Taasisi zote makini za kijamii huweka misingi imara ya itikadi zao kuanzia kwa watoto. CHADEMA jifunzeni kwa chipukizi CCM

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,303
Kwa siku kadhaa nimeshangazwa na wafuasi wa chama cha Mbowe kushambulia idara ya chipukizi iliyo chini ya UVCCM kana kwamba ni jambo la ajabu sana kuwahi kufanyika. Wanaoshangazwa na uwepo wa chipukizi wanatakiwa kujikumbusha kuwa chipukizi CCM haijaanza leo. Ni idara ambayo ipo kwa miaka mingi kwenye awamu zote. CCM imara inajengwa kwa mambo mengi sana kuliko wafuasi wa Mbowe wanavyodhani.

Taasisi zote za siasa, dini na zingine zote za kijamii zinazohusisha watoto huwa zinakuwa na programs maalum za kuwafundisha watoto itikadi zao na maono ya hizo taasisi. Kwa mfano kanisa la kisabato wana idara za PF na Adventures kwa ajili ya kuwanoa watoto. RC, KKKT, na madhehebu mengine nao wana programs zao kwa ajili ya watoto. Wenzetu waislamu wao wako makini kabisa kwa kuwa na madrasa. Watoto ndo Future ya taasisi hivyo ni muhimu kuwakuza wakielewa mwelekeo wa taasisi. Vyama vya siasa navyo pia hufanya hivyo.

Badala ya kuiongelea Chipukizi CCM ninawashauri CHADEMA wajitafakari na kuangalia namna gani wanaweza kuandaa viongozi wa baadae. Inachosha kila siku tunasikia Mbowe, Lema, Lissu, Sugu, Heche, Msigwa, Mnyika na John Mrema. Ni ngumu kusikia jina jipya limechomoza. Hao BAVICHA hawana makali mbele ya hao mafaza. Yaani hao mafaza ndo BAVICHA pia. Uimara wa chama ni wanachama wake na sio vinginevyo.

Mwisho ninawashauri CHADEMA impe kazi komredi Lucas mwashambwa kuwapa semina BAVICHA ili kuzidi kujiimarisha kisiasa. Mwashambwa ni kijana mzalendo mpenda nchi yake kwahiyo sidhani kama atakataa kuwanoa BAVICHA.
 
Hawa siyo watoto bali ni watoto wao
kama hivi

JamiiForums-787880945.jpeg
 
..kwenye nchi za wenzetu watoto wanafundishwa mambo ya maana yanayokuza vipaji vyao.

..Uvccm ni matunda ya Chipukizi. Sasa sidhani kama kuna mtu yeyote makini anayependezewa na Uvccm, au ana Amini wana msaada kwa taifa.
Kuwaweka watoto kwenye ideology ya vyama ni kuua umoja wa kitaifa...Hili jambo liangaliwe na vyombo vya usalama, Leo inaonekana sawa kesho hawa Wanaweza geuka kuwa magaidi kwakukosa kile walichoaminishwa.

Tuwajenge watoto wetu katika utaifa na core values zetu siyo ideology ya vyama ambavyo muda na wakati unaongea kuwa mambo yamebadilika sana
 
Ajabu ni pale ambapo JPM alikua ananunua watu waliopikwa vema,kutoka CHADEMA kama akina David Silinde,Lijuakali na wengine wengi na kisha kuwapa vyeo mara tu walipoingia CCM na kuwaacha hao UVCCM lialia wakikodoa macho,kwani wanaonekana ni MACHAWA tu,wasiokua na chochote vichwani mwao.Angalieni namna njema ya kuwanoa.
 
Onyesha mtoto wa Balozi wa nyumba 10 au Mwenyekiti wa tawi wa CCM anayegombea hapo, hapo jamaa wanasimika mizizi pindi wakiiba wasisumbuliwe baadae
 
Kuwaweka watoto kwenye ideology ya vyama ni kuua umoja wa kitaifa...Hili jambo liangaliwe na vyomno vya usalama, Leo inaonekana sawa kesho Hawa Wanaweza geuka kuwa magaidi kwakukosa kile walichoaminishwa.

Tuwajenge watoto wetu katika utaifa na core values zetu siyo ideology ya vyama ambavyo muda na wakati unaongea kuwa mambo yamebadilika sana
Viko sehemu gani?
 
Mtahangaika na chipukizi ila Viongozi Bora wapo CHADEMA. Ilibidi awamu ya tano waingie gharama za kurudia uchaguzi ndogo ili kupata Viongozi Bora kutoka CHADEMA. Hao chipukizi walikuwa wapi?. CCM kwa Sasa inawatamani akina Halima Mdee wahamie huko iwape vyeo. CHADEMA ipewe heshima yake.
 
Ccm wanalazimisha mambo ambayo yanakuja kuwasumbua huko mbeleni. Leo hii siasa zimepigwa marufuku chuoni baada ya ccm kuzidiwa ushawishi wa kisiasa. Na hata Sasa wapinzani wakiianza kufanya kama ccm, na ccm wakiona wanafunikwa, utasikia wanatunga Sheria ya kutenga watoto na siasa!
 
Kwa siku kadhaa nimeshangazwa na wafuasi wa chama cha Mbowe kushambulia idara ya chipukizi iliyo chini ya UVCCM kana kwamba ni jambo la ajabu sana kuwahi kufanyika. Wanaoshangazwa na uwepo wa chipukizi wanatakiwa kujikumbusha kuwa chipukizi CCM haijaanza leo. Ni idara ambayo ipo kwa miaka mingi kwenye awamu zote. CCM imara inajengwa kwa mambo mengi sana kuliko wafuasi wa Mbowe wanavyodhani.

Taasisi zote za siasa, dini na zingine zote za kijamii zinazohusisha watoto huwa zinakuwa na programs maalum za kuwafundisha watoto itikadi zao na maono ya hizo taasisi. Kwa mfano kanisa la kisabato wana idara za PF na Adventures kwa ajili ya kuwanoa watoto. RC, KKKT, na madhehebu mengine nao wana programs zao kwa ajili ya watoto. Wenzetu waislamu wao wako makini kabisa kwa kuwa na madrasa. Watoto ndo Future ya taasisi hivyo ni muhimu kuwakuza wakielewa mwelekeo wa taasisi. Vyama vya siasa navyo pia hufanya hivyo.

Badala ya kuiongelea Chipukizi CCM ninawashauri CHADEMA wajitafakari na kuangalia namna gani wanaweza kuandaa viongozi wa baadae. Inachosha kila siku tunasikia Mbowe, Lema, Lissu, Sugu, Heche, Msigwa, Mnyika na John Mrema. Ni ngumu kusikia jina jipya limechomoza. Hao BAVICHA hawana makali mbele ya hao mafaza. Yaani hao mafaza ndo BAVICHA pia. Uimara wa chama ni wanachama wake na sio vinginevyo.

Mwisho ninawashauri CHADEMA impe kazi komredi Lucas mwashambwa kuwapa semina BAVICHA ili kuzidi kujiimarisha kisiasa. Mwashambwa ni kijana mzalendo mpenda nchi yake kwahiyo sidhani kama atakataa kuwanoa BAVICHA.

Umenena vyema kabisa ila chadomo watapinga.
 
Back
Top Bottom