongo fleva, jioni na usiku ni vile vile imefikia wakati watangazaji nao kama wanaigana style za kuongea

Yote kwa yote kuna yule wa wasafi fm ambae kila siku lazima atamke neno "stuff like that" kama mara 10 hivii sjui the mvp the half man duh! Tuna safari ndefu sana

Hakika kiongozi nimeanza kuskiliza tangu inaanzishwa ila ladha iliyokuwepo mwanzo na sasa hivi ni vitu viwili tofauti kabisa kiongozi.
 
Back
Top Bottom