Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,095
- 159,977
ALBAMU ya reggae ya mfalme wa muziki wa reggae, hayati Bob Marley, ‘One Love’, imetunukiwa Tuzo ya Albamu Bora ya Reggae katika Tuzo za Grammy za 67, zilizofanyika usiku wa jana huko Los Angeles. Albamu hiyo ilizinduliwa Februari 2024 na Island Records, ikiwa na nyimbo 10 maarufu za Marley, ikiwa ni pamoja na ‘Natural Mystic’, ‘Exodus’, ‘Waiting in Vain’, ‘Redemption Song’, na ‘One Love’.
Miongoni mwa wasanii walioshirikiana kwenye albamu hii ni mjukuu wa Marley, Skip Marley, Daniel Caesar, Kacey Musgraves, Wizkid, Jesse Reyez, Leon Bridges, na Bloody Civilian. Albamu ilishinda dhidi ya uteuzi mwingine mkali, ikiwa ni pamoja na ‘Evolution’ ya The Wailers na ‘Never Gets Late Here’ ya Shenseea.
Ingawa Bob Marley hakuwahi kushinda Grammy wakati wa uhai wake, urithi wake umeheshimiwa kwa njia hii baada ya kifo chake, akiwa ametunukiwa Tuzo ya Mafanikio ya Maisha ya Grammy mwaka 2001 na tuzo kadhaa za Albamu Bora ya Reggae.