Chibudee
JF-Expert Member
- Dec 28, 2016
- 1,775
- 2,397
Amesisitiza kuwa Serikali imeamua kutowazuia Watu ndani ya nyumba zao wala kufunga mipaka kwa kutambua madhara mkubwa yanayoweza kutokeza kwa kufanya hivyo.
Aidha, amesema madhara hayo yanaweza pia kuziathiri nchi 8 ambazo zinatengemea kupata huduma na bidhaa kupitia Tanzania hususan bandari ya Dar es Salaam.
Lakini pia amebainisha kuwa kutokana na madhara ya #CoronaVirus upo uwezekano mkubwa wa kutokea kwa upungufu wa chakula, hivyo amewataka Wananchi kuzalisha chakula cha kutosha.
Pia, amesisitiza Wananchi waendelee kuchapa kazi kila mahali walipo huku wakichukua tahadhari ya kutokuambukizwa kwa kufuata ushauri wa Wataalamu na pia wasisahau kumuomba Mungu atuepushe na janga hili.
Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Waumini wa Kanisa Katoliki katika Parokia ya Mlimani, Wilayani Chato mkoani Geita ambapo alihudhuria ibada ya Ijumaa Kuu.
Rais wa Tanzania, John Magufuli akiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chato mkoani Geita leo. Picha na Ikulu