CHADEMA yatangaza kumwaga mishahara kwa watendaji wake wote kuanzia ngazi ya chini Kabisa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,651
218,131
Kauli hii ya kishujaa imetolewa na Mwamba Mwenyewe Freeman Mbowe alipokuwa anahitimisha mpango wa Operesheni Haki Mkoani Morogoro.

Mbowe ambaye sasa anaitwa Mtemi Isike, baada ya kusimikwa huko Tabora , amesema kwamba Chama chake sasa kinataka viongozi wake wafanye kazi moja tu ambayo ni kusuka chama kwa kukusanya wanachama wapya na kuhudumia wanachama wake 24/7 , hivyo ni lazima wapewe vitita vizito kila mwezi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Kwa kadri ya kumbukumbu zangu CHADEMA yaweza kuwa ndio Chama cha kwanza cha kisiasa nchini Tanzania kuwalipa wafanyakazi wake wote hadi wa ngazi ya chini kabisa Mshahara, vyama vingine watendaji wake wengi huishi kwa kutegemea RUSHWA ZA WAGOMBEA WAKATI WA CHAGUZI za ndani au Uchaguzi Mkuu.
 
Makamanda uchwara wanapiga miayo tu.
20210527_213348.jpg
 
Kama tulishindwa kutoa mishahara kipind kile tukipata ruzuku kubwa tutaweza Sasa kweli na je zoez litadumu kwa mda gani?

Chama changu nakipenda Sana lakn kwa hili mh?
 
Back
Top Bottom