Ofisi ya CHADEMA Kata ya Ndato Wilayani Rungwe

Ofisi ya CHADEMA Kata ya Ndato Wilayani Rungwe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,374
Reaction score
289,486
FB_IMG_1677428785150.jpg


Wakati vyama vingine vya siasa vikipora majengo ya Umma na kuyafanya mali zao , ama kurithishwa majengo ya viongozi waliokufa na kuyapiga rangi , Hali ni tofauti kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Chadema imeamua kujenga ofisi zake yenyewe kuanzia ngazi ya chini kabisa , wanachama wake wameamua kujipapasa mifukoni na kununua viwanja na kujenga ofisi za kisasa.

Tuliwahi kuandika humu kwamba mpaka sasa chadema imejenga ofisi za kisasa 457 nchi nzima , Wajinga wakabisha , Sasa huu ni mfano halisi wa tunayoyaandika humu mara zote.

Leo Freeman Mbowe amepita kwenye kata hii akitokea Kyela, amejionea mwenyewe jitihada za Wanachama hao, na yeye akaguswa na kujipapasa kwenye Kombati yake na kutoa Ubani wa Laki 5 , Mungu amzidishie.

Amina
 
Huwa siamin sana katika Majengo Mazuri ya kifahari katika kuelezea Ubora wa Taasisi au Chama au Kikundi fulan .

Huwa naamini katika Misingi , Uadilifu, Uzalendo, Maono, uchapa kazi ,Kusimama haki n.k .... Tunaweza kufanya hayo hata kama hatuna Ofisi nzuri.

Nawapa mfano:

Kanisa la Roman Catholic, ndio wanaongoza Kwa kua na reserve kubwa ya Dhahabu ,Almas na Fedha za kutosha na Kua na Majengo ya Kanisa makubwaa, yalopambwa Kwa Dhahabu na mapanbo ,Majengo mazuriiii kwelikweli ya kupendeza kuliko Serikali yoyote Ile hapa Chini ya Jua.

Kanisa la Angilkana, Hawa ndo wanafuatia Mama Yao RC.


Ndugu msomaji wa komenti hii...huwezi amini hayo ndo Makanisa yaliyo kipaumbele kupigania kuhalalisha, Ushoga, mapenzi ya Jinsia Moja, kufirana Wizi wa Mali za masikin ( Mfano pale DRC Kongo) Kumkufuru Mungu, kunipa uungu na mambo mengine ya ovyo ovyoo
 
Mmeamua kuudanganya umma kwa kujibanza kwenye mjengo wa mtu, hapo naona nyumba ya vyumba 3,sebule, choo, jiko, bafu na stoo!
 
View attachment 2530948

Wakati vyama vingine vya siasa vikipora majengo ya Umma na kuyafanya mali zao , ama kurithishwa majengo ya viongozi waliokufa na kuyapiga rangi , Hali ni tofauti kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...
Ametoa ubani kwani kafa mtu kwenye ujenzi wa jengo. Hongera kwa wananchi kujitolea kujenga, lakini mabillioni ya ruzuku na makato ya wabunge mbona hatuoni yanafanya nini?
 
Huwa siamin sana katika Majengo Mazuri ya kifahari katika kuelezea Ubora wa Taasisi au Chama au Kikundi fulan ...
Bwana Carlos, nakuunga mkono mpaka hapo kabla ya mfano. Ila mfano wenyewe ni potofu wala sio kweli unachokisema.

Huo ni uzushi usiofaa, na unasambazwa na wachache wenye malengo na nia ovu ya kuchafua kanisa katoliki.

Kanisa (Katoliki), tuna amini kwamba, dhambi zote ni sawa, hakuna kubwa wala ndogo.

Hivyo wote watenda dhambi (mfano waongo, wezi, mashoga n.k) bado wana nafasi ya kutubu na kumrudia muumba.
 
View attachment 2530948

Wakati vyama vingine vya siasa vikipora majengo ya Umma na kuyafanya mali zao , ama kurithishwa majengo ya viongozi waliokufa na kuyapiga rangi , Hali ni tofauti kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...
Hili jengo nalijua.

Mmiliki pia namfahamu.

Lina Siri kubwa sana.

Mwenyekiti kadanganywa.

Siasa za kukurupuka ni mbaya sana.

Kabla hata hajafika Njombe mwenye nayo atakuwa keshaanza plastering.
 
Bwana Carlos, nakuunga mkono mpaka hapo kabla ya mfano. Ila mfano wenyewe ni potofu wala sio kweli unachokisema...
Upo sahihi dhambi ni dhambi ,ila Je wajua Kuna dhambi ambayo Mungu mwenyewe Kasema hatokaa kuisamehe hata kama aloitenda ataomba Msamaha na kutubu Kwa kujichanachana na wembe ??
 
Back
Top Bottom