Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Pamoja na kwamba unayosema ni kweli mtupu ila kumbuka pia kuwa ubadilihsaji wa makocha ndio unatupa kutamba mitaani kwa makombe tunayobeba. Kuna timu zinakaa na kocha hadi inabandikwa tags kwamba wao hawanaga plan za kubeba makombe. Hiyo hiyo presure atakuja nayo Graham Potter usishangae akabeba EPL au UCL

Bahati mbaya tuliyonayo Chelsea ni dressing room
Makocha tunaowaajiri hawajui kuidhibiti dressing room
Aliweza kidogo Sarri ila naye akatimua kabla hajafukuzwa, japo mimi ningeamini Sartri angekaa muda mrefu kwa sababu alikuwa ana hekima ya kudela na dressing room
Ila hawa wengine wakiongozwa na MOU, Conte na huyu kichaa TT wamefeli hapo Dressing room. Tuseme ukweli
Babu sarri hadi keppa alimgomea mzee wa watu akauchuna issue ikaisha
 
Sioni Potter akibeba kikombe chochote THE BLUES kabla ya kufukuzwa

Sioni Pochetino akibeba kikombe chochote THE BLUES kabla ya kufukuzwa

Ila namuona Zidane akibeba kikombe ndani ya kwa msimu mmoja tuu kabla ya kufukuzwa.
Kiongozi napingana na wewe, Graham atabeba na atapata mafanikio makubwa ndani ya Chelsea changamoto nisiyoweza kuitabiri kama ataiweza ni Dressing Room tu
 
Inatoweka vipi wakati ndio kwanza usajili umemalizika?!
Mnaweza poteana mazima sasa.
Kuna mambo mengi yaliyojitokeza hata kabla ya TT kufukuzwa kwanza kilikuwa na mvutano kuhusu Lukaku wa Wamiliki na TT, Ronaldo na treatment ya TT dhidi ya wachezaji vijana kuwa mbovu, pamoja na mivutano hiyo the end Wamiliki wakaamua kushusha mabega chini na wakamtii TT ili waone TT ataipeleka wapi team msimu ulivyooanza team ikawa achezi vizuri si tu hatupati matokeo mazuri pekee hata uchezaji wetu ni mbovu, kuna wakati baadhi ya wachezaji wakawa wanalalamika mbinu za kocha, TT pia akawa awaamini vijana japo kasajiliwa na Wamiliki na siku zinavyozidi TT anadizi kupoteza dress room na huku akiendelea kupata matokeo mabaya.Baada ya Wamiliki kuona sera yao ya kutengeneza kikosi kizuri chenye mkusanyiko wa vijana na wakongwe hawaoni ikifanyika chini ya TT na mambo mengine niliyotaja ndio wakaona muda sasa wakufukuza
 
Sioni Potter akibeba kikombe chochote THE BLUES kabla ya kufukuzwa

Sioni Pochetino akibeba kikombe chochote THE BLUES kabla ya kufukuzwa

Ila namuona Zidane akibeba kikombe ndani ya kwa msimu mmoja tuu kabla ya kufukuzwa.
Kwa msim 1 huenda asilete ila kwa misim 2-3 atakuwa ashaleta,

Shida ni dressing room kama ataweza idhibiti au akapata support ya wamiliki anaweza tupa mafanikio
 
Haonyeshi dalili nzuri?
Amewafikisha Carabao na FA final.. Wote tulishuhudia mtanange ulivyochezwa hadi dakika 120..Tumeangalia ile mechi nikiwa nimeshika moyo.
Ni vile tu bahati haikuwa upande wenu kwenye penalties.

EPL kawafikisha top 5,
Uefa nusu fainali ..Madrid akawazidi kidogo tu ..Hata sisi ile nusu fainali tungekuwa kundi mlilopangwa basi tusingetoboa.

Leo mnasema hajaonyesha dalili nzuri?
Saint Anne Mashabiki wenzangu wengi wa Chelsea hakuna wanalojua kuhusu mpira wao wanataka ushindi tu. Mpira ni mbinu ukizidiwa unapigwa kweli kweli kama mlivyopigwa jana na Napoli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom