CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,754
2,000
7808A1B2-55A4-46B4-B470-F0F48AAC2B7C.png


Amesisitiza kuwa Serikali imeamua kutowazuia Watu ndani ya nyumba zao wala kufunga mipaka kwa kutambua madhara mkubwa yanayoweza kutokeza kwa kufanya hivyo.

Aidha, amesema madhara hayo yanaweza pia kuziathiri nchi 8 ambazo zinatengemea kupata huduma na bidhaa kupitia Tanzania hususan bandari ya Dar es Salaam.

Lakini pia amebainisha kuwa kutokana na madhara ya #CoronaVirus upo uwezekano mkubwa wa kutokea kwa upungufu wa chakula, hivyo amewataka Wananchi kuzalisha chakula cha kutosha.

Pia, amesisitiza Wananchi waendelee kuchapa kazi kila mahali walipo huku wakichukua tahadhari ya kutokuambukizwa kwa kufuata ushauri wa Wataalamu na pia wasisahau kumuomba Mungu atuepushe na janga hili.

Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Waumini wa Kanisa Katoliki katika Parokia ya Mlimani, Wilayani Chato mkoani Geita ambapo alihudhuria ibada ya Ijumaa Kuu.

EVQjmqDXsAMMAmD.jpg


FB_IMG_1586538003505.jpeg
FB_IMG_1586538001175.jpeg

Rais wa Tanzania, John Magufuli akiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chato mkoani Geita leo. Picha na Ikulu
 

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
3,294
2,000
Mbona kama yuko peke yake? Usalama wa viongozi wa kitaifa ni usalama wa taifa, ndio maana makamu wa rais na rais kipindi hiki lazima wana usalama wahakikishe wako salama kiafya ili taifa liwe salama, hawaonekani mara kwa mara wakiwa wamejichanganya katika jamii
Peke yake bila nani mkuu

Humuoni huyo jamaa kushoto kwa Rais hapo? Humjui huyu? Hata kama humjui mkuu hushangai yeye hafungi macho kanisani?
 

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
3,887
2,000
Rais Magufuli amesema Serikali imeamua kutowazuia watu ndani ya nyumba zao wala kufunga mipaka kwa sababu ya ugonjwa wa corona kwakutambua madhara yanayoweza kujitokeza kwa kufanya hivyo ndani ya nchi na kwa nchi 8 zinazotegemea huduma na bidhaa kupitia Tanzania

My take:
Huu ndio ukweli,tukifunga mipaka tutaathiri watu wetu na majirani zetu,viva jpm viva CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,605
2,000
Makanisa, Miskiti yote ingefungwa. Ningepiga marufuku abilia kuingia na kutoka Dar, Mipaka yote ingefungwa isipokuwa wanaoleta chakula, dawa na bidhaa muhimu, Kumbi zote za starehe zingefungwa kila mlevi anunue pombe dukani akanywe kwake.

Mishahara yote ya umma ambayo ni kuanzia milion 3 ingekatwa 50% ili kununua chakula kwa watu masikini.
 

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
8,350
2,000
digba sowey, Kuna wakati ambapo tunatakiwa kujitenga na ujinga na uwendawazimu. Hii kauli imetolewa na Rais wa nchi kwaajili ya Taifa zima. Ilitosha kuifikisha taarifa hii kwa umma kwa namna hiyo tu. Ujinga na uwendawazimu ni kuihusisha kauli hiyo na CCM.

Na wala hakukuwa na sababu za kutoa pongezi juu ya kauli ya Mh. Rais kwa kauli hiyo.

Tupo mahali ambapo tunakiwa kuamua tupite njia ipi - ndani ya mto ambako kuna mamba au nchi kavu kwenye simba. Kiongozi akisema tuvuke mto wenye mamba au nchi kavu, sidhani tunahitaji kupongeza. Hapa ndipo tunasema, kupanga ni kuchagua. Chaguo lolote tutakalochukua, kuna madhara. Sasa ni kuamua tuyakubali madhara gani.
 

BENNICK

JF-Expert Member
May 2, 2013
531
1,000
Wataathirika vipi mkuu, hebu dadavua.
Nijuavyo mimi lengo la kufunga mipaka ni kudhibiti human interaction, na sio cargo services and logistics.

Huduma za mizigo zinaweza kuendelea ( with caution ,kama ku limit cargo vehicles ziwe na Dereva na tingo tu na kuimarisha screening services kwenye borders) na ni rahisi ku control kuliko ukiacha mipaka wazi kabisa, hizo nchi nane zinazo tutegemea raia wake wanaweza wakafika bila kupitia Tanzania land.

Nchi kama New Zealand wamezuia raia yeyote asiye mkazi wa pale kuingia nchini for almost two months na juhudi zao zimeanza kuzaa matunda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom