DaveSave
JF-Expert Member
- Nov 20, 2010
- 440
- 634
Na Thadei Ole Mushi.
Ulishawahi kusikia Wimbo wa Mwamba Tuvushe ambao humwimbia Mbowe kipindi cha uchaguzi ndani ya Chama Hicho? Kama umewahi kuusikia basi wanachadema wanasababu za msingi sana kumwimbia Mbowe na kweli Freeman ni Mwamba.
Twende sawa hapa
Katika hali isiyotarajiwa mambo si Shwari sana ndani ya Chadema kwa kuwa kuna mvutano mkubwa wa ndani kati ya Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe na Tindu Lisu.
Ipo hivi.
1. Lisu anamtuhumu Mbowe kuwa amepewa magari Manne aina ya V8 nyeupe number E kama umeziona kwenye Ziara za Chadema. Lisu anadai kupitia Maridhiano Mbowe alihongwa Gari hizo ili asiisumbue Serikali. Ukweli ni Kwamba Mbowe Gari hizo ni zake Binafsi ambazo alizinunua kwenye Mnada kule Arusha tena kwa Bei Rahisi tu. Gari hizo ziliuzwa kwenye mnada wa hadhara za mali ya Shirika la Umoja wa Mataifa na Mbowe alitoa fedha zake kwenye account kuzinunua. Tuhuma za Lisu kwa Mbowe zinamkera sana Mwenyekiti na wawili hawa hawapo kwenye maelewano mazuri.
2. Jambo la pili linalochochea Mgogoro huo ni malalamiko ya Lisu juu ya Mwenyekiti kutumia Chopa kwenye ziara zake. Ikumbukwe kuwa Lisu na Mbowe wapo kwenye Ziara mbili Tofauti za kichama. Msafara wa Mbowe unatumia Chopa na Gari mbili V8 chini zinazobeba wasaidizi wake. Lisu anakalalamika kwa nini Mbowe atumie Chopa wakati yeye anatumia Magari mawili? Lisu anaona kama Mbowe anatumia Rasilimali za Chama kibaguzi. Ukweli ni kwamba Mbowe kwenye Ziara zake zote za Chama hatumii hata mia ya Chadema. Mwanzoni nilikuwa nakataa lakini nimefuatilia nikagundua ni kweli na kwa sasa Mbowe kasitisha Ziara zake yupo Moshi ana Mobilize fedha za kuendelea na Ziara. Kuna siku nilisoma andiko la Martin MM akimpongeza Mbowe kutumia Rasilimali za Famia yake kuendeshea chama nilimbishia lakini nimejionea mwenyewe.
3. Kwa sasa Lisu hana Shughuli ya kiuchumi ukiachana na Siasa. Lisu anamtuhumu Mbowe kuwa kazibwa Mdomo, na kwenye kikao cha ndani pale Morogoro Lisu alisema mbele ya Wajumbe wazi wazi kuwa “Mwenyekiti wenu kafungwa Mdomo” Lisu anataka kurudi zake nje ya nchi akafanye maisha kwa kuwa hapa nchini kwa sasa hakumlipi anataka Mbowe kama Mwenyekiti waanze harakati za kusumbuana na Serikali ili apate sababu ya kuondoka nchini hili nilishalitolea ufafanuzi kuwa Matusi ya Lisu ni njia ya kutaka kuondika nchini. Mbowe kamgomea kuleta tafrani na Serikali jambo hili limezidisha chumvi kwenye kidonda. Pamoja na Mbowe kukataa kuleta tafrani na Serikali anataka kurekebisha kauli yake kuhusu wazanzibari kuuza Bandari. Habari za ndani zinadai Mbowe ameshawaeleza watu wake wa karibu kuwa alichokisema hakutarajia kitaleta taswira hasi kama iliyopo na amepanga kutoka hadharani kurekebisha kauli yake hiyo.
4. Wanaomuunga Mkono Lisu ni Heche, Msigwa na Wenje ambaye Msimamo wake unayumbayumba. Hawa wana agenda kama ile ya Waraka wa Siri wa Zitto kabwe wa kutaka Mabadiliko ndani ya Chadema. Wanadai mwenyekiti kachoka anapaswa kuwapisha. Kizuizi kikubwa kwao ni wanachama wanampenda sana Mh Mbowe.
5. Wanaomuunga mkono Mwenyekiti ni makatibu wote wa kanda wa chama, wenyeviti wa kanda na Mikoa, makatibu wa Mikoa na jumuiya zote za Chama. Mbowe anapendwa sana ndani ya Chama chake kwa kuwa ana utu, na mara nyingine hutumia fedha zake kukisaidia chama na kusaidia watendaji wa Chama. Ukisikia wanaimba ule Wimbo wa Mwamba Tuvushe ni kweli wanaimba toka Rohoni sio kwamba kawanunua. Wanampenda sana.
6. Baadhi ya Viongozi wa Chadema wanamlalamikia Mwenyekiti kuhusu Kauli za Lisu dhidi ya Serikali zinafifisha mchakato wa Maridhiano ambayo yalikuwa yanawapeleka mahali pazuri. Viongozi hao wanamtaka Mwenyekiti achukue hatua za haraka kunusuru mchakato wa maridhiano ambayo ndani yake Chadema walikuwa wameshaanza kuona Mwanga. Kwenye Ratiba za Rais Samia angalau Kila Mwezi alikuwa anakutana nao mara Moja kuzungumza kuhusu maridhiano, toka Lisu ameanza matusi ni mwezi wa pili sasa hakijaitwa kikao hata kimoja cha Maridhiano, jambo hili linawasumbua sana viongozi wa chadema pamoja na mwenyekiti kwa kuwa wamepoteza.
7. Viongozi wa baadhi nikioongea nao wa chadema wanasema ili chadema ifanye Vizuri kwenye uchaguzi ujao ni Lazima Mbowe awe mgombea Urais. Wanadai Mbowe amekuwa akiwabeba wagombea ubunge wa chama chake kwa kuwapatia kila kitu tofauti na Lisu ambaye amekuwa hana uwezo hata wa kutengeneza mabango.
8. Mbowe anaaminika sana na wafadhili wa Chama wa ndani na nje ya Chama. Wafadhili hawa ndio wamekuwa angalau wanakipitisha Chama kwenye nyakati ngumu, viongozi wengi wa Chadema wanahisi siku Mbowe akiondoka Chadema na chama hicho kitajifia kwa kukosa fedha za kukiendesha.
9. Ndani ya Chadema wengi wanasema Mbowe anaangalia mbali sana kisiasa kuliko Lisu. Wanadai Mbowe anajua si Rahisi CCM kuachia dola kwenye mazingira ya Sasa, lakini Mbowe huwa anatengeneza mazingira ya Chadema ku-survive kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na chama kwa Ujumla. Hii ni tofauti na Lisu kuwa yeye anawaza kwenda ikulu tu na akiikosa anakimbia anakiacha chama kikiwa hakina chochote.
10. Viongozi wengi wa Chadema wanasema wazi wazi wapo huru zaidi kufanya kazi na Mbowe kuliko Lisu kwa kuwa Mbowe hana Roho mbaya, anaweza kuacha kula yeye lakini viongozi wa chini yake wakala kwanza. Wanadai pia Mbowe kila akimakiza ziara huitisha kikao cha tathimini kuangalia wapi wamekosea na wapi wanakwenda. Hili kwa Lisu huwa halifanyiki, yeye akimaliza mkutano gari humpeleka hotelini huku nje viongozi wa matawi, wilaya, Kanda na mikoa wakizurura kila mtu na njia yake.
Mkiwaona watu wanamwimbia Mbowe Tuvushe tuwe tunaelewa. Kweli huyu ni mwamba haswa…
Ole Mushi
0712702602