Wana CHADEMA wataka kufanyike ukaguzi maalum wa fedha na mali zote za chama

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,279
9,717
Ndugu zangu Watanzania,

Ni kama wanachadema wameanza kuzinduka kutoka katika usingizi walikokuwa wamepigwa sindano ya ganzi katika akili zao, ni kama wameanza kuukataa na kuukana unyumbu na ukasuku, ni kama akili zimeanza kuwakaa sawa na kuwarudi, ni kama wamechoka kuburuzwa na kuswagwa kama ng'ombe.

Ni kama wamekamuliwa mpaka damu na kuishiwa nguvu, ni kama wamelishwa unga wa rutuba uliowazindua akili zao, ni kama wameanza kufikiri kwa kutumia akili zao wenyewe na ni kama wamechukuwa kwa nguvu akili zao kwa viongozi wao waliokuwa wameziweka kabatini na kufikiri kwa niaba yao.

Sasa wameamka na wamechoka kufanywa mahayawani na manyumbu. Wanataka kufanyike ukaguzi maalumu wa fedha zote ambazo chama kimekuwa kikipokea ikijumuisha Ruzuku, michango ya wanachama, wadau, wahisani na wakereketwa mbalimbali.

Wanataka wajuwe mali za chama zipo wapi na zimeandikwa majina ya nani na zilinunuliwa kwa utaratibu upi na ikiwa mali au vitu vinaendana na uhalisia na thamani ya fedha zilizolipwa na chama.

Wanataka wajuwe wakati wote ambao chama kilikuwa kinapokea mamilioni ya fedha kama Ruzuku zilifanya kazi gani? Zilijenga nini na wapi?

Kwa kuwa wakati wa uchaguzi wagombea ubunge majimboni walikuwa na wamekuwa wanategemea michango ya wanachama na wakereketwa kuwawezesha na kuwasaidia kifedha kipindi chote cha kampeni pasipo msaada wa chama makao makuu, licha ya kwamba chama kilikuwa kinapokea Ruzuku za mamilioni lakini pesa zilikuwa hazishuki wala kufika kwa watendaji wa ngazi za chini huku mikoani zaidi ya hesabu zake kuanzia na kuishia makao makuu tu.

Wanachama wa CHADEMA wanataka kujuwa fedha za join the chain zipo wapi? Zilipatikana kiasi gani?zilifanya kazi gani na kwa utaratibu upi? Wanachadema wanataka pia kufahamu utaratibu wa kukodisha helikopta upoje?

Maana ukodishaji huo umeonekana kama uchochoro wa upigaji ,ufujaji na utafunaji wa pesa za chama bila jasho.wanataka kufahamu nani anayetafuta helikopta? Mapatano yapoje juu ya gharama za ukodishaji na uendeshaji? Kampuni ngapi zinakodisha na unafuu wa bei upoje ukilinganisha na huko wanakochukua na kukodi kwa sasa ambako kumeonyesha kukinyonya damu na kukikausha chama kifedha?

Mimi binafsi Lucas Mwashambwa nawaunga mkono wanachama hao wa CHADEMA ambao wamekuwa kama manyumbu kwa miaka mingi, waendelee kudai haki ya uwazi juu ya matumizi ya pesa za chama, waache unyumbu na ukasuku.

Kikubwa ni kuungana dhidi ya wale wachache ndani ya chama ambao wamekuwa wakifaidika na Minofu minono na laini ya jasho la wanachama wasikubali hawa wachache waliokatika meza ya wafalme wawavuruge katika adhima yao hiyo ya kudai haki yao.

Lakini nawasihi wanachadema wote mliochoshwa na ubabaishaji uliopo ndani ya CHADEMA kuwa jikusanyeni na karibuni sana ndani ya CCM Chama ambacho kimejaa uwazi, uadilifu na uaminifu katika uendeshaji wa shughuli zake za chama.

Ndio maana huku CCM hamsikii habari za ubadhirifu wa mali za chama. Ndio maana mnaona chama kikiwa na ofisi za kisasa kila sehemu, kina ofisi za makao makuu zenye hadhi ya kisasa kabisa na zenye kila kitu, tofauti na ninyi huko CHADEMA mnaoendelea kuwa katika kibanda kisichoendana na Ruzuku mliyopokea kwa miaka mingi sana.

Amkeni enyi wana CHADEMA mliobakia katika usingizi, teteeni chama chenu dhidi ya fisi wanaokitafuna na kukifanya kama mradi binafsi wa kukopea hadi pesa na kukiweka kama mdhamana sokoni. Amkeni msiwe kama manyumbu na mahayawani huku mkiendelea kuangamia.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Acha kujidanganya mkuu, kwa sasa hakuna mwanachadema anaeweza kuzinduka kutoka katika mtego wa Mbowe wa kuwageuza mazuzu.

Nasema hivi kwa sababu inaaminika kuwa yule jamaa aliemfanyia Mbowe mpango wa kuwageuza wanachama wake mazuzu ameshafariki. So itakuwa ngumu wanachama hao kuzinduka na kuanza kuhoji hela anazokwapua mwenyekiti wao.

Labda hilo linaweza kufanyika mbinguni, lkn sio hapa duniani. Mbowe bado anatawala na kutembea na akili za misukule yake mfukoni kwake apendavyo.

Kama unabisha subiri uone mazuzu hayo yatavyokuja kukushambulia hapa jukwaani 🤣🤣
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ni kama wanachadema wameanza kuzinduka kutoka katika usingizi walikokuwa wamepigwa sindano ya ganzi katika akili zao,ni kama wameanza kuukataa na kuukana unyumbu na ukasuku, ni kama akili zimeanza kuwakaa sawa, ni kama

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
We una akili kuliko CAG anaefanya ukaguz kila mwaka.

Jinga kubwa.

Mbo huulizi za ccm.

Hebu nenda mbweni na bunju uone mwenyekiti na katibu wenu alivyojenga majengo makubwa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ni kama wanachadema wameanza kuzinduka kutoka katika usingizi walikokuwa wamepigwa sindano ya ganzi katika akili za

0742-676627.
S soma gazeti la mwanamchi ukurasa wa 22 na 23 la tarehe 14/11 kampuni zinazomilikiwa na kinana
SHRAFF SHIPPING AGENCY ipo TALL building gerezabi

Na African shipping ltd ipo TALL building pia mshenzi wewe huangalii kunavyoungua huko kwako majizi wakubwa ninyi
 
nyumbu wewe soma gazeti la mwanamchi ukurasa wa 22 na 23 la tarehe 14/11 kampuni zinazomilikiwa na kinana
SHRAFF SHIPPING AGENCY ipo TALL building gerezabi
na African shipping ltd ipo TALL building pia.
mshenzi wewe huangalii kunavyoungua huko kwako majizi wakubwa ninyi
Hilo gazeti na hiyo mada iweke kwenye uzi wako ili tujadili.maana huu uzi unahusu wanachama wa CHADEMA wanaotaka kufanyika kwa ukaguzi maalumu ndani ya chama chao.
 
Kisa kile kibanda!
Huyu mtu kumbukeni ni mfanyabiashara mkubwa tu!
Kwanza ukitembelea kule migombani hii nyumba ni ya kawaida kabisa enyi viumbe mliolaaniwa!
Kibanda hakiwahusu wanachadema.wao wanachotaka ni kile kidogo wanachotolea jasho lao bila kujalisha ukubwa wake.wanataka kujua kinatumikaje? Kimefanya nini ? Chama kina nini mpaka sasa? Kwanini hakina hata ofisi mikoani? Kwanini kinashindwa hata kulipa kodi ya ofisi huku mikoani?
 
Naona sindano imegonga mfupa,
IMG_20231114_121418.jpg
 
Back
Top Bottom