MGILEADI
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 1,621
- 1,545
Malcom X ingawa familia ya malcom inaamini national islam(NI) ndio wamehusika kumuua, one member of NI john ally was undercover spy of FBI
Majuzi tu miaka ya karibuni Louis Farakhan, kiongozi wa sasa wa Nation of Islam (NI), alikiri mbele ya Binti wa Malcolm X kuwa maneno yake, yalichochea chuki baina ya wafuasi wa NI dhidi ya Malcolm X, ingawa yeye binafsi hakuhusika na mauaji hayo (You Tube Louis Farakhan na Binti wa Malcolm X). Lakini tunajua miaka hiyo, dola ya Marekani ilikuwa ikipambana na vuguvugu la Waamerika Weusi la kudai haki sawa za kiraia. Miaka hiyo Simba/Chui Weusi (Black Panther Party for Self Defence) ya akina Huey P Newton, Bobby Seale na kina Eldridge Cleaver ilikuwa kazini sana tu katika mitaa ya Oakland na kuwa tishio kwa mfumo mzima wa ukandamizaji wa haki za watu weusi Marekani. Katika mazingira hayo Malcolm X aliuawa, George Jackson pia akifia gerezani Soledad, Angela Davis akatiwa ndani na Martin Luther King akapigwa risasi. Unaweza kusema yalikuwa mauaji ya kisiasa. Unajua adui wenu atatumia matatizo yenu kuwamaliza yeye akikaa mbali. Kifupi, lilikuwepo shinikizo kubwa sana la kisiasa dhidi ya ustawi wa dola ya Marekani kwa ndani muongo huo. Lilikuwepo tatizo la vita vya Vietnam kupingwa kwa nguvu nchini, Muhammad Ali (Cassius Clay) akigoma kwenda kupigana huko, na kibaya zaidi Tommy Smith na mwanariadha mwenzake Mmarekani mweusi pia, wakipiga saluti ya "Nguvu ya mtu Mweusi" yaani Black Power, baada ya kupokea medali zao katika michezo ya Olimpiki huko Mexico mwaka 1968. Hilo liitokea huku bendera ya Marekani ikipandishwa na ulimwengu mzima ukiona. Jambo hilo lilileta hasira kuu kwa dola ya nchini mwao. Sasa katika mazingira ya jinsi hiyo Malcolm X (ama Abdul-Malik Al- Shabbaz) aliuawa na wengi wanaamini alikufa kwa sababu ya kupishana na wenziwe ndani ya jumuia ya NI. Yeye alipenda NI ijielekeze zaidi kwenye mrengo wa kidini wa Uislamu wa Mashariki ya kati (hususan Uislamu wa Sunni baada ya kwenda hija huko miaka michache kabla hajauliwa), ambapo viongozi wengine walitaka wadumishe desturi ya mwasisi wa imani yao huko Marekani, Elijah Muhammad.