Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Mambo kadhaa niliyogundua kwenye mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Leicester City.
.
.
Yule beki wa kati wa klabu ya Leicester City, Caglar Soyuncu, ni moja ya beki mzuri ana umbo zuri la kucheza mpira ya juu Giroud, na Abraham, walikuwa wanapata wakati mgumu sana kucheza mpira ya juu [emoji119] nina asilimia 80 anaweza kuziba pengo la Harry Maguire.
.
.
Tangu msimu uliopita apewe timu Brendan Rodgers, ni mwalimu wenye falsafa ya kuchezea mpira kumiliki Leicester kutoka kwenye kucheza mpira direct football mpaka kwenye mpira wa possession football amenikumbusha alivokuwa akihifundisha Swansea ikapewa jina la Swansealona [emoji119].
.
.
Kipindi cha kwanza Brendan Rodgers, alificha makucha yake kucheza kwa tahadhari kubwa na kuonekana na kumuacha Jamie Vardy, peke yake nyuma kama anazurura vile.
.
.
Maddison, yule anaevaa namba 10 wa Leicester City, ni mchezaji mzuri wenye spidi nguvu ana uwezo mkubwa ngome ya Chelsea, ilikuwa inapata wakati mgumu sana kumzuia.
.
.
Willian, bado ajawafiti ametoka majeraha mechi ilikuwa ina kasi sana muda mwingi alikuwa anachelewa kufanya maamuzi pale anapokuwa na mpira.
.
.
Kumtoa Jorginho, Frank Lampard, alifeli alikuwa anatuliza timu akiwa na umri kumuingiza Kovacic, maana yake anakwenda kuongeza nguvu ya kushambulia na kuwapa upenyo Leicester City.
.
.
Zouma naona anazidi kubadilika Siku hadi siku zinavosogea tofauti na mwanzo anaweza baadae huko mbeleni kuwa tishio.
.
.
Mwisho Lampard, unahitaji uwe na plan B kuanzia dakika ya 70 wachezaji wa Chelsea karibia wote walikuwa washachoka hii huenda ikakugharimu.

AROON
 
Hahaha tumpe muda bwana Lampard maana tumecheza mpira mzuri sana

Na kwakweli lengo letu ni mpira mzuri kwanza, hayo magoli badae sana 😊😊😊
 
2 points dropped. Actually hata hiyo moja ni bahati maana zile counter attacks za Leicester zilikuwa za kiwango cha Stigler Gorge. Nadhani kuna haja ya kuhakikisha Batshuayi anabaki tu. Tammy na Giroud hawatupeleki popote
Pale mbele hatuna mtu, na nyuma pia tunamhitaji Rudiger haraka sana
 
Naona umepanik ,kawaida tu ,mbona wenzako wakiona hali ngumu, wanajipiga ban
Nilishawaambien mpaka mech ya 10 , mkiingia top 6 bas mnaenda kuchukua EPL
Mna mech na Norwich & shefflied , mkishindwa kubeba point 6 nabadil mawazo, mnashuka daraja maana mtakuwa bado mnakibarua na kina Everton ,Watford , wolves hapo sijataja top 6 ambao mtawagawia point 4-6 kila mmoja
Aisee huna hata faraja kwa mgonjwa?
#Mwakawatabu
 
Tumefungwa wadau na hasa kipindi cha pili tumezidiwa na sababu hasa ni;
1. Wachezaji wametumia dk 120 kucheza dhidi ya timu nzuri katikati ya wiki

2. Leicester ni timu nzuri na inacheza vizuri hasa katikati

3. Leicester wana kocha mzoefu anayejua kucheza mechi kubwa.

Mimi kwangu bado naona huu ni mwanzo kujua kama timu ni nzuri mbaya. Nimejipa mechi 10 kufanya evaluation.
Mechi 10 kufanya evaluation wenzio wanachukua point?? Pre season ulikuwa unafanya nini sasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom