CIA walimuua Bob Marley?

CIA walimuua Bob Marley?

alikuwa na impact gani hadi wazee wa kazi a.k.a wazee wa mission CIA wamuue?????? au bange zake tu zilimzidia.
Ukisoma hili jarida la high times (lipo mtandaoni) utaona kwamba kipindi cha bob jamaica kulikua na vyama viwili vya siasa vyenye nguvu sana JLP na PNP, PNP kilikua na sera za Ki socialist wakati JLP sera zao zilikua za ki capitalist ambazo bob alikua haziungi mkono kwakua zilikua zina nyonya na kukandamiza wanyonge (babylonian system), sera hizi ziliungwa mkono na CIA kwakua ziliwapa fulsa mbalimbali.

Aidhaa bob alikua anaandaa matamasha ya bure jamaica na kufafanua madhara ya sera hizo za ki capitalist kwa njia ya nyimbo. Wajamaica walimpenda na kumuamini sana bob, jambo lililo wakwamisha sana JLP

BOB alinusulika kuuawa (ambush in the night) siku chache kabla ya tamasha lake la bure la smile jamaica lililokua na udhamini wa PNP, hii ilitafsiriwa na JLP kama kukipa kick chama cha PNP.
 
Wamejikomoa wenyewe,
Tunawashukuru kwa ku,uuwa Bob na kutuachia bangi zetu.Mbaya zaidi wangemuuwa Bob Marley na Wakamuuwa Bangi hapo wangenikera saaan
Msiovuta Bangi mnapata tabu sana,Sie wavuta Bangi tunawasiliana na Bob Marley na kuongea nae kama kawaida tu,na tunagonga tano.feelings za Ganja acha kabisa,yule jamaa mzimu wake upo pale.
Sasa ukitaka kuwasiliana na Bob na kupata ushauri wowote kutoka kwake,naomba tafuta Ganja kisha piga puri kama nne hivi,utaibukia Jamaica,Masharti yake tu mtu aiskustue wala kukusemesha wakati wa feelings,mwambie stim zinalipiwa.
Sasa kama wanaweza wauwe na Bangi.
ehhh,sasa ndio nimeandika nini !!!
 
Wakuu heshima kwenu.

Kwa muda wa miaka kama 20 hivi nimekua mshabiki na mfuatiliaji sana wa muziki wa reggae na waimbaji wake. Nimesoma taarifa mbalimbali juu ya waimbaji wa muziki huu hasa Robert Nesta Marley (Bob Marley) lakini leo nimekutana na taarifa iliyo nishtua kidogo juu ya kifo cha muasisi huyo.

Sote tunajua kwamba bob alifariki kwa kansa iliyo sababishwa na uvutaji wake wa bangi uliopindukia , lakini kwa mujibu wa jarida la high times, bangi haikusababisha kansa iliyomuua bob.

Jarida la ripoti kwamba kansa hiyo ilipandikizwa na aliejifanya muandishi wa habari kwa kumpelekea zawadi ya viatu vilivyo kuwa na waya ndani uliowekewa vimelea vya cancer, waya huo mlimchoma bob kidoleni alipokua akijaribisha zawadi hiyo aliyopewa, baadae mwandishi huyo alipochunguzwa aligundulika ana uhusiano na CIA waliofanya jaribio la kumuua bob (ambush in the night)

Bob kwa kujua alisha nasa kwenye mtego wa maadui wake waliokua wanamuwinda usiku na mchana aliamua ku -condense plan zake za muzik ili kufit ndani ya pindi kifupi cha uhai kilichabakia maana alijua hana muda mrefu wa kuishi, jimmy cliff msanii mwenzake anasema, bob alikua anakunywa chai na kula lunch kwapamoja asubuhi na kwenda mazoezi ya muziki siku nzima na hata usiku wa manane, ili kurekodi kila alichotaka kusema kwa njia ya nyimbo, hivyo jimmy cliff anaamini kwa kipindi hicho kifupi bob aliimba na kurekodi kila ujumbe aliotaka kufundisha kabla hajafa.

Pia moja ya madaktari waliokua wanamtibu bob alishangazwa na style yake ya uimbaji na ushikaji wake wa guiter (kama SMG) katika concert yake ya mwisho, hasa jinsi bob alivoimba wimbo wa REDEMPTION SONG,

"....these songs of freedom is all I ever had"

Daktari huyo alihisi maumivu makali (kutokana na kansa) aliyokua nayo bob kwa jinsi alivyokua akishika paji la uso mara kwa mara, baadae daktari huyo alikiri kwamba bob aliandaa concert hiyo maalum kwaajiri ya kuwaaga rasmi washabiki wake na kusisitiza mambo ya msingi ya kisiasa, kwani afya yake haikuruhusu kabisa.

Bob na timu yake walipokua kwenye mechi ya kirafiki kule ufaransa sote twajua aliumia kidoleni na kansa ikaanzia hapo, high times la endelea kuripoti kwamba kidole kile alicho umia ndicho kilicho chomwa na waya uliokua kwenye viatu, na mbaya zaidi akiwa uwanjani kuna daktari asiyefahamika alikuja kumchoma bob sindano (isiyofahamika) kwenye hicho kidole kama tiba. Lakini sindano hiyo inaripowa kuwa ilikua na lengo la kueneza viini vya kansa mwilini mwa bob. Kwa kweli nashindwa kuamini kama kweli CIA walimuua bob makusudi, sijui wadau mnalionaje hili.
Hapa duniani ukiwaambia watu ukweli wa mabaya yao na ukawachoma mioyoni mwao badala ya kuchukua uamuzi wa kubadilika wawe watu wema watakutafutia hata kifo,wazungu hawatupendi watu weusi hasa ukionyesha kua ni mtu mwenye kuweza kufikili kwa kina na kutenda jambo kama wao au zaidi ya wao.inawezekana kweli ikawa hivyo.
 
Mkuu kama MAJANI unamaana ya bangi, nimetaja
Ila kama unamaanisha producer MAJANI a.k. unywele mmoja kweli sijataja

Mambo ya Cia yanakujaga kimbele nyuma.Ebola ilipoanza W.Africa tukaona N.Korea wakaweka mabango kwenye migahawa ya kuzuia African wasiingie,nje ya pazia ilikuwa kama ubaguzi, lakini baadae ndo tikajua kwamba N.Korea ndio waliolengwa Africans ni wahanga.
Yawezekana kunakitu kipya inaanza kupandwa ili kututoa kwenye hoja ya bangi.
Sababu alizoziweka na muandishi ni zakawaida kabisa.kwavyovyote mtu ukishajua utakufa siku chache zilizobakia lazima uende race.
 
Back
Top Bottom