CIA walimuua Bob Marley?

CIA walimuua Bob Marley?

Wafuatao ni wahanga wa mauaji yaliyofanywa na CIA
Bob Marley
JF Kennedy
Ernesto che Guevara
Patrice Lumumba
Hugo Chavez

Mku umenigusa sana hapo kwa patrice lumumba.matatizo yote yawakutayo wa congo leo chanzo kiku ndio hapo.

Ongezea unaowajua wengine...
 
Je unajua kwanin kundi la Fugees lilikufa? Google out, you will be surprised. Dunia inaongozwa na makundi makubwa na yenye nguvu hivyo wakikuhitaji na ukakataa kujiunga lazima wakutoe kafara tu.. So sad!
 
Waislamu wa wapi hao maana kuna washikaji zangu wengi Waislamu ni wapenzi wa Bob Marley.
Sema now days kuna mashehk wanaendesha mihadhara kuhusu hawa jamaa sasa kupitia mashehk ndo wamegundua maneno mengi katika nyimbo za Bob ni za kumsifu shetani.
Ila watu hawajui tu na hili haliko kwa Bob tu lipo karibu kwa wanamuziki wote kwa sa babu karibia wanamuziki wote wapo huko.
Mkuu nakupa hii link ina lyric za baadhi ya nyimbo za bob, niambie nyimbo ipi amemsifu shetani, pia waweza taja nyingine ambayo haipo kwenye list. Wajulishe hata hao mashehe

Jah Lyrics: Artist - Bob Marley & The Wailers Lyrics
 
mkuu huyu Culture ni solo artist ambaye alifia stejini nchini ujerumani na hao hao jamaa walihusika ktk kifo chake! ananyimbo nyingi sana baadhi ni Jah alone a christian,money girl,one stone,pay day.
hivi culture amekufa ?
 
James Brown (soul Brother No. 1) amefariki miaka ya hivi karibuni karne ya 21 muda mrefu tu baada ya kustaafu uimbaji kama ilivyo kwa Barry White. Hivyo kusema Brown aliuawa na "hao hao," inaweza isiwe sahihi. Bob Marley alikuwa mwanamapinduzi na nyimbo zake ziliashiria hilo. Marley alikuwa sauti ya wanyonge wa Carribean na weusi kwa jumla. Vuguvugu lao la "Rastafarian", halikusomeka vizuri katika siasa za miaka hiyo. Mtakumbuka Walter Rodney mwanamapinduzi toka Carribean (Mhadhiri UDSM miaka ya sitini kuingia sabini) mwana-Rastafari kutokana na kuvaa nywele zao, aliuwawa kwa kupigwa risasi kwa Guyana baada ya kujihusisha na siasa za huko. Kitabu chake "Jinsi Ulaya Ilivyodumaza Maendeleo ya Afrika", hakikuwavutia wakubwa wa magharibi. Ukiunganisha mzunguko huo wa akina Rodney, Marley na hapo nyuma George Padmore na Marcus Garvey na vuguvugu lao la "Turejee Afrika" unaweza ukakubali ya kwamba Marley aliuawa na wakoloni mambo leo na taasisi kaidi za zama hizo kama CIA kutokana na uanamapinduzi wake na mvuto mkubwa aliokuwa nao kwa vijana wanyonge weusi wa Jamaica na Afrika na Amerika ya Kusini.
Mkuu asante kwa ku-share na sisi
 
Kifo cha Bruce kilichangiwa na mambo mengi yote hayakuwa na uhusiano wowote na masuala ya CIA, kitu cha kwanza ni utumiaji wake mkubwa wa cannabis aliwahi kuonywa na Daktari wake alipo patwa na ugonjwa wa kifafa ghafla akiwa kwenye studio yake aki-dub film, alikaa hosptalini kwa muda baadae akaruhusiwa na kupewa mashariti ya kumeza dawa kila siku ili kudhibiti kifafa kisijitokeze tena, akaonywa kwa mara nyingine kwamba asiwe anatumia/vitu bhangi na dawa za kulevya haionyeshi kama alizingatia mashariti ya madaktari wake!!

Kitu kingine Bruce alikuwa anafanya mazoezi ya viuongo ambayo mengine yalikuwa hatarishi mfano: kutumia umeme kustimulate misuli, wakati fulani aliwahi kuhumiza mgongo wake akiwa mazoezini nadhani alikuwa yuko kwenye zoezi la kunyanyua vyuma kama nakumbuka vizuri, injuries alizo sustain madaktari wake walifikiri hataweza tena kusimama vizuri au kwendelea na michezo/mashindano ya Kung-Fung lakini wapi bwana Bruce bounced back, lakini akawa anaendelea kutumia dawa za kupunguza maumivu ya mgongo - tukiweka maanani idadi ya madawa aliyokuwa anameza kila siku - namely: Dawa za kudhiti kifafa, dawa za kupunguza maumivu ya mgongo na uvutaji/ulaji wa aina fulani ya bhangi yote hayo anayameza kila siku - mtu ungetegemea long term abuse ya nadawa hayo yangeleta nadhala gani eventually.

Kitu kingine Bruce alikuwa anapenda wanawake sana, kifo chake kilitokea akiwa nyumba ndogo, sasa tabia hii ni rahisi sana washindani wako kibiashala kuwatumia wanawake kukudhulu, Bruce alijua kwamba Studio yake na Raymond iliyokuwa inajulikana kama Golden Harvest ilikuwa na ushindani mkubwa na Studio za manyangumi wa Hong Hong wa familia ya Run Run Shaw (sijui kama jina nimepepatia) familia hiyo ilikuwa haipendi jinsi Studio za Raymond Chow na Bruce Lee zilivyo kuwa zimekuja juu kibiashara - wote tunajua Wachina walivyo vicious, wanaweza kufanya lolote kuondoa ushindani.

Now a million dollar question - Vitu gani vilichangia kifo cha ghafla Cha Bruce Lee?

* Binafsi nafikiri sababu ya kwanza inaweza kutokana na utumiaji wake wa madawa mengi kwa wakati mmoja, actually wanasena dawa aliyo pewa (Super Asprin) na mpenzi wake kuzuia maumivu ya kichwa ndio ilichangia kufanya ubongo wake uvimbe na kumsababishia kifo.

* Sababu ya pili, mpenzi wake anaweza kuwa ametumiwa na Kampuni ya Studio za Run Run Shaw kumuua Bruce baada ya kulipwa hela ndefu - kwa nini nasema hivyo: alipo hojiwa na Polisi baada ya kifo cha ghafla cha Bruce, mwanamke huyo majibu yake yalikuwa yenye utata sana, walimuhoji kwa nini Bruce alifia nyumbani kwa binti huyo kwenye kitanda chake - akajibu kwamba Bruce alipitia nyumbani kwangu akanambia anaunwa kichwa nikampatia Super Asprin ameze baadae nikampeleka chumba changu cha kulala nikampumzisha, baada ya hapo akwenda kumwangalia hali yake inaedeleaje mpaka masaa nane yakapita - alidai baadae kabisa alikwenda chumbani kwake akajaribu kumwamusha Bruce bila mafanikio, badala ya kuwasaliana ni mke wa Bruce alawasiliana na Raymond Chow ambae alikuwa ni Business partner wa Bruce, binti huyo hakutaka mkewe wa Bruce afahanu ukweli wa kile kilicho jiri - ndio maana alikimbiza mahiti Hospitalini!! Je hili lilikuwa jambo la kawaida kweli - I don't think so?
BIBLIA YASEMA.
Usiwe Mtumwa Wa Mali Na Kupoteza Maisha Yako.
 
Nchi za kibepari ndo zao

Thomas Sankara a.k.a "AFRICAN CHE GUEVARA" mwaka 1984 kama rais wa Burkina Faso aliuliwa kinyama sana na Makamu wake ambaye alikuja kuwa Rais wa Burkina Faso mpaka miaka hii ya karibuni Blaise Compaore

Sankara aliuliwa kwa kuwa tu alikuwa na "FIKRA ZA NCHI YAKE KUWA SELF SUFFICIENT" na kuachana na kuwategemea wafaransa kwa kila kitu mpaka kuagiza sukari na vyakula

wafaransa na Huyo Bazazi compaore wakamuulia mbali maana waliona ni bonge la Threat kwa uchumi wao

wakamkatakata vipande na kumzika kusikojulikana mpaka mwaka jana ndo kaburi lake limekuja julikana

Blaise Compaore kakimbilia uhamishoni Cote' de Voire baada ya kutaka kubadiri katiba atawale milele wananchi wakaandamana nchi nzima akatoka nduki

Thomas Sankara alikufa akiwa kijana mdogo sana rika la miaka 30
 
Wafuatao ni wahanga wa mauaji yaliyofanywa na CIA
Bob Marley
JF Kennedy
Ernesto che Guevara
Patrice Lumumba
Hugo Chavez

Ongezea unaowajua wengine...
Tafuta muvi maarufu inaitwa "CHE"

ya mwaka 2008, wakisha kudedisha wanaigiza movie wanauza Hollywood

Che Guevara kama Thomas sankara wa Burkina Faso walikuwa ni watu wa Kueliminate haraka sana....
 
Nchi za kibepari ndo zao

Thomas Sankara a.k.a "AFRICAN CHE GUEVARA" mwaka 1984 kama rais wa Burkina Faso aliuliwa kinyama sana na Makamu wake ambaye alikuja kuwa Rais wa Burkina Faso mpaka miaka hii ya karibuni Blaise Compaore

Sankara aliuliwa kwa kuwa tu alikuwa na "FIKRA ZA NCHI YAKE KUWA SELF SUFFICIENT" na kuachana na kuwategemea wafaransa kwa kila kitu mpaka kuagiza sukari na vyakula

.....
Unamtahadharisha Magu au unamtisha?
 
Kwenye maelezo yako yote sijaona ukitaja MAJANI„„„„kivipi?
Majani ni tiba ya cancer jiangalie aisee....raisi wa dunia obama mwenyewe kala jani itakua ww kimpapure...?
 
Back
Top Bottom